Yani kuna dini inajiona iko sahihi sana kwa kudharau dini zingine huku ikijisifu ni dini ya haki kuliko zingine zote.
Kwa akili za kuzaliwa mwenye hekima anapaswa kutoka nnje ya boksi ajiulize ni kweli dini zingine kama Hinduism, Rastafarians, Paganism, Buddhism na wengine wote wasioishi katika imani za kidini wataadhibiwa na Mungu kwa kutoabudu hiyo dini au kutotenda mema kwa kuuishi upendo kwa Binadamu wenzao?
Mara dini hii ina Wanawake wenye maadili bora sana kwenye ndoa, mara maandiko yake ni sahihi hayana kasoro zozote kuliko maandiko ya dini zingine, mara oooh waumini wake ni watakatifu sana kuliko waumini wa dini zingine, kwani ni malaika hadi wasiwe na kasoro?
Kwa upeo wa kawaida utaona kabisa hakuna kitu kama hicho la sivyo huyo Mungu atakuwa ni katili kuliko hata Shetani.
Wakoloni walituweza sana kutupumbaza na hizi dini za kuletewa, itatugharimu hata miaka 1000 Waafrika kutoka kwenye huu utumwa wa kidini.
Sent from my CPH2387 using
JamiiForums mobile app