Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Jemedari mkuu Magufuli angelikuwa hai ningeamini hilo jambo linawezekana bila upembuzi yakinifu lakini hawa waliopo ni michakato tu!
Upembuzi yakinifu ni hatua muhimu sana kabla ya kufanya uwekezaji. Kuna wakati tulinunua boti ya kufanya safari za Dar Bagamoyo bila upembuzi yakinifu, bila shaka tunajua hasara tuliyopata.
 
Hawez kujenga huo mradi nchi Ina Hali ngumu na miradi iliyopo Bado inatakiwa pesa nyingi kukamilisha
 
Mwaka jana walisema ifikapo mwezi wa 4 mwaka 2023 wataanza ujenzi wa daraja pale Jangwani.
Wameshaanza?
 
Wachina Wana reserve kubwa sana ya Hela, hawataki zikae hivihivi, wanataka zizalishe, na wai-annex Dunia na uchumi wao, sisi tunaona daraja, wao wanaona wanaongeza sphere of influence, they are extending territorial influence, a sort of neo colonialism.

Our treasury will be paying bills, mirija itakuwa inanyonya kupeleka china.

M ona hawaleti teknolojia wafungue viwanda? Mbona hawaombi ardhi walime, huku ndiko Kuna ajira za watu wengi, na ni huko ndio tutapata export.

Ukijenga daraja maana yake unaanza biashara ya ku-import kutoka china labour, building materials, na daraja likiisha ndio basi tena, halizalishi kitu. Halafu daraja kwa ajili ya watu milioni moja walioko zenji?

May be kama wanatujengea for free
 
Haya madaraja tuliyonayo urefu usiozidi meter kumi maintance costs inatushinda yanachakaa mpaka yanasombwa na mvua.

Hilo daraja la baharani ambalo litakuwa battered na weather elements usiku na mchana 365 ili lidumu zinahitajika gharama kubwa za upkeep ndio tutaweza.

Huko serikalini kuna vitimbi vya ‘Masakuu na Utoro’ngo’ngo’ afadhali.
 
Hizi ndo hoja muhimu kwa nchi.

Tumezoeshana hoja za nani anataka urais, mara huyu kachepuka, mara fulani pisi kali......

Turudi hapa tujadili maendeleo ya nchi yetu.

Daraja lijengwe nitaomba nifanye jogging ya kwenda zenji na kurudi
Kujenga hilo daraja sio rahisi. Huo mradi kwa harakaharaka unaweza kugharimu trillion 30. Trilion 30 kujenga tu daraja kwa nchi hii bado sidhani kama tuna huo msuli
 
Kujenga hilo daraja sio rahisi. Huo mradi kwa harakaharaka unaweza kugharimu trillion 30. Trilion 30 kujenga tu daraja kwa nchi hii bado sidhani kama tuna huo msuli
Kiukweli haufai,hakuna Nchi iliyoendelea ilianza na mamiradi yasiyo na Tija kama hayo
 
Daraja Dar to Znz!!
Meli zitapitaje kuja Dar kutoka mataifa mengine....
 
Kiukweli haufai,hakuna Nchi iliyoendelea ilianza na mamiradi yasiyo na Tija kama hayo
Hata kama kungekua na tija, bado hatuna uwezo wa kujenga daraja moja kwa gharama hizo.

Nimeona umbali wa daraja unaweza kufanana na wa lile la Tianjin. gharama za Tianjin bridge za kule china, wao walitumia trilion 50. Hapo kil akitu wanazalisha wao, huku karibu kila kitu tunaagiza si inaweza kufika trilion 80.
 
Waliowahi kwenda .Jee huko kwao wameshajenga daraja la kupita mkondo mkali kama wa magogoni au Nungwi.
Miradi ya Viongozi wa Tanzania inashangaza sana ,just imagine anachoongea huyu bwana hapa kina logic kabisa ila wenye akili ndogo Huwa hawaelewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…