Kampuni ya Africell inadai ukiweka hela ndani ya siku 3 unapata Mara mbili yake. Je, imesajiliwa TRA, BRELA?

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Kuna Kampuni inadai wao wanajishughulisha na biashara mbalimbali, ikiwemo kuuza na kununua Mafuta oil diesel duniani, kuuza bizaa mbalimbali, kununua Madini, usafirishaji wa meli.

Wao wanadai wanesajiliwa TRA, Brella, staili yao ni Moja tu, ukiwekeza kuanzia laki moja Hadi milioni 50 ndani ya siku tatu unapata fedha mara mbili yake, mfano ukiwekeza milioni 10 ndani ya siku tatu unapata milioni 20. Kampuni hii inapiga promo na inaonekana watu wapo wakujiunga,

Ila hizi biashara za kuweka milioni 50 halaf ndani ya siku 3 unapata milioni 100, naishiwa nguvu kabisa. Watanzania tutaacha lini hizi chuma ulete

 
Hiyo kampuni hawana ubunifu hata kidogo, kwenye kujinadi wangeongeza na maneno haya: "tumedhamini filamu ya Royal Tour, pia wabunge wa JMT wamepanda pesa na kuvuna mara mbili kupitia kampuni yetu"
 
Pyramid scheme, ni DECI, ningekuwa Kamanda Siro ningeenda kuwakamata wote
 
Tozo tu ya sh 100 kwenye kiwese inataka kututoa roho bado na nyie tena mnataka mpite na marupurupu yetu tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…