Kama sio Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Watanzania tulikuwa tunapigwa na kitu kizito sana na DP World

Kama sio Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Watanzania tulikuwa tunapigwa na kitu kizito sana na DP World

Hiyo sio hoja mkuu, kwa maana nyie ndio mliodai ya kwamba sasa wageni waondoke na mjiendeshe wenyewe miaka ya 1960s ndio mkaita harakati za uhuru. Kiko wapi sasa?? Mliwafukuza ila sasa mnaomba warudi??

Alafu kwanini iwe bandari tu. Mbona hata TRA hakuna ufanisi na hamjampa mwekezaji??
Hao hao waliotutawala wanawapokea wawekezaji wa bandari, ndio utambue sasa kuwa dunia ina mabadiliko yake na siku zote yanaanzia kwenye maono binafsi.

Kule Dubai yalikuwa maono ya rais wao Al Makhtoum, na mpaka kufikia alipo hivi sasa kuna watu waliuliwa, hiyo ni gharama ya kuweza kufanikisha maono yake.

Bandari ni muhimu kwa maana ya huyo muendeshaji ndio mmiliki pia wa mizigo iliyopo huko Congo na Rwanda hivyo anaitoka huko kupitia reli ya SGR na kuifikisha bandarini halafu anaipandisha kwenye meli zake kuipeleka huko kwa wateja.

Inabidi kuielewa maana ya kisasa ya bandari ili uweze kuielewa biashara hii.
 
Rejea kichwa cha habari.........isije ikawa walikuwa wapigwe kwenye kiini cha makalio🙂🙂🙂aka...kijambio🤪🤪🤪
 
Binafsi sijaona kokote jumuiya ya kanisa langu likiongea chochote katika suala hili, imenipa kunitia nguvu sana kwa kuona NAMNA TEC walivyofanya....nataman kuwa RC....napenda watu STRONG!
 
Ndugu zangu Watanzania wale madingi wa Katoliki ni miamba sana, wamemaliza ujinga wa DPW.

Muda si mrefu Mama atatema bungo. Tender hiyo, wenye mbavu waipambanie. Ile sheria ya maliasili waliyotaka kubadilisha ili mikataba isipelekwe bungeni juzi nimeona kamati ya bunge ikipinga mapendekezo yote ya serikali. So far ile sheria haijaguswa.

Kama sio msuli wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC tungepigwa na kitu kizito vibaya sana.

Ahsanteni Maaskofu wa Katoliki.
Ikiwa itatokea kama mnenaji alivyo malizia, basi Spika na Bunge lake wamepoteza hadhi ya kuwa mjengoni, na kwa hiari yao waondoke, na pili Mahakama Kuu nayo ijitahmini na watupe mrejesho Kama wanaona ni haki nao kuendelea kukaa na kutafsiri Sheria.

Kama hayo yote yakifungiwa macho, basi lessons za Gabon, Niger nk ziwe options kwetu pia.
 
Wengi wanaoandika humu JF hawana biashara yoyote pale bandarini, hawajui wale wenye kusafirisha mizigo wanakutana na kero zipi katika michakato ya shughuli wanazofanya.
Hatukatai KERO zipo lukuki, kinachopingwa na wataaalam wetu kina shivji jaji walioba na wataaalam wengi wa sheria za mikataba ni baadhi ya masharti ni mabaya Kwa mno Kwa nchi, hatupingi uwekezaji tunahitaji mno ila usiwe kitanzi Kwa nchi kama kesi ambazo Tanzania inashindwa na kulipa Kila Leo
 
Hivi nchi yetu ina Wabunge kweli?
Wabunge wanao ishauri Serikali na kuisimamia.
Wabunge wanageuka kuwa Machawa wa Kiongozi.
Nchi za Kiafrika zitaendeleaje kama hali ndio hii.
Kila mtu lazima awe Chawa wa Mama.
Tuupige vita sana Umaskini.
 
Hivi nchi yetu ina Wabunge kweli?
Wabunge wanao ishauri Serikali na kuisimamia.
Wabunge wanageuka kuwa Machawa wa Kiongozi.
Nchi za Kiafrika zitaendeleaje kama hali ndio hii.
Kila mtu lazima awe Chawa wa Mama.
Tuupige vita sana Umaskini.
Utapigaje vita umasikini wakati unashinda kwenye mitandao?
 
Ndugu zangu Watanzania wale madingi wa Katoliki ni miamba sana, wamemaliza ujinga wa DPW.
Mkuu Mwande, Mwande na Mndewa, kitu ambacho kinafanyika kwa process, wakati process inaendelea, usijipe matumaini hewa kuwa TEC wamemaliza kazi!, walichofanya TEC ni kutimiza tuu wajibu wao kwa kutoa maoni yao kuhusu DPW na Bandari zetu, maoni hayo yatachakatwa na ama ni kweli yakasaidia, ama yakapuuzwa!. The process still goes on, it's not over yet until it's over!. Kwanza kuhusu ule waraka Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? hivyo umepuuzwa!. Kwa kukusaidia tuu, ni ukae ukijua mchakato wa DPW na Bandari zetu unaendelea! Baada ya IGA ya DPW na Bandari zetu, licha ya mapungufu, HGA yake inakuja. Ombi kwa Serikali yetu sikivu, tunaomba Maximum Transparency kwenye HGA
P
 
Back
Top Bottom