Kanali wa Iran auawa kwa mashambulio ya Pakistan katika ardhi ya Iran

Vita za India na Pakistan nyingi zilikua za mitutu na Mizinga na mashambulio ya anga kwa kiasi.
Border clash unahusishaje submarine embu usinichote broh.
Na vita zao hawa jamaa zilikua za kupumzika mnaviziana mnapumzika.
Iran Vs Iraq ilikua vita ilohusisha ndege vita,mizinga,makombora ,maroketi na vifaru ilifikia hatua mpaka mmoja wapo aliishiwa silaha na kufadhiliwa na USA
Na vita haikusimama ilipiganwa 8 years consecutively.
Usifananishe hizo vita aisee.
Syria pia IRGC ina operate kumbakisha Assad madarakani IRGC hao hao wafadhili wa washika silaha tata hapo middle east Hizbollah na Houthi .
Huwezi fananisha jeshi la Iran na la Pakistan kuwa serious bro.
 
Unacholalamika kwa Pakistan kulea magaidi ndicho kilekile Marekani ililalamikia Afghanistan ya Taleban kulea magaidi. Tofauti ni kwamba Marekani iliamua kuingia kuwakalia wakati hizo nchi nyingine haziwezi kuingia kwa Pakistan.

Ni sawasawa pia na Turkey kuishutumu Syria kulea waasi wa Kikurdi. Ni sawa na Israel kuishutumu Lebanon kuwalea Hezbollah na Gaza kuwalea Hamas.

Ukikubali kinachofanywa dhidi ya Pakistan pia kubali kinachofanywa kwingineko.
 
Sasa mkuu unachekesha sana rasilimali mlizo nazo hapa nchini hamuwezi kuzilinda zinaporwa tena bila bunduki ndo mtaweza kwenda kupora za nchi nyingine?
kila mnyonge na mnyoge wake.
 
Kwann baada ya shambulio la Iran ndani ya Pakistan serikali ya Pakistan ililaani hilo shambulio na ikamwita balozi wake kurudi Pakistani na pia ikawatimua raia wa Irani waliokuwa njiani kurejea Pakistani?
Bila shaka huwezi fanya operation ya kijeshi pasi na kuhusisha mamlaka husika.
Lazima hatua za kidiplomasia zichukuliwe.
Hata Turkiye anapoenda kuwawinda PKK huwa anatoa taarifa Damascus.
 
Iran hakupigwa hiyo vita sababu kuu mbili.

1. Serikali ya Iran ilikuwa ina silaha nyingi za Kimarekani na Israel hasa Airforce.
2. Pili hii ni moja ya vita ambayo ilikuwa na alliances za kipekee
Upande wa Iran

Syria
Libya
North Korea
Bulgaria
Poland, Yugoslavia,
East Germany,
China
Switzerland
Argentina
United States ,
Israel

 
Lebanon haiilei Hizbollah bali inaitegemea kiulinzi na hizbollah inatambulika nini inafanya toka 2000.
Hamas kilikua chama cha siasa kabla hakijaamua kushika silaha.
Na ndicho kilichopigiwa kura kuiongoza Gaza
Hayo makundi ya Pakistan unayaelewa lengo lake nini na yanatetea nini?
Taliban ilikua ikiiongoza Afghanistan miaka 20+ kabla US hajatia mguu pale.
 
Hawa hawafai kuunda taifa wataleta sana machafuko hawa jamaa.
Ni wabishi sana hao , unajua hata hiyo pkk ya Wakurdi ,miongoni mwa waanzilishi wake
na wapiganaji ni wanawake
Na ni wabishi haswa , kuna vita ya Kati ya ISIS na hawa Wakurdi pale Syria ilisaidia sana kuwatokomeza ISIS , ni wapambanaji na wabishi mno , ndio Maana Saadam na ubabe wake alisumbuka nao sana ,akaamua kuanza kuwaua kama siafu ,aliwashambulia na kuwaua kikatili sana kule Iraq enzi za baath party na wale watoto wake wawili
 
Sema Pakistan wabishi, ngoja tusubiri response ya Iran.
Wametumia ndege, askari au ballistic missiles kufanya mashambulizi?

Hapa wale wenye misimamo mikali hawana pa kusimamia. Maana mambo bulibuli..wanatoana roho wakimsifu Mwenyezi Mungu, kama ilivyomkuwa Iraq na Iran.
Jamani vita ni mali ya shetani. Tusijidanganye kuwa vita ina msaada
 
Bado unatafuta justification ya kudai Pakistan hawana uzoefu na vita? Kwamba Iran iliyopigana mara ya mwisho mwaka 1985 ina uzoefu mpaka leo ila Pakistan iliyoingia state of war mara kadhaa haina uzoefu.

Iran hawajawahi kutana na aircraft carriers wala submarines kwenye vita, vitu ambavyo Pakistan inakutana navyo kwenye naval blockade za India.

India na Pakistan zinaogopana, ni kama India na China. Iran na Iraq zilidharauliana ndio maana zilikuwa zinapigana kama dunia imeisha, sasa unategemea India na Pakistan wapigane hivyo wakati currently wana nukes.

Pakistan imeshambulia tena Iran jana, waite Iran wajibu ndio utajua kama Pakistan wana uzoefu au hawana.
 
Pakistan wapo mfukoni mwa Saudi Arabia na USA, chochote watachokiamuru hao mabwana wakubwa Pakistan haitofikiri mara mbili.

Pakistan hawakupigwa wao, waliopigwa ni kikundi cha ugaidi kisichoitakia mema serikali ya Iran, na ni baada ya diplomasia kubwa sana kupita.

Jana nilikuwa namsikiliza Waziri wa Mambo ya nje wa Iran anahojiwa huko Davos, kasema wazi kuwa hata kabla ya mashambulio waliwasiliana na Pakistan na kuwafahamisha.

Iran ilitumia "precision bombs" kama ilizotumia kutandika kituo cha Mossad huko Erbil, Kurdistan na kuwachapa ISIs huko Syria.

Walichofanya Iran ni kuonesha kuwa wanayo intelijenssia na wameshambulia vikundi vya Kigaidi.

Mengine yote ni propaganda za Wamarekani, Wasaudi na ndugu zao mazayuni.
 
Vita sikuhizi zinaenda kwa mwendo wa proxies , Una lea makundi hasimu wa adui yako kama mtaji wa kujilinda na kukichafua dhidi ya adui yako kwa maslahi yako
Ndio ulimwengu wa vita uko hivi siku hizi
 
Link ulonitumia hapo kumeonesha support ya ammunitions tu.
Tena wengi wakimuuzia Iran sio kumpa.
Wala sio support ya millitary personnel.
Pia ukumbuke jeshi la Iran lilikua bado halijawa stable maana ndio kwanza lilitoka kufanya mapinduzi.
 
Hata IRGC ni jeshi ndani ya Iran, na limefanya mashambulizi kwa Iraq na Pakistan.
Kama lina justification ya kushambulia ardhi ya nchi nyingine na mnakubali, kwanini mnakataa justification ya Israel kushambulia wanaoishambulia waliopo nchi nyinginezo?

Kwanini Iran kushambulia inaoita magaidi iungwe mkono, ila Israel kushambulia inaoita magaidi ilalamikiwe.
 
Hizbollah ni zao la Iran na wameiharibu kabisa Lebanon. Lebanon kwa sasa ni sehemu hatari sana ya kuishi. Ustaarabu wao umepotea mazima sababu ya kukaribisha wapalestina ambao kwao lengo bado ni kupigana na Israel.
Na vita haina macho. Inaharibu vitu vyote, mpaka culture ya watu mahalia
 
huuu mwakaaa tutaona mengi wauza silahaa kazikwenu
Huko USA order zimejaa ukiagiza Himars au Javellin Leo unaipata baada ya miaka 2-3. Imebidi Lockeed Martin waongeze uzalishaji, kupanua na kuongeza plants mpya za kufyatulia silaha.
 
Pakistan na Iran wanafanana tabia. India ina jeshi kubwa kuizidi Iran ila iliposhambulia magaidi waliolipua bomu kuua wanajeshi wa India na kukimbilia kambi yao deep within Pakistan. India iliwashambulia kwa fighter jets.

Pamoja na kwamba India ina nukes na jeshi kubwa, Pakistan walijibu mashambulizi haraka kwa kutumia ndege na kwenye mgogoro huo ndege moja ya India ilidunguliwa. Sasa ndio waiogope Iran kisa ballistic missiles na drones, kwani nani hana. Na wakati wao wana nuclear weapons.
 
Correction.
1)Sijasema Pakistan hana uzoefu,anao ila hajafikia wa Iran.
2) China na India haziogopani bali India inaiogopa China.
Hizo confrontation walizokumbana nazo Pakistan na India ni za kuviziana brothee hazina uzito.
Usifananishe na confrontation alizofanya Iran.
Iran ana jeshi la maji lenye nguvu ukumbuke kipindi cha Obama kuna submarine mbili za USS zilikamata 10 kilometres kabla hazijagusa Iran marine borders.
Bado unataka kufananisha Iran na Pakistan.
Miziki alocheza Iran ya kibabe mpaka anapigana proxy war usimfananishe na Pakistan.
Alipolipua Pakistan ni eneo ambao wanachangia wote na Iran hvyo haliwezi leta wider escalation.
Ila kama angegusa maslahi muhimu ya Iran ,Pakistan angetambua kwanini drone za Iran zilikua game changer kwenye vita ya Russia dhidi ya Ukraine.
 
Hii nchi hua inanishangaza Sana, Jeshi Lina ushawishi mkubwa kuliko serikali.
 
Kumbe Pakistan inalea makundi ya Kigaidi nchini mwao!!!?????
Basi hawafai hawa watwangwe tu.
Majirani zake wote wana mlalamikiaga.
Hata Osama ametafutwa sana kumbe alikuwa amejichimbia nchini Pakistan na serikali ya Pakistan ilikuwa inajua lakini wakapiga kimia.

Baada ya Marekani kufanya uvamizi wa siri na kumuuwa Osama serikali ya Pakistan ilimaindi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…