Kama upo mtaani muda mrefu bila kazi, tatizo ni wewe!

Nafikiri ukienda kwenye somo la riziki ndio unaweza zeeka umetulia unasubiri rizki.

Unajua kwamba rizki ni kama maji uwa inafata mkondo?

What if haukuzaliwa kwenye mkondo wa rizki?

Usitie huruma mzee hakuna wa kukuonea huruma dunia hii.
Hakuna lolote, pamoja na jitihada unatakiwa kuwa na bahati sometimes... haya mambo yapo... sio wote wenye maisha/ hali duni/ ukosefu wa ajira hawafanyi juhudi, watu wanahangaika sana kutoboa mzee... ila mambo yanagoma.

Nadhani ungewashauri watu wasikate tamaa badala ya kuwaona kama wana makosa.

Hivi kuna mtu anapenda kukaa tu mtaani bila shughuli ya kuingiza kipato? Acha ujuaji mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me nimejiajili sijaajiliwa, na nina vyeti safi mzee na nimeacha kazi 2 kisa naona maslahi hayafiki malengo yangu, sitilii huruma ila naelewa haso za watu
Anaehaso hatiii huruma kama wewe, wanaohaso wanapambana.
 
Na usipokuwa na bahati ndio unajustfy kitu gani? hahahahaha

Mimi sijatumia lugha ya kinafiki ndio maana ujanielewa.

Nachowashauri watu wasipambane kama maboya lazima wawe smart na waache maisha ya kutia huruma hayo maisha hayapo siku hizi.

Maisha ya nna mjomba wangu lakini hanisaidiii hayakufikishi popote.

Lazima uwe na package au silaha za kupambania kombe. Sio una degree yako ya statistics umekaa tu miaka na miaka unalaumu kwa nini una degree na hupati kazi..kwani nani hana degree siku hizi!? una nini cha ziada yani wewe ni data scientist na hujui hata kutumia goggle form na unataka ucompete na watu wanatengezeza ma-database wanafanya analysis kwa tools hata tatu tofauti.
 
Kwanza kwa kazi gani unakuja pigia watu kelele humu, unashangaa mwisho wa mwezi unasubiri 700k, afu unakuja pigia watu kelele.. ungekua MO wewe si ungekua unatukana maskini.. Afu tofautisha kutia huruma na kuongea ukweli halisia
Sasa mkuu kwani kuwa maskini unafikiri ni ujanja ukiwa maskini utatukanwa tu...usipotukanwa na mimi utatukanwa na mabebezi usipotukanwa na mabebezi utatukanwa na masela wako mpaka ndugu zako wa damu yani hauwezi kuwa salama....Pambana usitie huruma hakuna wa kukuonea huruma.

Tengeneza package yako maisha ni yako lazima uwe mnyama.
 
Leo kiumbe kapata anaona wenzake wazembe. Anadiriki kuwaita maboya, mafala, na watiaji huruma.

Labda mungu atakufundisha somo fulani kuhusu riziki as time goes on. Maana wapo watu waliokuwaga na kazi kipindi fulani na leo hawana na hivi sasa maisha yao yamebadilika tunawajua.

Kuwa na akiba ya maneno!

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Haya ni maneno yatayokupa relief lakini hayakusaidii wala hayabadilishi lolote kwenye maisha yako na yangu.

Mimi nimekupa dawa chungu lakini inayoponya.

Mimi nakupa homework nenda kapige dua mbaya kwangu alafu baada ya mwaka angalia tena maisha yako alafu rudi hapa kusoma tena nilichoandika bila hisia.

Utajifunza kitu kuhusu maisha yako.

Unaambiwa ajira ni janga la taifa na wewe inakuingia hiyo unakaa unaskilizia Mama atafungua ajira hahahaha unadanganywa mzee. Kama hauna ajira ilo ni janga lako kuna watu hizo ajira wanabadilisha tu wanazozitaka wewe unatia huruma eti nasubiria bahati yangu ipo siku na hufanyi lolote kupambania kombe eti kisa una vyeti.
 
Unafanya kazi wapi? Tuanzie hapo kwanza [emoji2][emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa Mtendaji Kata, ila wengine hatuna kadi za chama.
 
Hata ukijua nafanya wapi kazi au sifanyi kazi haikusaidiii lolote.

Target yako iweke kwenye kutoboa mzee baba...andaa silaaa hakuna kuletea watu unyonge nani anajali sasa unyonge wako [emoji23][emoji23][emoji23]
Nimeshatoboa kwa viwango vyangu mzee...nilipopitia ndio kunanifanya nisisitize kuwa pamoja na jitihada kudra za Mungu ni muhimu sana,na kila mtu humfikia kwa wakati wake..ni muhusika tu kujua kuzitumia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asa brother tusaidie namna ya kuandika CV kama yako Hata mfano tupatie
 
Sawa Mtendaji Kata, ila wengine hatuna kadi za chama.
Ona sasa hapa unalaumu chama na lazima unalaumu CCM.

Kipindi cha JK mtu aliyekosa ajira aliaminishwa kwamba hapati ajira kwa sababu ajira ni za kujuana wanapata only watoto wa kigogo.

Kipindi cha JPM wakaaminishwa ajira hakuna sababu zimebanwa akiondoka zitafunguka.

Kaja Mama Samia kuna watu wamejawa na matumaini kuwa sasa ajira zimekuja, lakini sad truth wataendelea kusugua benchi.

Tatizo kubwa ni wewe mwenyewe hakunaga excuse nyingine.

Kuna wajuba walitoboa kipindi cha JK.

Kuna wajuba walitoboa kipindi cha Magu.

Kuna wajuba watatoboa kipindi cha Maza.

Wengine wataendelea kutia huruma na kulaumu either ndugu zao au serikali au chama tawala.

Siku hazigandi uzee huo unapiga hodi.
 
Asa brother tusaidie nas namna ya kuandika cv kama yako ata mfano tupatie
Google kuna kila kitu ushindwe mwenyewe tu.

Nakushauri tenga muda walau wiki moja au mbili kwa ajili ya kutengeneza CV na cover letter yako.

Sababu hizi ndio silaha za kwanza kabisa hakikisha una invest muda wa kutosha kuzitengeneza.

Pitia Google ukiandika resumes examples au CV samples au CV pdf utapata CV zaidi ya buku ikiwezekana weka na position mfano CV samples human resource officer. Hivyo hivyo pia kwa cover letters.

Kosa lingine usifanye ni kutumia CV ile ile kuombea position tofauti za kazi ni kosa kubwa sana. CV sio msahafu inatakiwa kubadilika kila unapoomba kazi. Soma wanataka nini watoa kazi kisha twist CV yako.

Ipange vizuri hakikisha personal information, skills, education, work experience, reference ukishwaweka hivi vitu kwa kuvieleza vizuri kwa ufupi sana CV inatosha kabisa.
 
Mimi nimekuelewa sana Mzee Baba! Huu ndo ukweli ambao unatakiwa kusemwa na watu wote! Utasikia Kenge mmoja anakwambia eti na bahati inachangia muulize ashafanya jitihada zote akakwama?

Wengi humu wanasikiliza tu story za watu kwamba nishatafuta sana nikakosa kisa sina bahati basi na yeye anakomalia hapo hapo kwenye bahati wakati hapambani! Wachane Mzee wa kazi na mimi nakazia Hakuna kutia tia huruma! Hata Mungu alisema jisaidie nami nitakusaidia umelala tu gheto unasema ipo Siku atasaidia ..that will never happen
 
H
Ni kawaida lakini kwa mafanikio kidogo kuleta kiburi
 
Acha niwapelekee moto wazembe wazembe wanadeka kama yatima.

Dunia hii ukileta unyonge unanyooshwa tu hahahahaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…