Kanali wa Iran auawa kwa mashambulio ya Pakistan katika ardhi ya Iran

Pakistan wapo mfukoni mwa Saudi Arabia na USA, chochote watachokiamuru hao mabwana wakubwa Pakistan haitofikiri mara mbili.
Iran iliyoshambulia ndani ya Pakistan iko mfukoni mwa nani?
Iran ameshambulia umekubali, Pakistan ameshambulia unadai yuko mifukoni.
Pakistan hawakupigwa wao, waliopigwa ni kikundi cha ugaidi kisichoitakia mema serikali ya Iran, na ni baada ya diplomasia kubwa sana kupita.
Hata Pakistan imepiga kikundi cha kigaidi, huyo Kanali wa Iran inahitajika maelezo ilikuwaje yeye na bodyguards wake wamekutwa kwenye shambulizi dhidi ya magaidi.
Jana nilikuwa namsikiliza Waziri wa Mambo ya nje wa Iran anahojiwa huko Davos, kasema wazi kuwa hata kabla ya mashambulio waliwasiliana na Pakistan na kuwafahamisha.
Hata Israel huwa inaifahamisha Syria na Russia ikitaka kuishambulia magaidi yanayofadhiliwa na Iran ndani ya Syria.

Hata Uturuki nayo ikifanya mashambulizi Syria huwa iko mifukoni kwa Saudi Arabia?
Iran ilitumia "precision bombs" kama ilizotumia kutandika kituo cha Mossad huko Erbil, Kurdistan na kuwachapa ISIs huko Syria.
Iran ilitumia suicide drones na ballistic missiles. Haina ubavu huo wa kupeleka fighter jets kwenye anga la Pakistan kudondosha mabomu.
Walichofanya Iran ni kuonesha kuwa wanayo intelijenssia na wameshambulia vikundi vya Kigaidi.
Kama ambavyo Pakistan wamefanya
Mengine yote ni propaganda za Wamarekani, Wasaudi na ndugu zao mazayuni.
Pakistan kashambulia Iran, sio propaganda ni ukweli.
 
Kama ni giant ashambulie tena Pakistan tuone ugiant wake.
Giant kila siku watu wake muhimu wauawa ndani na nje ya nchi yake yupo tu anatoa macho.!!!!!
Hakuna mtu muhimu alouawa ndani ya Iran na Iran ikose kulipiza kisasi.
Labda kama ni mfinyu wa taarifa.
YES IRAN IS GIANT .
1)Kamtunishia Israel misuli kupitia Hizbollah.
2)Kamtunishia USA na Saudi Arabia misuli kupitia Houthi.
3)Kamtunishia misuli USA Syria kwa kumbakisha Assad madarakani.
Kamtunishia misuli UK na USA mediterranean sea.
Na mpaka sasa USA wanampigia kelele Iran aache kuwasapoti Houthi na Hizbollah.
Ligi anazocheza Iran sio za kitoto.
Kama Pakistan angekutana na uhasama wa USA na vikwazo vya USA kama Iran,Pakistan ingekua kama Haiti maana hata sasa ni nchi chovu.
 
Hawa Iran walishawahi kulalamika eti Israel inawaibia mawingu ili mvua isinyeshe kwao😂😂😂.
Taifa LA hovyo Sana.
😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣 Duuuh!Asa kaka hapa imetia fora.
 
Hakuna mtu muhimu alouawa ndani ya Iran na Iran ikose kulipiza kisasi.
Labda kama ni mfinyu wa taarifa.
YES IRAN IS GIANT .
1)Kamtunishia Israel misuli kupitia Hizbollah.
2)Kamtunishia USA na Saudi Arabia misuli kupitia Houthi.
3)Kamtunishia misuli USA Syria kwa kumbakisha Assad madarakani.
Kamtunishia misuli UK na USA mediterranean sea.
Na mpaka sasa USA wanampigia kelele Iran aache kuwasapoti Houthi na Hizbollah.
Ligi anazocheza Iran sio za kitoto.
Kama Pakistan angekutana na uhasama wa USA na vikwazo vya USA kama Iran,Pakistan ingekua kama Haiti maana hata sasa ni nchi chovu.
1.Unatunisha misuli kupitia proxy kwanini haingii front mwenyewe?!
Israel imeshafanya mashambulizi kibao ndani na nje ya Iran kuanzia kuua wanasayansi, viongozi wa jeshi mpaka kufanya operation na kulipua kituo cha nyuklia cha Nataz. Iran aliifanya nini cha maana Israel?!
2. Haothi kwasasa wanachezea kichapo, Mara ya mwisho ni Jana Marekani imewatandika kwa Tomahawks.

3. Syria ni failed state. Huna habari kama sehemu zenye visima vingi vya mafuta zinakaliwa na Marekani?! Iran na magaidi wake wameifanya nini Marekani zaidi ya kila siku kulalamika?!

4. Iran inalea magaidi halafu inailalamikia Pakistan kufuga magaidi. Tofauti yao ni ipi sasa. Atulie aonje joto ya jiwe.
 
Kwa matukio ya kijeshi alofanya Iran tokea 1979 Iran inaonekana kuwa na nguvu kuliko Pakistan.
Na silaha za Iran zime prove kuwa na ubora maeneo mbali mbali duniani kuliko za Pakistan.
Leo hii ukimwambia mtu umpe made in Iran au made in Pakistan lazima akwambie nipe Khordak made in Iran.
Pakistan makundi tu ya kigaidi yanayofanya mashambulizi kwake anashindwa kuyathibiti.
Makundi ya kigaidi ya Pakistan yanakuwa supported na India. Na wakati huo Pakistan ina policy ya kulea makundi ya maadui zake. Wakati Iran hakuna nchi inalea makundi dhidi yake, Israel ikiamua itengeneze kundi la kigaidi dhidi ya Iran mbona watateseka.

Silaha za Iran ni bora sijakataa, ila gap sidhani kama ni kubwa sana na za Pakistan. Ni kwamba Iran ina kiherehere ndio maana silaha zake zinaonekana sana. South Korea ina silaha nzuri sana ila hujawahi ziona vitani sababu haipendi kujihusisha na ugomvi.

Pakistan kwa msaada wa China sasa inaunda 4th generation fighter J-17 Thunder nyingine Nigeria wamenunua, Iran hata 3rd generation hawawezi.
Kuna vitu wanazidiana ila wakiingia vitani wataumizana, sio eti Pakistan itaumia sana alafu Iran itambe tu.
 
Iran iliyoshambulia ndani ya Pakistan iko mfukoni mwa nani?
Iran ameshambulia umekubali, Pakistan ameshambulia unadai yuko mifukoni.

Hata Pakistan imepiga kikundi cha kigaidi, huyo Kanali wa Iran inahitajika maelezo ilikuwaje yeye na bodyguards wake wamekutwa kwenye shambulizi dhidi ya magaidi.

Hata Israel huwa inaifahamisha Syria na Russia ikitaka kuishambulia magaidi yanayofadhiliwa na Iran ndani ya Syria.

Hata Uturuki nayo ikifanya mashambulizi Syria huwa iko mifukoni kwa Saudi Arabia?

Iran ilitumia suicide drones na ballistic missiles. Haina ubavu huo wa kupeleka fighter jets kwenye anga la Pakistan kudondosha mabomu.

Kama ambavyo Pakistan wamefanya

Pakistan kashambulia Iran, sio propaganda ni ukweli.
Umechanganya na kuja zpost mpaka sikuelewei. Weka moja mja nikujibu, unachanganya mambo mengi sana kwa pamoja. Jifunze kutumia mitandao ya kijamii kwa tija. Hakuna mtihani hapa, wewe ni mwalimu wa shule za kata nini?
 
Lebanon sio sehem hatari kuishi.
Watu wanaishi vizuri tu ila kuna matatizo tu ya kiuchumi yaliyotokana na vita na kutokua na serikali imara.
Sina uhakika kama zao la Iran ila wafadhili wao ni Iran pasi hiyo Hizbollah Israel ingekua inaimiliki Bint Jubeir mpaka sasa.
Kwahiyo matatizo ya kiuchumi huwa yanatengeneza nini? Paradiso? Anywa, kwangu ni stay aware country. Kama ilivcyo Pakistan. Mwenye macho haambiwi ona Arif
 
Makundi ya kigaidi ya Pakistan yanakuwa supported na India. Na wakati huo Pakistan ina policy ya kulea makundi ya maadui zake. Wakati Iran hakuna nchi inalea makundi dhidi yake, Israel ikiamua itengeneze kundi la kigaidi dhidi ya Iran mbona watateseka.

Silaha za Iran ni bora sijakataa, ila gap sidhani kama ni kubwa sana na za Pakistan. Ni kwamba Iran ina kiherehere ndio maana silaha zake zinaonekana sana. South Korea ina silaha nzuri sana ila hujawahi ziona vitani sababu haipendi kujihusisha na ugomvi.

Pakistan kwa msaada wa China sasa inaunda 4th generation fighter J-17 Thunder nyingine Nigeria wamenunua, Iran hata 3rd generation hawawezi.
Kuna vitu wanazidiana ila wakiingia vitani wataumizana, sio eti Pakistan itaumia sana alafu Iran itambe tu.
Kuna taarifa wanataka kununua J-31 (fifth gen) za mchina.
 
Umechanganya na kuja zpost mpaka sikuelewei. Weka moja mja nikujibu, unachanganya mambo mengi sana kwa pamoja. Jifunze kutumia mitandao ya kijamii kwa tija. Hakuna mtihani hapa, wewe ni mwalimu wa shule za kata nini?
Huwezi nijibu sababu huna uelewa na ulichochangia. Nimekujibu kila hoja yako ila kwa sababu ni mshamba huelewi unataka nijibu hoja zako tofauti kwa pamoja.

Shule ulienda kuvaa sare.
 
Kuna taarifa wanataka kununua J-31 (fifth gen) za mchina.
Hazijawa introduced bado ziko kwenye trials na development. Labda kama wana interest, tatizo lao wananunua sana silaha na uchumi hauruhusu. Wapo radhi wafe njaa ila bajeti ya silaha haikosi
 
Huwezi nijibu sababu huna uelewa na ulichochangia. Nimekujibu kila hoja yako ila kwa sababu ni mshamba huelewi unataka nijibu hoja zako tofauti kwa pamoja.

Shule ulienda kuvaa sare.
Naona weewe ulienda kusomea ujinga.

Wacha kuwa mwalimu wa shule za kata kwenye mitandao, huo ubakishe hukohuko shule unayowasomesha ujinga. Ku 'complicate" mambo yasiyihitaji "comlications".
 
Pakistan haiiogopi Iran, haitishiwi nyau. Leo Pakistan imewaua Wairan 7 inawaita magaidi ndani ya ardhi ya Iran, Pakistan sio kama Iran inayotoaga onyo zito kwa Israel kwa kutumia barua na maandamano. Kila tukio utasikia this is the last warning, na lingine likitokea utasikia this is the last warning [emoji3544]
Walio wote sio raia wa Iran kwa mujibu wa serikali ya Iran.
 
Iran ina air defense systems nzuri na missiles arsenal nzuri. Pakistan ina Airforce nzuri na wala sio chovu kwenye ballistic & cruise missiles.

Kwenda moja kwa moja kudai Iran inaizidi mbali Pakistan ni kujidanganyaView attachment 2875404
Pakistan ukiondoa uwezo wao wa kinyukilia ni nchi yenye uwezo wa kawaida sana hasa kwenye ground force na hata jeshi lake la anga halina makeke sana mbele ya ID za Iran ,upande wa Iran inashehena kubwa sana ya makombora na drone na inajeshi kubwa sana la ardhini.

Hata India anaiogopa Pakistan kwa sababu ya nyukilia tofauti na hapo Pakistan hana cha kumtisha India.

Hata hivyo vita ikitokea itawaumiza wote maana vita haijawahi kuwa lele mama.
 
Pakistan wapo mfukoni mwa Saudi Arabia na USA, chochote watachokiamuru hao mabwana wakubwa Pakistan haitofikiri mara mbili.

Pakistan hawakupigwa wao, waliopigwa ni kikundi cha ugaidi kisichoitakia mema serikali ya Iran, na ni baada ya diplomasia kubwa sana kupita.

Jana nilikuwa namsikiliza Waziri wa Mambo ya nje wa Iran anahojiwa huko Davos, kasema wazi kuwa hata kabla ya mashambulio waliwasiliana na Pakistan na kuwafahamisha.

Iran ilitumia "precision bombs" kama ilizotumia kutandika kituo cha Mossad huko Erbil, Kurdistan na kuwachapa ISIs huko Syria.

Walichofanya Iran ni kuonesha kuwa wanayo intelijenssia na wameshambulia vikundi vya Kigaidi.

Mengine yote ni propaganda za Wamarekani, Wasaudi na ndugu zao mazayuni.
Propaganda nawakati pakistan imemfukuza balozi wa irani na kumwita balozi wake aliyeko iran
 
Back
Top Bottom