Kanisa Katoliki lapata Papa mpya wa 267, ni Robert Francis Prevost kutoka Marekani, ataitwa Papa Leo XIV

Kanisa Katoliki lapata Papa mpya wa 267, ni Robert Francis Prevost kutoka Marekani, ataitwa Papa Leo XIV

Nina imani wewe siyo Mkatoliki. Maana kama Marekani tu na ukubwa wake, hii ndiyo mara yake ya kwanza inatoa Papa! What is so special about Africa?

By the way, Papa akichaguliwa huwa anawahudumia waumini wote wa Katoliki duniani kote. Na siyo waumini wa nchi yake tu. Na kuna Mabara mengi duniani, huku Papa akitakiwa kuwa mmoja tu.

Kwa Wakatoliki wa Afrika, sidhani kama kuna muumini anaweza kuwa na mtazamo kama huu wa kwako. Kwao Papa ndiyo muhimu, na siyo mahali anakotoka.
Well stated 👏
 
Kumbe mnawakubali sana Wakatoliki na kuamimi kuwa ndiyo Wababe wa dunia, sasa Chuki zenu na Mihadhara yenu ya Kuwatusi Wakatoliki huwa zinatoka wapi?

Wa Kuinama na Kujamba 24/7 bhana!!
😹😹😹 Kumekuchaaa.!!
 
Kama kuna VITUKO DUNIAN

Asbh kuna Plicha ilisambaa trump amevaa viazi la Ki pope

Na Leo hii Pope ametokea USA

All d best

Pope ROBERT.V.F
 
20250508_214406.jpg

Pope Smoke 🤣🤣🤣🤣
 
Kwa ubaguzi walio nao hawa watu hadi dunia inaisha haitakua na Papa mweusi, labda Papa mweusi atabaki kuwa Papa Mafido na Papaa Wemba
Ila sisi Wakatiliki wala hatufikirii hivyo vitu. Kwetu sisi tunapozungumza kanisa ni kitu kimoja hatuna mipaka ya kidunia, ni mwili mmoja wa Kristo, ambaye alikufa kwa ajili ya yeyote anayeridhia aokolewe naye. Huyu ni Mmarekani ambaye alikuwa akichunga kondoo wa Bwana huko Peru kabla hajahamia makao makuu, na anaweza kuongoza hadi akafa hajafika kwa Trump, ila akatembelea maeneo yenye uhitaji duniani kwa kadri anavyoongozwa na Roho Mtakatifu, eneo lake ni kubwa mno hata hawafikagi kote hadi wanakufa.

Ila komenti yako imenifanya nipaliwe kwa kucheka, ningekufa leo 🤣🤣.
 
Kwa ubaguzi walio nao hawa watu hadi dunia inaisha haitakua na Papa mweusi, labda Papa mweusi atabaki kuwa Papa Mafido na Papaa Wemba
Kwa ubaguzi walio nao hawa watu hadi dunia inaisha haitakua na Papa mweusi, labda Papa mweusi atabaki kuwa Papa Mafido na Papaa Wemba

Katika hali ya kawaida, hivi wewe kwa akili yako uliyonayo ulitarajia kabisa kwamba mtu mweusi kutoka katika bara la Afrika angeweza kuchaguliwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki duniani?? Seriously???
Mimi binafsi niliwahi kueleza bayana hapa mtandaoni kwamba kwa Sasa haupo kabisa uwezekano wa kuweza kuchaguliwa kwa Papa Mwafrika (Mtu Mweusi), completely impossible!
 
Dunia imempata Papa mpya

Naam tamanio la Trump la kumpata papa wa Kimarekani limetimia. (Shuka kwenye comment ya kwanza)

Moshi mweupe umeibuka na Robert Francis Mmarekani mwenye asili ya Italia na Ufaransa, naam amechaguliwa kuwa papa 267 na kuchagua jina la Papa Leo XIV.

Katika siasa hakuna (ga) ajali, ni mipango tu ya elites kwa maslahi yao ya ulimwengu huu. Washngton na Vatican ndio wakuu na wachezaji muhimu wa siasa za kikanda ulimwenguni. Nitaeleza wakati mwingine juu ya hili

Hivyo wale waliokuwa na tamanio la kumpata papa mweusi basi habari ndio hiyo. Rejea makala yangu inayosema (sio rahisi kupata papa mweusi) na ndani yake kulikuwa na swali la tafakari linalosema (je moshi mweupe unaweza kuibuka na papa mweusi?)....utaelewa ni kwanini nasema hawezi tokea papa mweusi duniani. Rafiki zangu wa kikatoliki walinijibu kuwa hatuendeshwi na hisia za watu. Ingawa kama angetoa papa mweusi kama ilivyokuwa kwa Obama wangepiga shangwe hata mimi ningefurahia, maana hisia hizi zilikuwepo na kuenea hadi katika media kubwa duniani. Hata wengine wakadiriki kudanganya umma kwamba walikuwepo mapapa watatu weusi huko zamani za kale. Ni uzushi. Na nitaupa post yake maalum.

Anyway isiwe hoja maana papa hafanyi yake bali upapa unavyotaka. Haijalishi amekaa nani hapo sharti afanye kulingana na kiti.

Kongole Wakatoliki wa Kirumi kwa kumpata papa mpya.
 
Katika hali ya kawaida, hivi wewe kwa akili yako uliyonayo ulitarajia kabisa kwamba mtu mweusi kutoka katika bara la Afrika angeweza kuchaguliwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki duniani?? Seriously???
Mimi binafsi niliwahi kueleza bayana hapa mtandaoni kwamba kwa Sasa haupo kabisa uwezekano wa kuweza kuchaguliwa kwa Papa Mwafrika (Mtu Mweusi), completely impossible!
Wakatekumeni mna shida sana. Sisi Walei tunawaangalia tu mnavyo hangaika na mambo yasiyo kuwa na tija. Kwani lazima Papa awe ni mtu mwenye ngozi nyeusi? Au anayetakiwa kuongoza Kanisa Katoliki ni Papa?
 
Trump na tamanio lake....limetimia. Trump hakuvaa hivi kama wanavyopotosha wabongo, ni picha ya AI ambayo official White House social media waliunda sababu ya kuhojiwa kwa Trump na kuulizwa vipi kama ukichaguliwa kuwa papa, akasema itapendeza sana. Ingawa baadae alisema itakuwa vema conclave ikamchagua papa wa Kimarekani. Hivyo naposema katika siasa hakunaga ajali mnielewe.
 
Back
Top Bottom