Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Ndivyo Katiba yao inavyosema. Na ni haki ya msingi kumpa binadamu nafasi ya kukata rufaa katika mamlaka ya juu zaidi. Hata nje ya mfumo wa chama kilichokuwa chao wana haki ya kwenda Mahakamani. Na huko Mahakama itaangalia kama walitendewa haki kulingana na Katiba ya chama kilichokuwa chao.

Amandla!
Hivi wajumbe wa Kamati hiyo ni wangapi? Kwa nia njema tu naomba kuwafahamu kwa majina.
 
Nadhani Aida Kenani ni kwamba yeye na wananchi wake watumie hekima tu kufuata matakwa ya Chadema ama la! Nisingeshauri wamfukuze mpaka hapo watakapoongea na wananchi wa huko!
 
Kwa maaamuzi haya magumu, CHADEMA itabaki kuheshimiwa na kuthaminiwa na WaTz kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Kile chama caha kuiba, kuua, kufoji, kutesa kwa kutumia vyombo vya dola kwa kushirikiana na NEC, PCCB, POLICE, BUNGE, DPP, SPIKA na kimamiliki na ku-contol na kuamrisha mihimili mitatu AIBU KWENU.
Ila kumbukeni lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho na chochote mnachopanda MTAVUNA KWA WAKATI
 
Nawasalimu wanajukwaa,

Kwanza nianze kwa kuwapongeza Chadema kwa kutumia strategy kali ili " kuwazuga" mashabiki wenu wa mitandaoni ambao wao kazi yao ni kuwapa moyo na siku ya kupiga kura hawaendi kuwapigieni kura.

Hivi ni nani asiyetaka ruzuku ili chama kiendelee kufanya kazi yake? Msitudanganye hapa mliwaruhusu hawa wakina Mama waende wakaape na pia mkaandaa strategy ya kupambana na wanazi wenu wa mitandaoni na kwakweli mmefanikisha.

Kwasasa ni bao moja kwa moja mmesawazisha, wao hawakuenda kuwapigia kura na mlipo waamasisha hawakuitikia wito wenu na nyie mkaamua tusikie ruzuku nendeni mkaape ili kila mtu apambane na lake.

Hongereni sana Chademaa law strategy kali namna hii.
Hongereni wakina Mama kwa ushujaa,
Hongereni Watanzania kwa umoja na mshikamano.
Kwa hiyo kuwafukuza uanachama nayo ni strategy? Maana hawapo kwenye chama tena!!
 
Hiyo future ya kisiasa ingewasaidiaje kuvuka hapo waliokuwa?Maana kama ni ubunge wengine tayari wameuishi Sana,na tayari walikuwa wameukosa.
kwa hiyo kukua kisiasa lazima uwe mbunge?hao waliopata ubunge leo wote walikuwa wabunge kabla?
 
Hiyo future ya kisiasa ingewasaidiaje kuvuka hapo waliokuwa?Maana kama ni ubunge wengine tayari wameuishi Sana,na tayari walikuwa wameukosa.
kwa hiyo kukua kisiasa lazima uwe mbunge?hao waliopata ubunge leo wote walikuwa wabunge kabla?
 
Kwa maaamuzi haya magumu, CHADEMA itabaki kuheshimiwa na kuthaminiwa na WaTz kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Kile chama caha kuiba, kuua, kufoji, kutesa kwa kutumia vyombo vya dola kwa kushirikiana na NEC, PCCB, POLICE, BUNGE, DPP, SPIKA na kimamiliki na ku-contol na kuamrisha mihimili mitatu AIBU KWENU.
Ila kumbukeni lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho na chochote mnachopanda MTAVUNA KWA WAKATI

Yeah wacha utaratibu ufuatwe; naona sasa NEC watakua wanawabunge wao ili wafurahi!
 
Kwa hiyo kuwafukuza uanachama nayo ni strategy? Maana hawapo kwenye chama tena!!
We chukua popcorn tulia uangalie Mtaalamu wa kubali gear ndege ikiwa hewani anavyomaliza mchezo
 
Mahakama kuingilia mambo ya chama sehemu ambapo chama kishajiwekea utaratibu wa kichama unaokubalika ni illogical, invasive and undemocratic.

Pia, hapo kuna hatari ya mahakqma kutumiwa kisiasa, hususan na chama tawala, kuvuruga vyama vya siasa, hususan vyama vya upinzani.

Hapo ndipo unaweza kupata mwanachama mamluki anafukuzwa uanachama na vikao halali vya chama, halafu analazimisha uanachama mahakamani na kushinda.

Ni kama Papa wa Wakatoliki ana mu excommunucate muumini, na kusema huyu kwa mujibu wa Canon Law kafanya makosa haya na haya, si Mkatoliki kuanzia leo, halafu huyo muumini akimbilie mahakamani kudai abaki kuwa Mkatoliki. Na mahakama imoe ushindi muumini abaki kuwa Mkatoliki. Litakuwa jambo la ajabu sana.

Kuhusu unlimited jurisdiction, tuchukue mfano kuichunguza hii unayoisema unlimited jurisdiction.

Tuchukulie mfano Rais akimfukuza kazi Mkuu wa Mkoa summarily, Mkuu wa Mkoa anaweza kwenda mahakamani na kudai haki yake kwamba hajasikilizwa na Mahakama itengue uamuzi wa rais?

Mkatoliki akifukuzwa Ukatoliki anaweza kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya kanisa ili arudishwe Ukatolikini na mahakama?
H
Kasome vizuri judicial review ujue nguvu na jurisdiction ya mahakama kwenye masuala hayo
 
Hivi nyie Mnawasikiliza akina Mbowe mnafikiri wana nia njema na nchi hii?
Jiukize kwa nini Mnyika hakugombea ubunge?

Kwa nini wagomee viti maalum ?
Hivi unaweza kuumbia umma kuna umuhimu gani wa kuwanyima wale akina mama fursa ya kwenda bungeni kuendeleza mapambano ndani ya bunge ?

Je, wewe binafsi unafaidika nini wale wa kina mama kunyimwa fursa hiyo iliyopo kikatba kwa kuchukua form na kuzikalia ofisini tu bila kuwapa fursa ya kutoa maoni yao kuwa waende au wasiende?

Demokrasia ni pamoja na kuwasikiliza wale waliopinga wazo la kuvunja katiba ya nchi kwa kukataa kupeleka wabunge wa viti maalumu.

SWALI la kujiuliza ni Je, Mbowe ametumia kifungu kipi cha katiba ya nchi kuzuia wabunge waliotakiwa kuteuliwa kikatiba kuingia bungeni!

Je, kuna sheria inayoruhusu Chama cha siasa kuamua mambo yake kinyume na katiba ya nchi!?

Je, ni kifungu kipi cha katiba ya Chadema kinachowapa mamlaka viongozi kuacha kupeleka wabunge wa viti maalumu Bungeni kwa sababu za kizushi kuwa uchaguzi ulivurugwa bila ushahidi wa kutosha zaidi ya kulalamika tu?
Ni lini uchaguzi ulikua huru na haki ?

Kama hakuna sheria wala katiba inayowaruhusu viongozi wa Chama cha siasa kukiuka matakwa ya kikatiba basi Mbowe anapaswa kukamatwa na kuburuzwa mahakamani pamoja na Mnyika na kufungwa jela miaka mia.
Katiba unayoinukuu inatoa mwanya wa "kuminya haki za raia?
Je,Katiba hiyo inalazimisha raia kushiriki asichokikubali?
Katiba ipi inaruhusu na kulinda wanaoivunja wazi wazi bila kuwajibishwa?

Kila kitu kina utaratibu,na taratibu zikikiukwa na wahusika kuna hatua za kuchukua.
Unajua wabunge wa viti maalumu wanapatikanaje,mamlaka husika hufanyaje ili wakidhi matakwa ya sheria na Kanuni ili wawe halali?
Je,taratibu zimezingatiwa ktk kupatikana na kuapishwa kwao? Au kwa vile ni CDM ndiyo tatizo kwa vile hawajakubali "kuonewa na kuunga mkono"juhudi" uchwara?

NB. Kama Membe alijaribu tu kutumia haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa akafurushwa (kwa kifungu kipi cha Katiba?) huoni tatizo sembuse mambo ya wazi na bado unaona wabaya na wakosaji ni CDM,basi kuna tatizo kubwa ktk kuchambua,kutafakari na kufikiri. Haya ndiyo madhara ya "elimu bure!" KWELI NI BURE KABISA.
 
Back
Top Bottom