Wanaume wanapitia crisis kubwa sana kwa sababu kuu 3.
1. Kuna wale wanataka mwanamke mwenye kipato ili amlee au kujitafutia ahueni ya maisha. Hapo ataoa binti kutoka familia yenye jina kubwa au yenye connections. Kuna wanaofanikiwa, lakini kuna wale wanakuja kugundua mambo siyo rahisi namna hiyo, anakuta na wale jamaa kule ukweni wanataka kuona una cha kuchangia siyo kubebwa bebwa tu. Ndo hao wanaishia kuwa na ndoa zimejaa ghadhabu maana ukweni wanakuona kama shamba boy tu.
2. Kuna wale wanataka mwanamke mwenye kipato yaani anayehustle, still kwa lengo la kujitafutia ahueni ya maisha, anamkuta binti ana nyumba, gari, mshahara mzuri anaona ok hapahapa. Most of the time mwanamke wa namna hiyo ataendana sana na mwanaume mtafutaji vilevile, hiyo combination ni unstoppable yaani wanafanikiwaga sana financial. Lakini wanaoenda pale kwa lengo la kutumia vya mwanamke ndiyo hao utakuta wanalalamika eti wanawake wenye hela wana kiburi, si kweli, ni vile wameshindwa kumeet standard za utafutaji za mwanamke, mwanamke huyu hana time ya kulea jitu vivu, kama ni ndoa hapo chali, wala si sababu ya mwanamke ni kwa sababu ya hili jamaa vivu lililotarajia easy ride.
3. Kuna wale wanaume hard working, amefanikiwa lakini anaamini anastahili mwanamke mzuri wa sura. Anasahau zile sifa nyingine kukamilisha maana halisi ya ndoa, humo ndani anakutana na bibie hajui kupika, hajui kufua, kila siku club , matunzo gharama juu, ndoa inazingua anaanza kulalamika wanawake hawafai. Anaoa kujifurahisha tamaa ya mwili na macho yake, na jamaa zake waone ameoa piai kali, siku ya harusi watu wamsifie bibi atakavyowaka, ujinga tu. Mwqnamke mrembo ni sehemu ndogo sana ya what defines maisha, mvuto kila mwanamke anao, ni vile utakavyomtunza na kumsupport na kumpa upendo.
In reality, oa mwanamke anayejitambua, atakayekuwa MSAIDIZI wako nawe ukiwa umeshikilia usukani. Biblia kwa mfano, imeweka hayo wazi, wanawake wanaofaa wako wengi sana, shida wqnaume wanakimbilia kwa matajiri au warembo halafu wanakuja kulia lia hapa. Kwa mfano, ukioa mwanamke anayetafuta nawe ukachangamka umewin big time, cha msingi heshima iwepo, strong women hawakubaliani na ujinga ujinga, utaachwa hapo ushangae. Uzuri wa mwanamke ni matunzo na upendo, hapo you can design her the way you want, unataka mwembamba au mnene you get one, na nuru usoni inakuja kutokana na amani moyoni. Vijana wengi wamefeli kabisa kulitatua hili fumbo, na wengine wanadiriki hata kutamani waliotengenezwa na wenzao. Young generation inapitia crisis kubwa sana kuliko wakati mwingine wowote. Ugumu wa maisha na kutamani yaliyo juu na kutokuwa tayari kuyakabili magumu kumewafanya hata wawe tayari kugeuzwa na wanaume wenzao kingono, mwanaume wa namna hii lini atakuja kutulia awe family guy alee mke na watoto, impossible. Hali ni mbaya sana.