Mkuu nimepata shida kidogo kukuelewa huko juu kuhusu "ustahimilivu..."; kidogo nibwage manyanga chini!
Unazungumzia umiliki, kama huo wa Rwanda? Mbona umeishia hapo mkuu, umejaribu kuangalia "The Pride of Africa" wanavyofanya?
Hata kama hutaki kuangalia mfano huo na mingi mingine huko nje ya mipaka yetu, mbona unajisahaulisha kirahisi rahisi..., hapa hapa nyumbani una uhakika hapajawahi kuwepo na mpango kama huo, tena sio katika shirika hilo hilo la ATC pekee, na mashirika mengine kibao yaliyowahi kuwa na washiriki na serikali kubaki na hisa kadhaa. Hivi unadhani pendekezo lako ni jipya?
Haya, sote tunajua, at least nategemea kuwa unajua: hivi ni nani anayemiliki na kuendesha Ethiopian?
Haya mambo tunayajadili hapa wakati mwingine tukitumia hisia tu tunazozipata toka kwa watu na hatuyafikiri kwa kina tukaangalia hasa ni kwa nini serikali ijihusishe kwenye baadhi ya haya mambo.
Unajua, mimi nitakubaliana nawe moja kwa moja kuhusu kujiondoa kwa serikali kabisaaaa kwenye haya mambo iwapo kama hawa binafsi tunaowalilia watatoa huduma safi kabisa na wananchi wafaidike na huduma hizo.
Lakini historia inaonyesha, sio hapa pekee, bali na kwingine pia, kuna mambo ambayo ni lazima serikali iyabebe hata kama ni kwa mzigo mkubwa. Tulikuwa na IPTL hapa iliyotupatia taabu kweli kweli. Mara hii tumejifanya kusahau? India hawakuja hapa na kutaka kuua kabisa reli? Mifano ipo chungu nzima, na hiyo si pekee hata kama tungesema akina Mo waendeshe mashirika haya, kuna athari chungu nzima ninazoweza kueleza ni jinsi gani bado tutakuwa tumekwama.