Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Niliyoyaongea huyajatokea?
bro unahitaji msaada wa kisaikolojia chadema inasemekana impegwa kimbunga kikali ina mbunge mmoja,ni wakati wa wewe kusaidia chama kilichoweka historia afrika kwa kushinda asilimia 99.9 ya bunge....magunzi 19 mnayakazania tena wapinga maendeleo?
 
Kitendo cha kuitwa covid 19 maana yake hawakutenda vitendo vizuri kwenda kuiba nyaraka kughushi kujiteua ubunge kienyeji kwa njia haramu za kishetani huku wanachama wa chadema wapo jela kwa kesi za kubambikiwa kipindi cha kampeni ndicho kimepelekea watanzania kuwachukia wakike 19 wanandungai kwa kipimo cha kutisha mno, hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu kabsa anaweza kukaa kuwatetea akina mdee waganga njaa pasipo kujali wanachama wanaoteseka magerezaccm kwa kuwatetea wao
Na hili halijafika mwisho....
Kuna wahuni watakula nao sahani moja.
Tusubiri.
 
Mahera amesema chadema wamepeleka barua yenye Muhuri wa Katibu mkuu. Chadema ni pamoja na Mbowe mwenyewe
Hupati uteuzi ng’oo ujue hata CCM huangalia wa kumpa uteuzi wakiona ni Mzushi mno kama cyprian Musiba na Le mutuz huuchuna sana
 
Mkuu Ingia you tube sikiliza mwenyewe tamko
WAMEVULIWA uanachama wao

Kuwavua uanachama ni hatua zinafuatwa haitokani na maamuzi ya kamati kuu. Kuwavua uongozi ni atua ya kwanza , may be ndiyo waendelee na utaratibu wa kuwavua uanachama. Hatua ya kuvuliwa uanachama inaweza kupingwa kisheria.
Tatizo nyumbu ushabiki mnaweka mbele bila kuelewa process.
 
bro unahitaji msaada wa kisaikolojia chadema inasemekana impegwa kimbunga kikali ina mbunge mmoja,ni wakati wa wewe kusaidia chama kilichoweka historia afrika kwa kushinda asilimia 99.9 ya bunge....magunzi 19 mnayakazania tena wapinga maendeleo?
Leo chadema ilikuwa inaenda kufariki kifo cha ghafra kama UDP DP TLP NCCR na CUF ya Lipumba lakini kitendo cha kuwafukuza wakike wanandungai 19 imerejesha Heshima yake toka kwa wadau wote wa demokrasia
 
Kuwavua uanachama ni hatua zinafuatwa haitokani na maamuzi ya kamati kuu. Kuwavua uongozi ni atua ya kwanza , may be ndiyo waendelee na utaratibu wa kuwavua uanachama. Hatua ya kuvuliwa uanachama inaweza kupingwa kisheria.
Tatizo nyumbu ushabiki mnaweka mbele bila kuelewa process.
Kama kweli unazijua process kampitishe nduguai azijue
 
Baada ya kupata taarifa hizo za ki-intelijensia wangetuma Kamanda Mambosasa akatawanye mkutano kwa kuwa unalengo baya la kuwadhulu hao COVIDs
Kibuli na dhalau havitakuacha salama. Halafuu kwa matusi yenu haya mlitaka wamama wa watu wafike uwanjani simngewafanyia majanga makubwaa.
 
Mkuu Benson heshima kwako. Nakubaligi sana makala zako hasa humu jamvin.

Mangi Aisee kuna makala yako moja uliwekaga humu ndani 'NGUVU YA KUNYA' nimeitafuta kichiz. Yani ulishusha nondo za hatarii.

Ulikuwa 'unawahasa' vijana njia peke ya kumuondoa Mbowe kwenye uenyekiti ni NGUVU YA KUNYA tu.

Nifanyie wepesi kuipata tena iyo linki.

Natanguliza Shukrani zangu za dhati kabisa
Mwenzio yupo busy kusaka uteuzi kwa njia haramu za kishetani unakuja kumuomba Link atakuelewa?
 
Hii kamati imelitendea haki jambo hili. Kwakuwa kumeonekana ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi ikiwa ni pamoja na Katiba yetu ya nchi ninategemea Rais wetu mpendwa ambaye tangia aapishwe kuilinda katiba yetu hata mwezi haujaisha aagize wote walihusika katika ukiukwaju huu wa sheria wachukuliwe hatua kwa kufikishwa mahakamani haraka ili sheria ichukiwe mkondo wake. Haiwezekani nchi yetu ianze kuongozwa kama banana Republic. Na Mahela aliyehusika kufanya huu udanganyifu achukuliwe hatua mara moja kwakuwa kitendo cha kugushi barua ni kosa la jinai ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya madaraka na kugushi nyaraka za serikali. Haya yafanyike haraka ili kurudisha angalau heshima kidogo maana kama anguko la nchi linakuja muda si mrefu.
 
Mojawapo ya failure kubwa sana ndani ya CHADEMA ni ile ya kutokuwa na conflict resolution strategies nzuri; ndiyo maana imekuwa inamegeka vipande kidogo kidogo. Timu ya Samson Mwigamba, Zitto kabwe na Kitila Mkumbo ilianza kumegeka, halafu ikaja timu ya Slaa, na pigo kubwa likawa ni lile la timu ya Lowassa na Sumaye, na sasa litakuja hili hili la timu ya Bawacha. Ningekuwa nimeazimwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA; kwanza ningemzuia Katibu Mkuu asiwashe taa kali kwa chadema kwani Mnyika aliiweka chadema kwenye spotlight kwa kuwatishia akina mama hao kuanza kuigopa chadema. Halafu tungeshughulika ndani ya chama kutafuta jibu lake mwafaka hata kabla ya kuita waandishi wa habari.

Lakini chadema huwa na papala ambazo husababisha imeguke kwa sababu za kujitengezea tu. Sijajua kama yule mama aliyempiga chini mgombea wa CCM naye watamfukuza uanachama ili wabaki kuwa irrelevant kwa kutegemea kuwa wafadhili watainyima serikali misaada. Sikujua kuwa siku hizi CHADEMA kuna watu wana akili ndogo sana ya kupambanua mambo. Kosa kubwa sasa ni kuwa wameshajigawanyika tena.

Niliwahi kusoma hapa JF kuwa Mnyika alisoma UDSM lakini hakumaliza chuo, na halafu Mbowe naye alikwenda kusoma Hull lakini pia hakumaliza!! Sijui kama trend hiyo ya kutokukamilisha mambo ni reflection ya sasa ya mwelekeo wa chama au vipi. "... we will see....." by Trump
Wanafukuzwa chadema,wanaoumia ni CCM,kaaaz kweli kweli mataga.
 
Hii kamati imelitendea haki jambo hili. Kwakuwa kumeonekana ukiukwaji mkubwa wa sheria za nchi ikiwa ni pamoja na Katiba yetu ya nchi ninategemea Rais wetu mpendwa ambaye tangia aapishwe kuilinda katiba yetu hata mwezi haujaisha aagize wote walihusika katika ukiukwaju huu wa sheria wachukuliwe hatua kwa kufikishwa mahakamani haraka ili sheria ichukiwe mkondo wake. Haiwezekani nchi yetu ianze kuongozwa kama banana Republic. Na Mahela aliyehusika kufanya huu udanganyifu achukuliwe hatua mara moja kwakuwa kitendo cha kugushi barua ni kosa la jinai ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya madaraka na kugushi nyaraka za serikali. Haya yafanyike haraka ili kurudisha angalau heshima kidogo maana kama anguko la nchi linakuja muda si mrefu.

Hakuna chochote kifanyikacho bila Baraka we mgeni nn yote sarakasi hii ni kuzitaka hela za mabeberu.
Wawape tu huo viti maalumu
 
Again CDM wanakubali kupoteza msingi wa kwanza wa chama (watu) kama ilivyokuwa kwa wakina Zitto,Prof Kitila,Dr.Slaa na Prof.Mashinji kwa kutaja wachache.
Hivi hawaoni CCM ilivyodili na wakina Nape,Mzee Makamba na Katibu Kinana? Kwanini hawajifunzi jinsi ya kutatua matatizo yao kwa wakati (Taking all time they needed) kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi makubwa kama haya ndani ya masaa 72 ?
Kwanini kila uchaguzi au kwenye michakato ya uongozi ndani ya Chadema inaondoka na watu ?

CDM ili ifike mbali ni lazima ijijengee uwezo wa kumudu,kutunza na kukaa na watu/wanachama wake wa aina zote kwa maana Kuna msemo wa pwani usemao “Mtu si mbwa” leo hii wanapoteza wanachama 19 ambao wengi wao wanaushawishi mkubwa kwenye Ngome ya wanawake ya CDM na mbaya zaidi wanawapoteza kwa mtego wa kawaida sana.

CDM inacheza ngoma ya vyama vingine na kusahau shughuli yao ! Tokea M4C izimike na Dr.Slaa hakuna jambo la kimkakati la kujenga chama au kukuza chama limefanyika zaidi CDM imekuwa iki-REACT kutokana na matukio na matendo ya CCM pamoja na Serikali badala ya ku-ACT katika mipango na mikakati yake .

Itachukua muda sana kujenga watu wengine kulikoni ingepatikana suluhu ya kunufaisha chama zaidi.
 
Sorry boss

Ingekua ww ndio chadema ungefanya nini?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama

Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.

Stay Tuned for Updates

======================
Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.
Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.
22:08
Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini
Mkutano huo utakuwa live kupitia
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini
Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe
"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe
“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe
“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.”
@freemanmbowetz

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE

"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -

Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-

"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -

"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-

“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”
"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe

Mnajidai wana demokrasia kumbe wanafiki tu, ilitakiwa muwaite na muwajadili nao wajieleze,tukisema hii ni SACCOSS mtapinga, kule CCM hata kachero mbobezi alipewa muda wa kujieleza.
 
Sorry boss

Ingekua ww ndio chadema ungefanya nini?

MUDA ni somo kubwa sana ! Unadhani kwanini mtu anaweza kuua akakamatwa na kichwa cha marehemu lakini hukumu yake ikachukua muda kutolewa?
CDM walitakiwa kufahamu kuwa wanao MUDA na hili swala lingewachukua MUDA kuamua si swala la kwenda kwa mhemko na kutafuta shortcut .
Chama ambacho hakiwezi kutunza watu/wanachama wake kwasababu yoyote bila kujali manufaa mapana ya chama itachukua muda kufikia malengo yake.
Hili swala lilihitaji muda na si kwa uharaka huu waliofanya.
 
Mnajidai wana demokrasia kumbe wanafiki tu, ilitakiwa muwaite na muwajadili nao wajieleze,tukisema hii ni SACCOSS mtapinga, kule CCM hata kachero mbobezi alipewa muda wa kujieleza.
Ficha ujinga wako.

Nyau wewee
 
Again CDM wanakubali kupoteza msingi wa kwanza wa chama (watu) kama ilivyokuwa kwa wakina Zitto,Prof Kitila,Dr.Slaa na Prof.Mashinji kwa kutaja wachache.
Hivi hawaoni CCM ilivyodili na wakina Nape,Mzee Makamba na Katibu Kinana? Kwanini hawajifunzi jinsi ya kutatua matatizo yao kwa wakati (Taking all time they needed) kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi makubwa kama haya ndani ya masaa 72 ?
Kwanini kila uchaguzi au kwenye michakato ya uongozi ndani ya Chadema inaondoka na watu ?

CDM ili ifike mbali ni lazima ijijengee uwezo wa kumudu,kutunza na kukaa na watu/wanachama wake wa aina zote kwa maana Kuna msemo wa pwani usemao “Mtu si mbwa” leo hii wanapoteza wanachama 19 ambao wengi wao wanaushawishi mkubwa kwenye Ngome ya wanawake ya CDM na mbaya zaidi wanawapoteza kwa mtego wa kawaida sana.

CDM inacheza ngoma ya vyama vingine na kusahau shughuli yao ! Tokea M4C izimike na Dr.Slaa hakuna jambo la kimkakati la kujenga chama au kukuza chama limefanyika zaidi CDM imekuwa iki-REACT kutokana na matukio na matendo ya CCM pamoja na Serikali badala ya ku-ACT katika mipango na mikakati yake .

Itachukua muda sana kujenga watu wengine kulikoni ingepatikana suluhu ya kunufaisha chama zaidi.
It's now official kuwa Chadema iko mikononi mwa wanaharakati, sio wanasiasa...
 
Back
Top Bottom