Kama tunaaminishwa kuwa Mungu hakosei inakuwaje hakuna kiumbe mkamilifu chini ya jua?

Kwa biology yangu ya form 2 mkondo B.

Mule ndani ya pua katengeneza vinyweleo vya aina zaidi ya 10 vyenye uwezo wa ajabu wa kuchuja vumbi kwa ufanisi wa hali ya juu zaidi na haliwezi kufikia na kudhuru ubongo. Huu ni ushindi mkubwa maana alijua vumbi litamsumbua binadamu.

He is still the best designer ever.
 
Labda ungeweka bayana kati ya vitu vipi alivyo zungumza(maana ni vingi kazungumza)

Ambavyo wewe labda unahitaji uhakika kwavyo.
 
Best designer wakati viumbe vyake ni vidhaifu kupitiliza? Baada ya kuumba alisema"tazama kila kilichoumbwa ni chema", all of a sudden hicho kitu chema kimekuwa dhaifu kuliko maelezo.
Je wewe Eli79 unajiona upo mdhaifu?Hufurahii kazi ya mungu katika kukuumba wewe? Ulitamani uumbwaje ili umtukuze Mungu?
 
Labda ungeweka bayana kati ya vitu vipi alivyo zungumza(maana ni vingi kazungumza)

Ambavyo wewe labda unahitaji uhakika kwavyo.
TENA ZAIDI ZAIDI NI UKUU NA UPENDO
 
Mungu ni Perfect wala hakosei hiyo misemo uliyoweka ni ya kibinadamu tu.

Mungu hafi kama ilivyo kwa binadamu wengine.

Ni kama alivyokua binadamu wa kawaida Elia na Enock kwani anaenda Mbinguni bila kosa.

Ni kwamba ni mpango wa Mungu usitende dhambi ila kwa kua miili yetu hii mara nyingi ipo kinyume na matendo ya Mungu.

Nimalizie kama walivyokua hao kina Enock na hata leo wapo hapa duniani ni Kusali kila siku kila saa.
 
Binadamu hawajakamilika
Ndiyo awajakamilika
Mungu alvotaka kutuumba sisi hivi ingekuwaje binadamu kama. Mngepewa ukamilifu? Hali hii amjapewa mnafanya balaa duniani?

Kutikamilika kwako n kwamba dhaifu umeumbiwa ule na ukikosa kula utakufa, umeumbiwa maradhi hata ujilinde vp lazma uumwe na ajakuacha bure ukiwa unaumwa mungu anakupunguzia madhambi yako wkt uko kitandani,

Umeumbiwa usingizi ulale na uwez kukosa kulala maishan mwako.

Pia ili ujue pia ujakamilika kweli hakuna alokamilidha even maisha ya hapa duniani.

Mungu hakosoi wala ajakosea ametaka kukuumba ww kichaaaa unayemjaji hapa ulimwenguni ili kuonesha yeye n mjuz wa yalvofcha na ya dhahiri...

Leo unamjaji pumbavu go to hell
 
God is divine energy.. Na energy ina nature moja ...energy according to the greatest scientist Albert Einstein. Sayansi inakiri "energy can neither be created nor destroyed it can only be transferred from one source into another source"

We are human being.. We are energy too..we have our bigger source. God.

He never slumber.

God will never die!
 
Nakujibu kiufupi na kirahisi,

ULICHOOANDIKA NA UNACHOULIZA HAKIPO NA HAKITA KAA KIPATIKANE.

KUKOSEA AU KUTOKUKOSEA KWA MUNGU HAKUJULIKANI NA BINADAMU.

My take, wanafilosophia na teolojia kwenye metaphysics inasema MUNGU HAFIKIRI/NOT REASONING (GOD IS IRRATIONAL).
 
Mkuu umemjibu vyema sana!
 
Binadamu aliyekamilika ni yule mwenye mapungufu mkuu
ukiona binadamu hana mapungufu ujue huyo hajakamilika
na binadamu asiye na mapungufu ambaye hajakamilika
bado kutokea......
 
Duuuh! Bahati mbaya sina Logical Reasing ningechangia.
 
Mungu amekuumba wewe katika mfano wake yeye na si katika matendo yake yeye, Mungu hakumuumba binadamu na matendo, matendo ni utashi binafsi na hapo ndipo tusemapo hakuna binadamu aliyekamilika, maneno haya husemwa na binadamu si Mungu. Binadamu alipoumbwa aliumbwa amekamilika kwa viungo vyake jinsi vilivyo kwa wakati husika, lakini pia tulipewa mamlaka ya kuamua jema na baya ili tuitawale dunia na vilivyomo pia tumuabudu yeye aliyetuumba. Kosa ulitendalo ni lako wewe si lake yeye, yeye alikupa mema uyatende na si vinginevyo.
 
Mfano wako si sahihi, binadamu huishi kulingana na alivyo, wapo watu wnaokula chakula na kufanya shughurl zao kwa kutumia miguu kwani hawana mikono, hivyo nasi tungeweza kukaa na tusingeona tofauti.
 
Ha ha ha!
 
Mfano wako si sahihi, binadamu huishi kulingana na alivyo, wapo watu wnaokula chakula na kufanya shughurl zao kwa kutumia miguu kwani hawana mikono, hivyo nasi tungeweza kukaa na tusingeona tofauti.
Huo ndio ukuu wa Mungu.Akifunga mlango mmoja basi atakufungulia mwingine.
Kuna mwanariadha wa Africa Kusini hana miguu lakini aliweza kushinda medali ya dhahabu kwa kutumia miguu ya Bandia.Natumaini unamkumbuka Pistorius.
Uumbaji wa Mungu hauna makosa.
 
Umemaliza Mkuu.
 
Mwanadamu hajakamilika sababu Mungu alitaka asikamilike na akafanikiwa kumfanya asikamilike hivyo Mungu hajakosea kwa kutokamilika kwa mwanadamu sababu ndio takwa lake. Pengine angekamilika angekuwa Mungu pia sasa jiulize miungu wote hawa tungeishije? ndio maana tunabaki kuwa mfano tu kama ilivyo picha ya mwanadamu ni mfano wa mwanadamu lkn haiwezi kamwe kuwa mwanadamu inabaki kuwa haijakamilika kwa kulinganisha na mwanadamu halisi.

Tunasema Mungu hakosei sababu tunaamini ndie alieumba universal yaani mpangilio wa sayari zote jua na kilakitu kilichopo angani lkn bila kushikiliwa kimeendelea kwa miaka yote hii. Tunaamini tabiri za Mungu zote zilitokea exactly alivyotabiri hakuwahi kukosea (Mungu hakosei)

japo kwa uchache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…