Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Nimekuelewa
 
Acha porojo

Nitajie shirika moja la serikali lililofanya biashara na likafanikiwa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 

Una point ya msingi - kuwa serikali iondoe matatizo yanayosababisha kushindwa kwa hii miradi! Bahati mbaya hukutaja hata jambo moja unalodhani ni kikwazo. Lakini tukiangalia miradi mingine kama viwanda ya Nyerere, ATC, reli ya kati, TAZARA, bandari, mabasi na kadhali - ilishindwa!!! Sababu kubwa sio kukosekana kwa wataalamu, vifaa, uongozi nk - sababu ni hii - ustahamilivu wa udhaifu ili kufaidisha siasa (patience for failure/mismanagament). Serikali imekuwa ikikwepa hata kuonesha tu miradi hii inashindwa (rejea magawio ya ATC, TTCL na wengine). Ustahamilivu wa kushindwa umekuwa mkubwa mno na wa maana ili kufaidisha siasa za serikali. Njia nzuri ni kuiondoa serikali katika uendeshaji ili stahamilvu hiyo iishe. Kuiondoa serikali simaanishi wayauze au wabinafsishe. Ninamaanisha wawe sehemu ya umiliki kama ambavyo watakuwa wamiliki wengine wenye hisa! Serikali anaweza kuwa mmiliki mkubwa tu (51%) na wana hisa wakawa na 49%. Ni hawa 49% ndio watakaoendesha mashirika haya kwa ufanisi!! Ndio hao watakataa hasara. Ndio hao hawatataka faida za kisiasa ziharibu uwekezaji wao. Air Rwanda kwa mfano inamilikiwa na Rwanda 51% na Qatar Airways 49%. Baada ya miaka minvi ya hasara, sasa Rwanda sio mwendeshaji wa shirika tena. Inaitwa PPP (public private partnership).

Mambo haya yamejaribiwa na kufanikiwa sehemu mbalimbali duniani. Uwekezaji wa kiraia ndio uwekezaji salama unaoweza kubakiza sehemu kubwa ya faida ndani ya nchi!!

Faida za kisiasa ni hasara kwa uchumi!! Tuwezeshe raia kuachana na siasa na wawe wazalishaji. Serikali ibaki na kazi ya kukusanya kodi, kutunga sheria na kudhibiti shughuli za hao raia.
 

Website yao inasema London underground asilimia 41% ya matumizi yao yanatoka kwa walipa kodi. Na wanasema mapato yao wanatumia kuiendesha hiyo kampuni na bado hayatoshi. Ina maana inaendeshwa kwa hasara ila kwa sababu ni huduma wapiga kura wanaiona muhimu serikali inaendelea kuisaidia.

 
Mkuu nimepata shida kidogo kukuelewa huko juu kuhusu "ustahimilivu..."; kidogo nibwage manyanga chini!

Unazungumzia umiliki, kama huo wa Rwanda? Mbona umeishia hapo mkuu, umejaribu kuangalia "The Pride of Africa" wanavyofanya?

Hata kama hutaki kuangalia mfano huo na mingi mingine huko nje ya mipaka yetu, mbona unajisahaulisha kirahisi rahisi..., hapa hapa nyumbani una uhakika hapajawahi kuwepo na mpango kama huo, tena sio katika shirika hilo hilo la ATC pekee, na mashirika mengine kibao yaliyowahi kuwa na washiriki na serikali kubaki na hisa kadhaa. Hivi unadhani pendekezo lako ni jipya?

Haya, sote tunajua, at least nategemea kuwa unajua: hivi ni nani anayemiliki na kuendesha Ethiopian?

Haya mambo tunayajadili hapa wakati mwingine tukitumia hisia tu tunazozipata toka kwa watu na hatuyafikiri kwa kina tukaangalia hasa ni kwa nini serikali ijihusishe kwenye baadhi ya haya mambo.

Unajua, mimi nitakubaliana nawe moja kwa moja kuhusu kujiondoa kwa serikali kabisaaaa kwenye haya mambo iwapo kama hawa binafsi tunaowalilia watatoa huduma safi kabisa na wananchi wafaidike na huduma hizo.

Lakini historia inaonyesha, sio hapa pekee, bali na kwingine pia, kuna mambo ambayo ni lazima serikali iyabebe hata kama ni kwa mzigo mkubwa. Tulikuwa na IPTL hapa iliyotupatia taabu kweli kweli. Mara hii tumejifanya kusahau? India hawakuja hapa na kutaka kuua kabisa reli? Mifano ipo chungu nzima, na hiyo si pekee hata kama tungesema akina Mo waendeshe mashirika haya, kuna athari chungu nzima ninazoweza kueleza ni jinsi gani bado tutakuwa tumekwama.
 
Sina hakika kama British Airways ni tofauti na hao, na hata BBC!
 
Ebu onesha hiyo sehemu waliposema hayo.

Nilichoona mimi mapato yao ni service fees, government grants (mikopo ya serikali ya kibiashara yenye riba nafuu), wanakopa bank, paid advertising and other toll charges za barabara zilizochini ya jiji.

I doubt kama serikali itatumia kiasi icho cha pesa kuendesha underground, be it ni sensitive kwa uchumi wao.

The mere fact wanakwambia 80% ya profit wanarudisha kwenye kuboresha miundombinu ina maana hiyo profitable organisation isiyotegemea government subsidies.
 

Mbona umeshaiona hiyo sehemu tayari? Labda kama huoni kwamba government grants na mikopo ya European Investment Bank vyote ni hela za walipa kodi. Hela za serikali ni hela za walipa kodi.
 
Mbona umeshaiona hiyo sehemu tayari? Labda kama huoni kwamba government grants na mikopo ya European Investment Bank vyote ni hela za walipa kodi. Hela za serikali ni hela za walipa kodi.
Grant ni mkopo nafuu unaotolewa na serikali na unalipwa; nani kakwambia ni hela ya bure hiyo.

Fungua hiyo statement nenda kaangalie kwenye notes za current na non current liabilities utaona grants ni madeni.
 
Ethiopia Airlines ilikuwa Shirika pekee la ndege la Ethiopia kati ya 1950 hadi 2002. Unahitaji kuwa TANESCO ndio ushindwe kujijenga na uendelee kupata hasara ukiwa mwenyewe sokoni.

Usiongelee IPTL aliyekuwa supplier tu na ambaye ni dili la wanasiasa.Ongelea TANESCO ambayo haijawahi kutoka mikononi mwa serikali, haijwahi kupata faida na huduma zake ni tia maji tia maji tu siku zote. Na vigogo wa serikali hawataki kusikia suala la sekta binafsi kwenye umeme!!!

Kama una mashaka na Huduma kutoka kampuni binafsi nenda Agha Khan, Regency, Kairuki. Nenda Feza, St Mary's, ISM, St Anthony. Angalia wanafunzi wanaotoka shule za kata na hao kutoka st st, Angalia usafiri wa dalaldala za binafsi ulivyo na uhakika kuliko hizo daladala za mwendokasi, Angalia usafiri wa mikoani kwa mabasi ambako serikali haina hata basi moja la abiria.

Serikali iliwaindoa Maxmalipo kwenye mwendokasi,wakati huu tiketi zinachanwa na huduma ya kadi imekufa. Sasa hivi ni miaka miwili hilo dude lao la E-government bado liko linajenga mfumo wa kielectronic.Two damn years!!!.
 
BBC sio shirika la kutengeneza faida. Linaendeshewa kwa license fee ambayo ni kama kodi inayotozwa kwa kila mtu anayemiliki TV Uingereza.

British Airways ni shirika binafsi lilo kwenye soko la hisa la Uingereza.
Sina hakika kama British Airways ni tofauti na hao, na hata BBC!
 
Kusema 80% ya profit wanarudisha kwenye kuboresha miundombinu haina maana hiyo ni profitable organisation isiyotegemea government subsidies ina maana hiyo ni sera yao pale wanapopata faida. Sio ajabu ukakuta aini hiyo ya maneno hata TANESCO au ATCL kwenu.
 
Sekta binafsi ndio solution sababu serikali kila kitu ni siasa hivyo biashara hawaziwezi.

Wauze hiyo company.
Kweli kabisa ikishindikana basi ni serikali kuwa na hisa tu kwenye shirika kuliko kuendelea kula hasara, manake kwa nchi zetu especially za Africa, mara nyingi watu wafanyao kwenye mashirika yetu yanayoendeshwa na serikali, huwa hawana uchungu wowote na pesa inayotumiwa na kama shirika linajiendesha kwa ufanisi au kwa hasara, kwani wafanyakazi wao alimradi wanakuwa na uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi na kuangalia wapi penye upenyo wa ufisadi wao wachote basi... manake wanaona btw ni mali ya umma tofauti na kama shirika lingekuwa linaendeshwa na private entities, ambao wanakuwa serious kuhakikisha linakuwa na tija...tofauti kabisa na mashirika yanaendeshwa na serikali zetu za kiafrika, ambazo zinakuwa zinaingiza siasa na kutotumia watu sahihi, kwenye mambo ya kiutendaji, na hata ktk mambo mengine ya msingi ambayo yanahitaji utaalamu uliobobea kwenye eneo husika. Mifano michache ya matatizo kama haya, nimeyaona kwa mashirika ya ndege ya huku kusini mwaka Afrika, ya SAA na pia shirika la ndege la Air Namibia ambayo kwa muda mrefu, yaliendelea kuwa ' bail out' kila mwaka kwa pesa za serikali pamoja na kuingiza hasara miaka mfululizo, kwa sababu nyingi zikiwepo za kisiasa na mashirika kuingiliwa na serikali kwenye uendeshaji....na tayari kama Air Namibia bunge na serikali wamenyoosha mikono na limevunjwa( liquidated) na huku South Africa ,SAA inapumulia mashine... Mie ninashauri nchi zetu bado ni maskini, na tujaribu tuwe na priorities na kufanya mambo ambayo tulio na uwezo nayo kwa kipindi husika.... kazi iendelee.
 
Ni majanga,Lisu alisema miradi ya Magu ni kichefuchefu nyie subirini mda utasema
 
Hayo yalifanywa kwenye TRC ,kuna tija ilipatikana?

Wakati wa JK alijaribu kwa kuleta watanzania waliokuwa nje ya nchi kwenye sekta binafsi kama TIC,NSSF,NHC nk nk walijitahidi lakini mwendazake alivyokuja akadai hawezi lipa salary kubwa na hadi leo hii mashirika yamejifia huko

Tukubali serikali iwe na hisa tuu ila shughuli za uendeshaji zifanywe na sekta binafsi tena kipaombele iwe watu wa ndani ndio wawe investors
 
Hakuna mtu ataweka jita kwenye kitu ambacho hakifaidishi yeye binafsi.

Kwenye uchumi wa soko kuna dhana ya kwamba mtu anavyojibidiisha kujinufaisha binafsi,in turn anafaidisha na wengine third part
 
Graduate wa master au degree hajawahi fanya biashara na hana exposure anaanzia wapi kuwa mbujifu?

Ukinolewa kutoka sekta binafsi ukaja sekta ya umma ndio unaweza kuwa mbunifu,,

Nimewahi fanya Kazi sekta binafsi kwa miaka 2 tena kwenye kampuni ya Kenya hapa hapa Bongo uchumi ulivyovurugika ikafungasha nikatafuta Kazi serikali,to be honest huku serikali no one cares ni mwendo wa kufukuzia posho tuu na kufanya Kazi kwa mazoea, wanasema sio Kazi ya baba yako chukua chako sepa na vile mishahara ni midogo

Pia tatizo ni ajira za kudumu bora zingekuwa za mkataba ingeleta tija kidogo
 




Umeona hapo ☝️mwaka jana walitengeneza faida ya £671.2 million.

Yes kuwekeza 80% back ni sera yao kwa sababu kampuni ni 100% mali ya serikali hawana interest na dividend bali kutoa merit good zenye ubora na kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Ndio maana wanarudisha kwenye kujiboresha.


Tazama hapo ☝️ juu tena utaona aina ya grants wanazopata zifuatilie zote kupitia google utaona ni za kulipa. Kuwa mali ya serikali aina maana wanaendeshwa kwa subsidies.

Grants ni sources of finances za kawaida sana nchi za wenzetu, hata taasisi binafsi zinapata provided serikali inataka kusaidia sector fulani, wanao qualify kwenye hiyo industry can apply.

Acha kumsikiliza huyo jamaa alieni quote anaunga unga tu ubishi wala ajapitia hiyo statement yenyewe aliyoileta.

PS. British Airways sio mali ya UK kwa sasa inamilikiwa na ‘International Airline Group’ (AIG) shirika lilisojaliwa Spain.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…