Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Siyo comment yangu Bora,

Ila usiingilie taratibu za kijeshi,unadhani ni vyema kuonesha silaha zako wakati humjui adui yako ni nani
Kweli hakuna mnalojua vijana.

Aliyekwambia jeshi halitambui adui yake ni nani? Umeshawahi jiuliza kwanini Mkuu wa Majeshi anatokea Jeshini? Sio kwamba eti wao ndo wana silaha nzito tu pekee, hapana kaka.

Wao ndo wana kitengo maalumu cha kuweza kutambua nani ni threat ktk Taifa. Jeshi lina kitengo chake kinachojitegemea kabisa cha Intelligenc, chenyewe kimejikita hapo tu na wala hawawategemei sana Usalama wa Taifa.

Hawa hata leo tukitaka kuzipiga na Uganda, wao wanajua tunaanzia wapi na tutaishia wapi, wao wanaweza wakajua Idad ya silaha zao na ukubwa wake n.k

Narudia tena, sio kila jambo tunaweza zungumza humu. Ila eleweni tu kuwa hatuna jeshi lenye sifa ambazo tunawapa.
 
Upo sawa zana hizo za vita ni za enzi za USSR,lakini ukae ukijua Tanzania hatuna potential enemy,tangu utawala uliokuwa wenye sera za ubaguzi wa rangi kule Afrika ya kusini ulipoachia madaraka,tangia hapo nchi ya Tanzania haina adui wa moja kwa moja ambaye unaweza kumyoshea kidole kwamba huyu hapa,kwa hiyo hakuna hoja ya msingi ya kutumia mabilioni ya fedha za wakulima na walipa Kodi,kununua vifaa vya vita ambavyo vitakuwa vinaoza taratibu kwenye mabohari ya jeshi,hebu google uone ndege moja ya kivita mfano F16 inauzwa sh ngapi halafu jaribu kucompare hiyo hela na gharama za kujenga shule na kununua madawati,au gharama za kujenga vituo vya afya na kununua vifaa vya afya.
Mfumo kama wa nchi za India na Pakistan wa kuwa na jeshi lenye vifaa vya gharama kubwa sana vyenye teknolojia za Hali ya juu,wakati ambapo hakuna vita yeyote ni ukichaa ulio wazi kabisa.
 
Mzee mambo ya watu kupiganisha yalishapitwa na wakati. Sasa hivi ni technology ndio inapigana. Achana na mawazo ya kijima ya Nduli Idd Amin Dadaa.
Sawa na hiyo vita ya Afghanistan na Wamarekani nayo ilikuwa wakati gani, wakati wa ujima!? Mbona tunawaona wakienda kwa miguu bila ku apply hiyo technology? Are you saying INFANTRY SOLDIERS hawana kazi siku hizi? Fikiria upya huo ni ujima au ni nini!?
 
Bado tupo kizamani mno. Mavifua ya kutishia waandamanaji.
 
Huo ni utaratibu wa kawaida nyakati kama hizi, hata hivyo silaha unazo onesha SI kwa ajili ya kupigana bali ni kwa ajili ya kuonesha utayari wako likitokea la kutokea! Hata hivyo you do not show all that you have au siyo!?
Kwa kutazama tu parade ya silaha zako, watu wanajua what you have, what you thinking.

Kuna watu wapo trained ktk intelligenc kumsoma mpinzani kwa style hiyo.
 
Infantry ni kwaajili ya kisafisha baada ya technology kufanya Kazi yake.
 
Hivi unafikiri Kenya,Uganda na Rwanda hawajui silaha tulizonazo hadi wasubiri 9/12 ndio wazione?
Tena hao Rwanda ndo balaa, bora mwendazake alikwenda tu.
 
Ni kweli nalijua hilo lakini hapa africa mataifa yenye silaha za kisasa yzfiki hata matano pia kumbuka silaha huwa zinaboreshwa utendaji kazi wake
Na hazijawa obsolete bradha bado ziko kazini kama ilivyo AK 47! Hiyo ni ya 1947 lakini bado ni moto wa kuotea mbali hata hizo za kisasa kama UZI ya Israeli na nyingine nyingi hazioni ndani!
 
Hivi ulishasikia wapi vita vikaishia angani ubora wa jeshi letu uko ardini mkuu

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
Kasome kuhusu Highway of Death pale jeshi la Saddam Hussein linafanya evacuation kutoka Kuwait ndio utajua umuhimu wa jeshi la anga. Kunakuwa na air denial na naval blockade ila hutosikia wanahangaika kuzuia ground movement mwanzoni. Jeshi la ardhini rahisi kuzuia likiwa halina air cover
 
Hizo cougar zilinunuliwa toka enzi za JK.

Zitatokea figisufigisu, nikisema hivi nadhan unaelewa mzee mwenzangu, utawala wa JK uligubikwa na mambo hayo.

Zoezi likasimamishwa, wakasubir ngoma ipoe, ilipopoa ndo wakazileta. So ni enzi za JK manunuzi ndipo yalipofanyika ya hizi Cougar, na zilikuwa 6.
 
Zamani vita ilihitaji watu wazalendo, tulimzid jamaa hapo. Sasa hivi mambo yamebadilika mkuu.
 
Mzee hata manati inaua. But ilitumika kipindi cha ujima. Huwezi ku display manati kama silaha yako.

Leo hii tunaoneshana madaraja, kweli!?
Kwa hiyo unasema silaha zote walizoonesha
Ni za kizamani

Ova
 
Amka toka usingizi! Hakuna ndege wala drone ilishawahi kupaa kwenye anga la Israel ukiachana na Egypt walipoingia jangwa la Sinai kwa ghafla na wakitegemea cover ya anti aircraft missiles kutoka kwenye mainland yao. Sio drone wala jet fighter, Israel haijashambuliwa kwa anga na yeyote.

Iran tusimseme hapa kwanza una tabia ya kuleta dini kwenye hizi mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…