Mahakama kuingilia mambo ya chama sehemu ambapo chama kishajiwekea utaratibu wa kichama unaokubalika ni illogical, invasive and undemocratic.
Pia, hapo kuna hatari ya mahakqma kutumiwa kisiasa, hususan na chama tawala, kuvuruga vyama vya siasa, hususan vyama vya upinzani.
Hapo ndipo unaweza kupata mwanachama mamluki anafukuzwa uanachama na vikao halali vya chama, halafu analazimisha uanachama mahakamani na kushinda.
Ni kama Papa wa Wakatoliki ana mu excommunucate muumini, na kusema huyu kwa mujibu wa Canon Law kafanya makosa haya na haya, si Mkatoliki kuanzia leo, halafu huyo muumini akimbilie mahakamani kudai abaki kuwa Mkatoliki. Na mahakama imoe ushindi muumini abaki kuwa Mkatoliki. Litakuwa jambo la ajabu sana.
Kuhusu unlimited jurisdiction, tuchukue mfano kuichunguza hii unayoisema unlimited jurisdiction.
Tuchukulie mfano Rais akimfukuza kazi Mkuu wa Mkoa summarily, Mkuu wa Mkoa anaweza kwenda mahakamani na kudai haki yake kwamba hajasikilizwa na Mahakama itengue uamuzi wa rais?
Mkatoliki akifukuzwa Ukatoliki anaweza kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya kanisa ili arudishwe Ukatolikini na mahakama?