Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Hahaha mambosasa anaweza kuwa na fortune teller, anajua wote watakao andamana kesho.
Anaweza kuwa nabii.

Anakamata watu kwa hisia zake tu , kwamba waandamanaji ni wanachama wa chadema tu.

Angesubiria hata waandamane kidogo ndio wakamatwe, sasa shitaka lao lipi kwa sasa?!
 
Sawa.

Lakini, hilo ndo kosa la kusababisha mtu akamatwe na kuwekwa ndani?
Katika shughuli za kipolisi hiyo ni tactic ya kudhoovisha hamasa kwa wale wanaochochewa kwani wasipowaona viongozi kule mbele basi hawawezi kujitokeza mstari wa mbele.

Pili, Mambosasa ametoa sababu za kuwakamata wahusika na wamekutwa na vidhibiti kadha wa kadha.

Hivyo ni kazi ya polisi kuthibitisha vidhibiti hivyo, kukusanya ushahidi wote na wakiridhika wawapeleke mahakamani.
 
Katika shughuli za kipolisi hiyo ni tactic ya kudhoovisha hamasa kwa wale wanaochochewa kwani wasipowaona viongozi kule mbele basi hawawezi kujitokeza mstari wa mbele...
Ah wapi!

Hakuna lolote zaidi ya sababu za kisiasa tu.
 
Sasa ndo wakamatwe na kuwekwa ndani?

Halafu mbona Lissu yeye hajakamatwa?

Au yeye wanamwogopa sasa hivi?
Lissu ni mwanasheria hivyo si mjinga kiasi hicho.

Pia Lissu namwona akicheza kete fulanifulani hivi.
 
Kwasababu polisi walijua kwamba mipango si kuomba kibali bali ni kuingia tu barabarani kienyeji.
Walijuaje? Unaweza kumkamata mtu kwa haki kwa kosa ambalo bado hajafanya?

Kama hilo linawezekana, nini kinawazuia polisi kuzusha tu kwamba wanakukamata wewe leo kwa sababu wanajua kesho utaiba?

Yani iwe kwa mfano umemshinda polisi kwenye kupata penzi la mwanamke mliyekuwa wote mnamuwania, polisi kakuchukia, akakuzushia tu kwamba anakukamata kwa kuwa utaiba kesho.

Nini kitamzuia kufanya hivyo?
 
Walijuaje? Unaweza kumkamata mtu kwa haki kwa kosa ambalo bado hajafanya?

Kama hilo linawezekana, nini kinawazuia polisi kuzusha tu kwamba wanakukamata wewe leo kwa sababu wanajua kesho utaiba?...
Sasa mkuu, Mambosasa si ameeleza sababu za kukamatwa kwa Mbowe na wenziwe?

Kwa mfano hata huko uliko, polisi si huweza hata kubomoa mlango wako kisa tu mtu fulani kawapa tip kuhusu mtu huyo na shughuli zake zisizoeleweka?

Anti terror police na polisi wa kawaida wana uwezo huo walopewa na sheria.

Hivyo hata Tanzania polisi wake wana intel na wana uwezo wa kukukamata endapo washukiwa au kuhisiwa kuwa wapanga kufanya uhalifu.
 
Sasa mkuu, Mambosasa si ameeleza sababu za kukamatwa kwa Mbowe na wenziwe?

Kwa mfano hata huko uliko, polisi si huweza hata kubomoa mlango wako kisa tu mtu fulani kawapa tip kuhusu wewe na shughuli zako zisizoeleweka?...
Unaelewa kwamba hawa ni wanasiasa na Polisi wanatumika kuwadhibiti kwa sababu za kisiasa?
 
Watakuwa wanaogopa backlash hao.

Maana Lissu naye kasema atakuwepo kwenye maandamano.

Sidhani kama Magufuli yuko tayari kwa backlash atayoipata akimdhuru Lissu.
Believe me or not Lissu na wenzie wote mipango yao ipo viganjani mwa serikali.

Tundu Lissu hataguswa kwa namna yoyote ile.
 
Unaelewa kwamba hawa ni wanasiasa na Polisi wanatumika kuwadhibiti kwa sababu za kisiasa?
Ndio ni wanasiasa.

Ila sikubaliani na wewe kwamba polisi kwa walichokieleza leo wametumika kuwadhibiti kisiasa.

Hiyo ni kutokana na hali ilivyo sasa ya kisiasa.

Mambosasa ameeleza na ametanabaisha kabisa kila kitu.

Kuna haja kubwa kwa somo la siasa kurudishwa mashuleni ili vijana wajifunze uzuri siasa na waelewe khasa.
 
Wewe Mambosasa unahangaika bure, maandamano yako palepale sanasana ndio wametuongezea munkari subirini kesho asubuhi polisi uchwara ndio mtaelewa nguvu ya umma ni nini ? Mnaambiwa maandamano ya amani mmekazana tu na upimbi wenu .
usiku huu wananchi wameanza kukusanyika kwenye daraja la mfugale kwa ajili ya kuanza kazi saa 2 asubuhi Buguruni sheli
 
Back
Top Bottom