Kama Rais Samia ameshindwa kazi basi ajiuzulu maana hali inazidi kuwa mbaya

Kama Rais Samia ameshindwa kazi basi ajiuzulu maana hali inazidi kuwa mbaya

Nimegundua wewe Ni Tapeli kutoka Chadema, mkulima gani asiye mpongeza na kumshukuru Rais Samia? Mkulima gani ambaye hajafaidika na jasho lake mwaka huu? Mkulima gani ambaye hajafurahishwa na utoaji wa Ruzuku na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea? Hao siyo wakulima Bali Ni mkusanyiko wa wapiga soga na wababaishaji kutoka hapo ufipa makao makuu ya kutafuna Ruzuku na michango ya akina Sabodo na wadau wengineo

Wakulima wa Tanzania kwa umoja wao wameikataa serikali goigoi.

Wanasema serikali ya Samia na genge lake haina tija kwao.

Sasa hivi kila mkulima anafanya kazi kwa bidii, wengi wanatunza pesa Ili wachimbe visima, wanunue sola lakini pia wanashirikiana kwa umoja wao kupata masoko ya mazao bila kutengemea serikali.

Asilimia 100% ya wakulima wameikataa serikali ya Samia. Kifupi hawana time nayo.
 
Wanadai vifurushi ni ofa za biashara wakitaka wataviondoa
 
1. Umeme umekuwa bidhaa adimu kwenye maeneo mengi huku kila siku kukiwa na matamko ya megawati.

2. Upatikanaji wa maji safi na salama imekuwa ni anasa maeneo mengi na hasa katika jiji la Dar es salaam.

3. Vifurushi vya intaneti vinapandishwa kadri watoa huduma wanavyojisikia ikiwa ni pamoja na wizi wa vifurushi kwa kuvimaliza mapema.

4. Wabunge wasiokuwa na chama na hata hawajui nani aliwateua bado wanaendelea kukaa bungeni na kulipwa kodi za watanzania.

5. Uzembe wa serikali katika kuimarisha mfumo wa kukabiliana na majanga. Hili jambo limejirudia sana na watu wanakufa bila msaada.

6. Mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa mbalimbali hasa kwenye chakula, usafirishaji na ujenzi.

7. Mizaha juu ya upatikanaji wa katiba mpya. Sheria iliyotungwa kukamilisha upatikanaji wa katiba mpya inapuuzwa.

8. Ukosefu wa ajira na mitaji kwa vijana kumepelekea udhalilishaji wa sekta ya elimu na kumomonyoka kwa maadili.
Mtanikumbuka
 
Miaka mitano ya utawala wake kulikuwa hakuna ajira,kapora uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020,Kaingiza wale wanawake wahuni 19 Bungeni,katusababishia majanga mengi leo Mama Samiah anahangaika namna ya kuboresha nchi iliyoharibiwa na yule Kibaraka wa shetani.
Anaboresha nn wakati anaharibu kila alichotengenezewa? Na jibu mnalo mana anahangaika km Anataka kutaga kila mahali hapashikiki na bado kantre haipoi haiboi mpka atasanda[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ongeza kukosefu wa mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu! Itasababisha dada zetu wengi kujiuza wakiwa vyuoni! Huyu mama kashafeli tokea anaanza alikuwa na mihemko sana kana kwamba anaenda kuongoza Saccos!
Ongeza hapo , kuwachagua akina Mulamula wengi wadogo na uwezo wa kufikiri na kuchapa kazi
 
Ongeza hapo, kwenda kwenye mikutano ya wananchi ( hadhara)bila kutoa nafadi ya kusikiliza kero moja kwa moja kutoka kwa wananchi.
 
Rais Samia Ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kujivunia tulipo na kutembea kifua mbele, kwa namna alivyofanya kazi Anastahili kuungwa mkono na kila mtanzania
Hv wewe ni mwanaume na una mke kabisa nyumbani anajisifia nae kaolewa??? Frankly akili yako Inawezekana ina matatizo mana hata uchawa huu ni ukunguni khaa
 
Hakuna awamu iliyofanya mabaya ya kutisha kama awamu ya tano.
Amesahau ile awamu mpaka ukaibuka usemi wa vyuma vimekaza ,mi kwangu ccm ninaona kama maruhani tu ,ccm ni ile ile na mentality yao ni ile ile ,hamna nafuu
 
Kipindi hicho hakukuwa na haja ya kufanya maandamano.Awamu hiyo ilifanya mazuri yaliyowasaidia wananchi kupata mahitaji yao kiurahisi tofauti na sasa kila kitu bei juu
Ule usemi wa vyuma vimekaza ulianzia awamu ipi ?
 
Hivi mnaona dar slam ndiyo Tanzania nzima? Yaani maji yakose dar basi wote tulie kuna maeneo umeme unakatika kwa nadra sana, yaani mtu unaweza kumaliza hata miezi miwili umeme hujawahi kukatika hata siku moja, ikitokea ukakata hata dk haiwezi kuisha umesharudi, kuna maeneo tangu dunia iumbwe hayajawahi kuona umeme, kuna watu unaposema internet haelewi unazungumzia nini, kuna jamii vizazi na vizazi hawajawahi kutegemea ajira za serikali.....kuna maeneo mtu hajawahi kuona ukame au ukosefu wa maji uliokithiri yaani kuna mito , madimbwi na mvua zinapiga kwa wakati kila mwaka..... hivyo hoja zako si nzito kiasi kumfanya Rais wa Taifa zima kujiondoa madarakani bali uanze na viongozi wa ngazi za chini ambao wanaishia kwenye eneo ambalo lina changamoto hizo
Ona limsukule hili ,Yaani akili za hivi ni nyingi nchi hii ndio maana ccm inazidi kutawala aiseee ,Dah !
Kwa hiyo umasikini na poor living conditions ni sifa sasa hivi au sio ?
 
Nyinyi haiwezekani kuandamana bila kikomo, sababu ni kwamba - mlo wa siku lazima utafutwe siku hiyo hiyo (daiwaka)! Ukienda maandamanoni, ujuwe siku hiyo huli.
Maana wengi wetu ni vibarua. Wachache wenye kazi za kudumu wanamsaporti huyo mtawala!
Taifa hili linasikitisha sana , taifa la vibarua na machinga
 
Back
Top Bottom