Kama una shida ni ngumu sana kupata msaada kwenye kanisa la KKKT kama hawakujui

Naona Wasabato mmefika. 😁😁😁Yaani mnaupeo mdogo sana nyie!
 
Mimi siyo msabato. Sifuati mapokeo bali mimi ni Mwanafunzi wa Yesu
Sasa petty issue kama kubatizwa mtoto au mtu mzima Ndio zinakusumbua...suala ni kuwa na Imani Kwa kristo..hao ndugu zenu Wasabato wanashika Sabato na kutokunywa pombe Halafu wananyanduana wao Kwa wao kwenye makambi!
 
Allah auongoze moyo wako uyaone mengi zaidi mazuri ya uislamu.
 
Ndo maana europe makanisa hayana watu sitakaa nimsahau yule mlinzi hivi unamfokeaje mtu mwenye shida
Nilijiuliza utu uko wapi

Tokea siku hiyo nikasema sitakaa nikanyage kanisani mpaka sahivi sina dini tena
Karibu kwenye dini inayoendana na umbile lako na mfumo wako wa maisha mkuu, tangu kuzaliwa mpaka kufa na baada ya hapo.
 
Sasa petty issue kama kubatizwa mtoto au mtu mzima Ndio zinakusumbua...suala ni kuwa na Imani Kwa kristo..hao ndugu zenu Wasabato wanashika Sabato na kutokunywa pombe Halafu wananyanduana wao Kwa wao kwenye makambi!
You said petty issue lakini nakuwekea andiko hapa uone how petty it is....

Ufunuo wa Yohana 22:18 - 19

Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Halafu soma hili...

Marko 16:16
Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
 
Makanisa ya katoliki na kkkt ni mfano mzuri sana wa mfumo wa upepari hakuna cha bure menyeka kwanza ndio upate malipo yako..
 
Makanisa mengi ya wakristo kama huna hela na hawakujui utaonekana takataka tu
Nenda Bunju kanisa la Roma kila wiki wanatoa misaada kwa wasiojiweza Michele, mafuta n.k
Tena makanisa mengi tu yana huu utaratibu
 
Hapo mwenye shida ni mlinzi sio kanisa la KKKT. Siku nyingine unajaribu sabato pale pembeni japo wasabato wengi hawanaga hela, wanaweza kukugonga neno la faraja na kakitabu ka kujifariji (jipatie amani moyoni).
 
Ila twende mbele turudi nyuma, ndugu zetu wafilisti wana utu sana, unaweza kupata hifadhi ya kulala msikitini kuliko kanisani na huo ndo ukweli

Nimeshuhudia misikiti mingi watu wanalala asubuhi wanaenda kujitafuta ila sio makanisani
 
mimi sio KKKT, mimi ni mlokole. ila ukweli ni kwamba, kati ya watu wanaoweza kukusaidia kwa haraka kati ya madhehebu yote haya, ni KKKT. unaweza kufika kwa mchungaji wao, akakulaza, akakulisha, akakupa maji ya kuoga, akakuruhusu uondoke kesho yake bila hata kumpa kitu, na ukiondoka mgeni mwingine akaja akasaidiwa. speaking from experience. siongei kinafiki.
 
Siku nyingine anza kwa kutaja namba ya bahasha yako ya kanisa.
 
Wakoloni walitupa kila kitu bure makanisani, kuanzia tiba, elimu, mitumba na vyakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…