Kama wewe ni 80s na 90s kid na haukuangalia hizi movies utotoni wakati unakuwa basi labda ulikulia msituni

Kama wewe ni 80s na 90s kid na haukuangalia hizi movies utotoni wakati unakuwa basi labda ulikulia msituni

Anord anamuita mwanae "Jeany..... Jeany...."

Jeany anaitikia "Daaaaddy....."

Oya tuache kidogo enzi hizo hakuna CD ni mwendo wa VHS tu
 
Hizi za nyumbani ambazo jini linapaliwa na mate hadi linakohoa je? Hamkuziangalia?
Screenshot_20250805-230534_Chrome.jpg
 
Hizi za nyumbani ambazo jini linapaliwa na mate hadi linakohoa je? Hamkuziangalia?
View attachment 3432799
Hahaha sema hawa wangeendelea kidogo tu walikua wamefika mbali sana, sema basi tu ndio movie za kwanza kuonyeshwa kwenye Banda umiza na watu wanaingia na Kiingilio kuangalia Insyuka na inawekwa Tape kwenye Deki daah enzi hizo hakuna AzamTV na Sinema Zetu
 
1: rambo (1, 2, 3)

2: predator

3: commando

4: sarafina

5: nelia

6: blood sport

7: enter the dragon

8: drunken master

9: rocky

10: tai chi master

11: lion king

12: titanic

13: anaconda

14: coming to america

15: blade

16: friday

17: scarface

18: terminator (1, 2)

19: deadly prey (komando kipensi)

20: godfather

Ongezea nyingine mwana ex-kibanda umiza😁
Hatya, Disco dancer, ghayal, baazigar dah. Sapna na Shani cinema
 
Kuna vyuma hivi wachache sana hapa wameviona kama wapo wanyooshe mkono
1, Never say never again (James bond)
2, seven man army
3, one down two to go (Fred Williamson & Jim Kelly)

Wahindi,
Achaaanakk
Dance dance
Naishia hapo
 
Hahaha sema hawa wangeendelea kidogo tu walikua wamefika mbali sana, sema basi tu ndio movie za kwanza kuonyeshwa kwenye Banda umiza na watu wanaingia na Kiingilio kuangalia Insyuka na inawekwa Tape kwenye Deki daah enzi hizo hakuna AzamTV na Sinema Zetu
Kweli mkuu. Sijui walifeli wapi.
 
Hiyo The bodyguard from Beijing naipenda mpk kesho haichoshi, ila why Jet Li hajamtafuna mke wa boss wake 😥😹😹
Sijapentraaa kabisa, kila nikijitahidi kuirudia nione labda kuna sehemu kagusa hata shavu holaaa..!! 😹

Sema yule jamaa alimtandika Jet Li ila ndo hivyo staring hauwawi..!!
AI ilianza zamani sana. Tulichelewa kujua
 
Kuna wajomba walikuwa wanaleta tv kuonyesha kijijini kwetu siku ya soko bahati nzuri wakawa wanailaza kwetu(kwa ajili ya usalama) baada ya kutoka sokoni kwahiyo sisi kama host tukawa tunapata ofa ya mkanda mmoja usiku. Moja ya movie nalokumbuka lilikuwa la makomandoo watatu wanaenda kwenye mission moja bahati mbaya mmoja akang'atwa na mamba, dah bonge la movie sijawahi kulibahatisha tena toka miaka ya 2000. Sikumbuki hata linaitwaje ningelitafuta nikumbushie
inaitwa the hard way
 
Back
Top Bottom