Kanisa Katoliki lapata Papa mpya wa 267, ni Robert Francis Prevost kutoka Marekani, ataitwa Papa Leo XIV

Kanisa Katoliki lapata Papa mpya wa 267, ni Robert Francis Prevost kutoka Marekani, ataitwa Papa Leo XIV

Wakatekumeni mna shida sana. Sisi Walei tunawaangalia tu mnavyo hangaika na mambo yasiyo kuwa na tija. Kwani lazima Papa awe ni mtu mwenye ngozi nyeusi? Au anayetakiwa kuongoza Kanisa Katoliki ni Papa?

Mimi nimeeleza hayo niliyoeleza kutokana na sababu Maalumu kabisa nilizonazo, sijakurupuka !
 
Why do they choose Roman names ?​
Papa anaweza kuchagua ( halazimiki) jina la papa wa zamani ambaye anam-inspire katika utumishi wake, hii ikiashiria mwelekeo wa Papa huyo katika kazi zake. Majina yote yanaweza kutamkwa Kirumi au lugha yoyote, Mfano Francis aliitwa pia Francesco, sisi huku tulimwita Papa Francisco, au Papa Yohana Paulo wa Pili nk. Ni vile tu unavyotamka kwa lugha yako. Hata Yesu anatamkwa kwa namna nyingi sana depending na lugha mtu anaitumia.
 
Yametimia: Papa Mpya kutoka Chicago Marekani, Cardinal Robert Prevost, akichagua jina Papa Leo X1V:

Kwa wanauliza mambo haya yalianzia wapi:

Muda mfupi Yesu kabla hajakamatwa, alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi wake kama kawaida yake. Katika mazungumzo yake ya mwisho mwisho, Injili inatuonesha namna alivyomkabidhi Petro jukumu la kusimamia kanisa akisema maneno haya:

" Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni." Maneno mazito kwelikweli!


Baadaye tena alikuwa na mazungumzo tena na Petro:

"Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.” Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.” Akamwuliza mara ya tatu, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Hapo Petro akahuzunika kwa sababu alimwuliza mara ya tatu: “Wanipenda?” Akamwambia, “Bwana, wewe wajua yote, wewe wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu!

Yesu akaendelea kumwambia tena:

"Kweli nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.” (Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu)

Huyu ni yule Petro aliyedai hamjui Yesu usiku ule Yesu alipokamatwa, akaulizwa mara tatu akikana mara zote, mara ya tatu Yesu akageuka akamtazama, na jogoo akawika, kama ambavyo Yesu alimwambia itatokea. Udhaifu wa kibinadamu lakini kazi aliiweza.

Naam, safari ya Petro haikuwa rahisi. Baada ya kusimamia kuimarisha Ukristo yeye na wenzake, Petro alisulubiwa kwa amri ya Nero, mtawala wa Warumi, akining'inizwa miguu juu kichwa chini katika eneo linaloitwa sasa St. Peter's Basilica,eneo maalum kwa makusanyiko ya waumini Katoliki kote duniani, eneo ambalo watu walimwaga Papa Francis na walimsubiri Papa mpya, mjini Vatican ( ambao upo katikati ya mji wa Rome 🤣🤣)


Historia ya Papa huyu mpya wa kwanza kutoka Marekani, inaanza leo, akiwa amebeba jukumu alilokabidhiwa Petro, na mrithi wa Petro, na kuendelea, kuwachunga kondoo wa Bwana wanaokadiriwa kufikia 1.6 bilioni.

Tumuombee!
Umeeleza vizuri
 
I used to think Catholics pick their Popes from a smoking goblet. A sign of divine providence. It's all banter. These eunuchs run brutal campaigns along the Vatican boulevards 🤣🤣🤣​
Hichi ni kingereza cha Tanganyika au umekopa kutoka uRaya?
 
Katika hali ya kawaida, hivi wewe kwa akili yako uliyonayo ulitarajia kabisa kwamba mtu mweusi kutoka katika bara la Afrika angeweza kuchaguliwa kuwa Papa wa Kanisa Katoliki duniani?? Seriously???
Mimi binafsi niliwahi kueleza bayana hapa mtandaoni kwamba kwa Sasa haupo kabisa uwezekano wa kuweza kuchaguliwa kwa Papa Mwafrika (Mtu Mweusi), completely impossible!
Kuna ulazima gani Papa awe mwafrika ?...kwanini asiwe Muhindi, Muarabu n.k
 
Papa anaweza kuchagua ( halazimiki) jina la papa wa zamani ambaye anam-inspire katika utumishi wake, hii ikiashiria mwelekeo wa Papa huyo katika kazi zake. Majina yote yanaweza kutamkwa Kirumi au lugha yoyote, Mfano Francis aliitwa pia Francesco, sisi huku tulimwita Papa Francisco, au Papa Yohana Paulo wa Pili nk. Ni vile tu unavyotamka kwa lugha yako. Hata Yesu anatamkwa kwa namna nyingi sana depending na lugha mtu anaitumia.
Francesco is a latin name.
 
Ila sisi Wakatiliki wala hatufikirii hivyo vitu. Kwetu sisi tunapozungumza kanisa ni kitu kimoja hatuna mipaka ya kidunia, ni mwili mmoja wa Kristo, ambaye alikufa kwa ajili ya yeyote anayeridhia aokolewe naye. Huyu ni Mmarekani ambaye alikuwa akichunga kondoo wa Bwana huko Peru kabla hajahamia makao makuu, na anaweza kuongoza hadi akafa hajafika kwa Trump, ila akatembelea maeneo yenye uhitaji duniani kwa kadri anavyoongozwa na Roho Mtakatifu, eneo lake ni kubwa mno hata hawafikagi kote hadi wanakufa.

Ila komenti yako imenifanya nipaliwe kwa kucheka, ningekufa leo 🤣🤣.
Ingekua wakatoliki wote ni kitu kimoja basi angekuwepo Papa muafrika, hamna umoja wowote mnabaguana ndani kwa ndani
 
Sawa, lakini bado ni coincidence tu.

Najua watu wanapenda kujiumbia nadharia njama zao vichwani.

Hakuna ushahidi wowote ule kuwa Trump kahusika hapo.

Kwanza kisiasa Papa Leo na Trump hawafungamani kivile.
Wataalamu wa nadharia njama watapinga hili.

Mathanzua
 
Sawa, lakini bado ni coincidence tu.

Najua watu wanapenda kujiumbia nadharia njama zao vichwani.

Hakuna ushahidi wowote ule kuwa Trump kahusika hapo.

Kwanza kisiasa Papa Leo na Trump hawafungamani kivile.
Trump na Pope Leo wote ni mafirimason. Wanajuana.

Kaangalie kwenye peji ya DA MANGE kuna udaku wote wa Pope Leo.

Cc: Pdidy
 
Maandiko kwenye Biblia yanaonyesha viongozi hawakuchaguliwa bali waliitwa na bwana kwa nyakati tofauti. Hii ya Vatican naona haina tofauti na michakato ya nafasi za kisiasa au ile ya katibu mkuu wa UN.
Bado hujasoma Biblia
 
Sawa, lakini bado ni coincidence tu.

Najua watu wanapenda kujiumbia nadharia njama zao vichwani.

Hakuna ushahidi wowote ule kuwa Trump kahusika hapo.

Kwanza kisiasa Papa Leo na Trump hawafungamani kivile.
Ndio hakuna ushahidi wala uthibitisho wowote wa Trump kuhusika.

Lakini hii coincidence inatafakarisha sana.
 
Trump na tamanio lake....limetimia. Trump hakuvaa hivi kama wanavyopotosha wabongo, ni picha ya AI ambayo official White House social media waliunda sababu ya kuhojiwa kwa Trump na kuulizwa vipi kama ukichaguliwa kuwa papa, akasema itapendeza sana. Ingawa baadae alisema itakuwa vema conclave ikamchagua papa wa Kimarekani. Hivyo naposema katika siasa hakunaga ajali mnielewe.
Kaka unatafutwa kule kwenye jukwaa la Asenali.
 
Trump na tamanio lake....limetimia. Trump hakuvaa hivi kama wanavyopotosha wabongo, ni picha ya AI ambayo official White House social media waliunda sababu ya kuhojiwa kwa Trump na kuulizwa vipi kama ukichaguliwa kuwa papa, akasema itapendeza sana. Ingawa baadae alisema itakuwa vema conclave ikamchagua papa wa Kimarekani. Hivyo naposema katika siasa hakunaga ajali mnielewe.
Weka uthibitisho na ushahidi hapa.
 
Back
Top Bottom