Yani mtu unalala ndani huombi kazi ukakosa unaropoka tu ajira ngumu kisa unasikia story za waliokosa! Siku hizi hata ukiwa na connection utaulizwa kitu gani unaweza kufanya (skills) tunarudi tena pale pale kwenye ujuzi! Ukishajibu hilo swali ndo linakuja swali la vyeti ila swali namba moja ni ujuzi unao! Yani ili uajiriwe au kujiajiri upate wateja unatakiwa uwe na Thamani flani (skill) ambayo itamvutia mteja au mwajiri unatakiwa uwe mtabe wa kitu flani yani piga ua garagaza kitu flani uwe nacho ambacho unasema kabisa hapa kwenye hiki hakuna wa kunitisha! Vijana wengi wapo nusu nusu unakuta anajua hiki kidogo na kile kidogo sasa waajiri hawataki mtu wa kuja kufanya majaribio kazini au kuja kujifunzia kazini, kazini sio Shule au Chuo, watu wanataka product wanataka kazi ugonge show utengeneze faida sasa ukiwa nusu nusu unalia lia ajira ngumu lazima uone kila mtu ana roho mbaya
watu wanakuwa wakali sababu hawataki kutoka kwenye comfort zone.
Maana ukishazungumzia ujuzi inabidi kujifunza na kujifunza ni kunahitaji muda na akili, hapo ndio kijana wa kitanzania anaona unamtukana ukimwambia bado hatoshi kwenye mapambano ya ajira.
Mwingine anakwambia sio lazima kuajiriwa nitajiajiri anafikiri kwenye kujiajiri ndio hatuitaji skills ukiwezeshwa mtaji ndio umemaliza kila kitu.
Skills + Connection = Money
More skills more money
Kama hauna skills ulimwengu wa sasa ajira ni ngumu sana kupata. Hata wanaotoboa kwenye ujasiriamali walikubali kuinvest kupata ujuzi flani.
Jifunze jifunze jifunze kisha jifunze tena mpaka uwe competent lazima utaona mabadiliko. Uzuri tunaishi ulimwengu mwepesi kila kitu kipo mtandaoni either bure au kwa kulipia. Au nenda kwa wanaojua upate ujuzi umekaa kitaa miaka mitano bila kazi ila unaona unapoteza muda kujifunza kitu kwa miezi sita.
Imagine una kampuni yako unatafuta watafiti. Wanakuja watu wawili mmoja anajivunia tu kuwa na degree ya udsm, mwingine maybe ana degree ya teophil kisanji university ila ni hustler wa kitaa anakuja na package ana degree, anaweza kutrain watu, anaweza kudesign research tools kama questionnaires, interview guides etc, anaweza kutumia digital tools like google forms, kobo, tangiline etc...anaweza kufanya analysis ya data, anaweza kufanya presentation ya data, anaweza kuandika technical report.
Hapo ni wazi mmoja ataondoka kwenye interview akisema Mungu ajanijalia acha niendelee kusubiri kudra.