Kama Rais Samia ameshindwa kazi basi ajiuzulu maana hali inazidi kuwa mbaya

Natamani tuweke Siasa za Maji taka Pembeni Dr. Slaa ni Kiongozi Bora sana na mwenye msimamo. Bila msimamo watendaji wanapora Kwa Kasi Mali za umma
Huyu sasa hivi alee wajukuu, umri umeshamtupa mkono.
 
Ongeza kukosefu wa mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu! Itasababisha dada zetu wengi kujiuza wakiwa vyuoni! Huyu mama kashafeli tokea anaanza alikuwa na mihemko sana kana kwamba anaenda kuongoza Saccos!
Mbona wanajitapa kuwa pesa ya mkopo imeongezeka? Kwani hizo nyongeza anakulaga nani.
 
Yalipokuwa yakiuzwa 1500 jembe lilimtupa mkulima.?

Leo wanatuuzia 3600 kg, halafu wakienda kununua vifaa vya ujenzi wanakuta moto! Pembejeo rushwa kibao, huduma za hospital dawa hakuna na rushwa njenje!

Hapo bado jembe halijamtupa?
Mpaka watu wanafikia kwenye foleni ya kununua mbolea ya ruzuku
 
Heri ya leo Wakulima wana enjoy bei ya mazao imepanda.
Walanguzi ndiyo wana enjoy wala sio wakulima, middleman ndyo wanufaika wala si wakulima wanalima kwa taabu ilihali pembejeo wanazipata kwa gharama kubwa.
 
Sasa hao walamba asali wanamtetea ili asione matobo, kazi anayofanya ni kuchota maji nakuyamwagia katika chujio la nazi yeye akizani ni bakuri.
 
Inaelekea akikaa hapo ikulu ni kuwaza mwezi unaofuata aende nchi gani na asaini mkataba wa mwekezaji yupi.

Hakuna maamuzi yeyote ya maana yaliyofanyika mpaka sasa kuwanusuru wananchi na ugumu wa maisha.

Waitishe tu uchaguzi mapema.

Dah wewe jamaa nakumbuka miaka ya nyuma ulikuwa kichwa ngumu unatetea serikali hata pale wananchi wanapoumia.

Nini kimebadilika sasa?

Nikukumbushe; siku zote chagua upande wa wananchi, hata kama ni masikini na wanaonekana wajinga. Wananchi ndiyo sauti ya Mungu.
 
Hakika nakubaliana na wewe!
 
Hakika nakubaliana na wewe!

Huyo jamaa ana stroke.

Ukisoma michango yake ya nyuma utaona unafiki wake.

Alikuwa hana huruma hata kidogo na wananchi. Kazi kubwa ni kusifia na kutetea wanaume wanaojiita viongozi wa kiserikali.
 
Samia imeshamshinda. Sema tu ili mradi kunakucha hakukuchi wananchi wanajiishia tu.
 
Inaelekea akikaa hapo ikulu ni kuwaza mwezi unaofuata aende nchi gani na asaini mkataba wa mwekezaji yupi.

Hakuna maamuzi yeyote ya maana yaliyofanyika mpaka sasa kuwanusuru wananchi na ugumu wa maisha.

Waitishe tu uchaguzi mapema.
Kazi aliyoifanya Rais Samia Ni kubwa Sana katika muda huu mfupi aliokaa ikulu Kama Rais wetu, Amefungua milango mingi ya uwekezaji, Sasa wawekezaji wanazidi kufurika na kumiminika nchini Hali inayochochea ongezeko la fursa za ajira pamoja na mapato ya kikodi, kila secta imeimarika na inasonga mbele, wananchi Wana Imani kubwa na uongozi wa mama Samia maana wameona namna anavyowajali
 
Amebadilika baada ya mwendazake kwenda zake.
 

Huyo unayem-quote alikuwa mtetea serikali hata pale wananchi walipokuwa wanaumizwa.

Ni kama wewe tu.

Mwisho shetani amempiga na stroke.
 
Leo yupo kigamboni akizindua visima baada ya hapo anakwea mwewe tena sijui wapi? Walamba asali wameshamwandalia safari tayari!
Huku nyuma wanabaki wanakwangua mpaka nyusi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Sudan walimtoa Omar lisa kupanda kwa bei ya mkate tu, mambo madogo madogo kwa wananchi yanayochukuliwa simple na viongozi wa kiafrika, ndo huwa yanawagharimu!
 
Hakuna mtu anayemuonea, yeye ashughulikie haya matatizo sugu ili nchi isonge mbele na kama ameshindwa atuachie ofisi.
Mzee hiyo ofisi ni ngumu. Unakula na kulala na mafisi yanayokuzunguka. Sijui kama umefanya kazi serikalini ukaona mali za nchi zinavyoharibiwa. Ukiwasema tu maisha yako yanakuwa hatarini. mimi nilibidi nitoroke tu maana sikua na jinsi. Ku fight na hao mafisi ni ngumu maana ukizunguka huku wao wako kule wanachapa. Sana sana inabidi uwe na moyo wa kidi kteta kwa kiasi fulani.
 

Usiwe mlaini hivyo

Hao mafisadi ni wajinga wajinga tu.

Uwe Rais wa nchi halafu uogope mafisadi?

Are you serious?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…