Yes ni sahihi kabisa mkuundugu mtoa mda. Kama alikataa bila sababu ni sawa ila kuna ka upande ka pili usiombe kakukute. Hawa wadada kuna muda huwa wana vituko vya kiwanfo cha SGR. Mkuu umewahi kuambia hii mimba sio yako, au ukaulizwa una uhakika gani huyu mtoto ni wako? Halafu ukionesha reaction anakuambia nilikua nakutania tu au zilikua hasira tu. Mkuu hii isikie isikukute.
Mkusikia mwanaume kakataa mtoto muwe manafuatilia kwanza ndio mtoe hukumu, shida ni kwamba wabinti wanaaminika kirahisi sana na akijiliza ndio kabisaa, hata useme nini itachukua muda sana mwanaume kueleweka na vile huwa hatuongei ndio shida.
Nina mikasa miwili ya rafiki zangu wawili tofauti.
1. Wa kwanza alizaa na binti aliyemtolea mahari ila hawakufunga ndoa. Baada ya mtoto kukua binti alianza sarakasi za kufa mtu hio ilikua 2018, 19. Kufikia 2021 ilibidi waachane. Mwaka huu jamaa ndio kaja kufunguka vituko vya yule binti. Anasema amewa kuulizwa ana uhakika gani kama ile mimba ni yake? Ila jamaa alikua mvumilivu alifunika kombe na sasa kapata binti mwingine na mtoto yupo nae na bunti amekua muuza baa.