PostGE2025 Kanisa Katoliki limetoa maagizo ya tangazo la misa ya kuwaombea watu waliouawa 29 Oktoba 2025

PostGE2025 Kanisa Katoliki limetoa maagizo ya tangazo la misa ya kuwaombea watu waliouawa 29 Oktoba 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Kanisa Moja la Mitume.
Roman Lacuta Causa Finit East.

Ndugu zetu wapumzike kwa Amani.
Na Walaaniwe wale waliofanya Ule Unyama.
Waliohamasisha machafuko,na vitendo vya ugaidi,uporaji na uharibifu wa mali za Uma na Mali za raia wasiokuwa na hatia pia walaaniwe sana.
Kama si vitendo hivyo vya uhalifu vilivyofanywa na watu wasiolitakia mema taifa hayo mauaji yasingetokea.
 
Kwa kua ni Kanisa Katoliki hawana ubavu wa kuzuia
Wazuiwe kwani hayo maombi yao yana madhara gani kwa serikali? Semeni maandamano muone kama mtaruhusiwa!. Hayo maombi mtafanya, serikali itawapuuza na maisha yataendelea!
Polepole hatopatikana na Nchimbi hataonekana hadharani na maisha yataendelea!
Hawa maaskofu serikali ilishaona kuwa dawa yao ni kuwanyamanzia kwakuwa KELELE ZA CHURA HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI!.
 
Misa hiyo ni muhimu sana, sote tujumuike maana kwa kweli Taifa letu limeingizwa kwenye laana mbaya kabisa, laana ya umwagaji damu kama njia ya kutwaa madaraka kwa nguvu.

Tumwombe sana Mungu, atujalie kuwapata viongozi wenye upendo wa kweli, wapenda haki, wenye akili timamu ambao kamwe hawawezi kumwaga damu za binadamu wenzao kwaajili ya kupata madaraka.
Dr.Samia Suluhu Hassan na Deo Ndejembi na Mwigulu Nchemba ni viongozi wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hadi 2030. Na mh Deogratias John Ndejembi ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hadi 2040.
 
Nawaza tu neno kuu katika maombi hayo itakuwaje maana hapo bibi mdashi atasokotwa kwa neno hadi kichwa kiwake moto
Watazisokota roho zao wenyewe na watakufa kwa chuki zao walizonazo zinazotokana na udini uliopita kiasi.
Rais ana majukumu makubwa ya kuliongoza taifa na kuwatumikia watanzania waliomchagua kuwatumikia na haweziumizwa na maneno ya mipasho ya mashoga wanaoishi bila kazi kwakuwa kuna wajinga wanaowapa hela za bure kwa kisingizio cha kumtolea Mungu sadaka.
Kama watu wakigoma kutoka sadaka wataacha kutoa mipasho yao na watatafuta kazi ya kufanya kwakuwa hawatakuwa na hela za bure wanazopewa bila kufanya kazi yoyote.
 
Ndiyo kanisa linalojitahidi kuuishi upendo wa Mungu kwa vitendo. Huwezi kusikia Kanisa Katoliki likihamasisha chuki za kidini, upendeleo wa kidini, au kuhamasisha ulipizaji wa kisasi. Ni Kanisa ambalo linajitahidi kufuata mapokeo ya kiimani. Msingi wa ukristo kwa kadiri ya Mafundisho ya Kristo mwenyewe, ni upendo, haki, msamaha, huruma, wema, upatanishi, upendo usio na mipaka, kuunena ukweli bila ya hofu, kukemea uovu hata kwa ukali bila ya kujali anayeutenda huo uovu ni nani. Hakuna utawala au shetani anayeweza kulitisha Kanisa Katoliki lisiunene ukweli daima.

MAOMBI
Ee Yesu Kristo uliyetufundisha kuwa na upendo usio na mwisho, uliyetufundisha kuwa wakweli, na kwamba tuukemee uovu bila woga, tena kwa ukali, tunaomba hekima yako kwa watumishi wetu wa dini ii wayaishi mafumdisho yako kwa vitendo, na kamwe wasiwe waungaji mkono wa uovu wowote wa watawala au kwa sababu ya woga au pengine kwa kupewa hongo yoyote ile. Tunaomba kila kauli ya kweli na ya kukemea uovu, itokayo kwa mtumishi wako, ikapate nguvu kwa watu wote na ikabadilishe mioyo ya waovu, wakurudie wewe Bwana wa haki, ukweli na upendo. Tunaomba ukamnyong'onyeshi na kumshusha yeyote mdhulumu haki asiyetaka kuujutia uovu wake na kukurudia wewe Bwana wa haki.

Wewe Bwana Mungu wetu unajua jinsi watawala wa nchi wanavyowaonea watu wako kwa sababu tu wana nguvu za kuwaua, kuwateka na kuwabbikia kesi za uwongo ili kuwatesa. Tunaomba utusamehe pale tulipokengeuka na kuwashangilia wadhulumu haki, tunatubu makosa yetu, tunaomba ukatujalie ufahamu mpya ili daima tukufuate wewe Mungu wetu, Mungu wa HAKI na UPENDO., Tunaomba utujakie hekima yako ili tuchukie udhulumaji haki na maovu mengine yote. Mkono wako wa baraka na Ulinzi, tunaomba ukapate kuonekana kwao watafuta haki ili siku moja nchi yetu ikapata kubadilika na kuwa nchi ya haki, upendo, amani na umoja.
 
ni muhimu sana hata yule albino alieuawa na Padre nae aombewe, pamoja na familia yake iliyosahaulika nadhani itapendeza zaidi gentleman🐒
Inaonesha yale mauaji ya oct 29 yalikufurahisha sana. Yaani hata kuwaombea wale mliowauwa unakereka.
Kweli mmelaaniwa na CCM yenu.
 
ok.
sawa na ibada ifanyike kwa amani.

msisahau pia kuwaombea na wale wote walio athirika baada ya dhuluma za kingono kama vile kupigwa mimba na kulawitiwa na mapadre na viongozi mbalimbali wa kanisa dunia kote na Mungu wa huruma awajaalie faraja ya amani mioyoni mwao na itapendeza zaidi 🐒
Tutawaomba na viongozi wasaga
Ulisagwa mkuu?!+😳😳😳 Pole sana
Wewe na mimeo ni victims
 
Kuna muda ni ngumu sana kuliondoa kanisa katika matukio yaliyotokea, mwaka jana waliandaa tukio same dates. This time wanarudia kosaa lilelile. Any way huenda sio kosa ila ukisoma ni kama kuna ushari ndani yake.

Mwisho..... dini zipo, zina nguvu na kwa sehemu kubwa hutumika. Tanzania ipo na ni ya wote. Kila la kher

SITASHANGAA KANISA KUINGIA KWENYE MTEGO AMBAO KUTOKA ITACHUKUA MUDA MREFU. ILA SITASHANGAA PIA KUONA SERIKALI IKABILIANA NA MTEGO WOWOTE
 
Tunayasasubiria na makanisa ya walokole, wauza keki, mafuta, maji na vitambaa nao waseme siyo wanapiga biashara tu
 
ni muhimu sana hata yule albino alieuawa na Padre nae aombewe, pamoja na familia yake iliyosahaulika nadhani itapendeza zaidi gentleman🐒
kuna baadhi ya waamini wa kanisa katoliki siku hizi wanakimbia misa zinazo ongozwa na fr. Kitima sijui kwanini?

au kanisa nalo linafukuta ndani kwa ndani na limegawanyika kiaiana right?🐒
Fr.Kitima kila mkisikia jina lake vinyeo vinawawasha, mkiona sura yake nyuso zinanyong'onyea, mkisikia sauti yake matumbo yanawashika, kwanini mnachukia wanaowaambia ukweli? Uchawa na ushoga ni vitu viwili vyenye laana hapa duniani. Yeyote anayekuwa shoga ameshalaaniwa hali kadhalika machawa wote wameshalaaniwa piq
 
Misa nchi zima, Kanisa limeagiza Kesho watangaziwe kwenye jumuiya ndogo ndogo, jumapili tutangaze kanisani, na wiki yote inayofuata Itakuwa ya kutangaziana.

======

Mwadhama Kardinali,

Wahashamu Maaskofu Wakuu,

Wahashamu Maaskofu.

Bwana Awape Amani!

YAH: WITO WA KUADHIMISHA MISA TAKATIFU KWA NIA YA KUOMBEA MAREHEMU NA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU SIKU YA TAREHE 29 ОКТОВА 2025​

Kwa moyo wa kichungaji na kwa kutambua wajibu wetu wa kuliongoza Taifa la Mungu katika ukweli, haki upendo na mwanga wa Injili. Kwa barua hii nawaalika kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuliombea Taifa letu la Tanzania na sisi wenyewe. Katika kutimiza mwaka. moja tangu uchaguzi wa mwaka jana, tunakumbuka baadhi ya watu wetu kuumizwa, kupotea na hata kuuawa. Hali hiyo ya maumivu na msiba bado ipo kati ya watu wetu.

Katika mazingira haya, tunaitwa kusimama pamoja kama jumuiya ya waamini, tukimkabidhi Mwenyezi Mungu mwenye huruma Taifa letu, viongozi na watu wake. Tukiomba umoja, upendo, ukweli, mshikamano ambavyo ni matunda ya haki na amani. Kwa sauti ya upole, unyenyekevu, unyofu na majuto tuombe faraja kwa wanaolia, tumaini kwa waliokata tamaa, imani kwa wenye mahangaiko, haki na ukweli kwa waliopotea, busara kwa wasioelewa, uponyaji kwa wenye majeraha na upendo kwa wenye chuki. Pia huruma ya Mungu kwa wale waliotangulia mbele ya yake.

Tunaomba Misa Takatifu ziadhimishwe kwa nia hizo; walioumizwa, kupotea, kuuawa na kuliombea Taifa letu. Tunashauri Misa hiyo ifanyike katika Parokia, vituo vya sala na Taasisi za Kanisa kadiri iwezekanavyo siku ya Alhamisi 29 Oktoba 2026. Misa inaweza kufanyika asubuhi muda wa kawaida, au muda wowote unaofaa. Masomo ya siku au ya kuchagua yanaweza kutumika kwenye Misa hiyo.

Tukizidi kuliombea Taifa letu, naendelea kumshukuru Mungu kwa kila moja wenu kwa upendo, uelewa, ushirikiano na majitoleo yenu yasiyokoma.

Katika utumishi, upendo na ukweli,

+ Wolfgang Pisa, OFMCap

Askofu wa Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
View attachment 3697014
Huyu ni Dini gani?
 

Attachments

  • IMG-20250122-WA0047.jpg
    IMG-20250122-WA0047.jpg
    32.8 KB · Views: 7
Fr.Kitima kila mkisikia jina lake vinyeo vinawawasha, mkiona sura yake nyuso zinanyong'onyea, mkisikia sauti yake matumbo yanawashika, kwanini mnachukia wanaowaambia ukweli? Uchawa na ushoga ni vitu viwili vyenye laana hapa duniani. Yeyote anayekuwa shoga ameshalaaniwa hali kadhalika machawa wote wameshalaaniwa piq
waamini wake si ndio kama wewe tu, yeye mlevi, mzinzi, muongo, mchochezi halafu anakimbilia madhabahuni kana kwamba yeye ni ni mfogo wake yesu :pedroP:


halafu wewe na wenzako pamoja na kwamba mmepokea ekaristi takatifu na kipaimara but, shetani bado anawapiga magoli daily ndio maana hamuachi kutukana na kuporomosha matusi jukwaani eti ndio mnamtetea mtakatifu kitima:pedroP:
 
Nitavaa nguo nyeusi full siku nzima na misa nitahudhuria St Joseph. Tumsifu Yesu Kristo....
 
Hili kanisa linaongozwa na wasomi hasaa. Hawababaiswi ,hawana uchawa , na hawacheki na manyani ,makunguni na zaidi hawasapoti wauaji , watekaji ,na majizi .
 
Asante sana kwa mtazamo mzuri ulionao! Kuna wanaodhani dr.Samia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anaogopa kelele za makanisani!.
Kama Polepole na Nchimbi wameminywa kimyakimya na maisha yanaendelea , hao maaskofu pia watapiga kelele na serikali itawapuuza na maisha yataendelea!.
Hakuna aliemuogopesha rais, ni maamuzi yetu. Wewe kama umeona tunamuohopesha ni wewe na mtazamo wako.
 
Mimi ni Mkatoliki niliyepokea Sakramenti zote kama MLEI isipokuwa Sakramenti ya Mpako Mtakatifu wa Wagonjwa kwa maana ya;
i) Nimebatizwa katika Kanisa la Mtakatifu Peter Oystebay mwaka 1978.
ii) Nimepokea Ekaristi Takatifu mwaka 1985 Parokia Mpya (wakati huo) ya Mtakatifu Maximilian Kolbe, Mwenge.
iii) Nimepokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara Parokia ya Kabashana, Buyango, Jimbo Katoliki Bukoba mwaka 1988.
iv) Nimefunga Ndoa Takatifu mwaka 2005 katika Parokia ya Mt. Justine Bujora (kwenye nyoka za Wasukuma, ahahahahaha) mwaka 2005.
Pia ni Mwana Jumuiya ndogo ndogo mwenye IMANI THABITI na dini yangu ya Kanisa Moja Katoliki la Mitume LAKINI sipo tayari kushiriki UJINGA unaoenezwa na kusambazwa na wajinga wajinga!
Wewe ni mkatoliki uliyekengeuka , hatukushangai
 
Cha ajabu kuna watu wanakereka sana na haya maombi, tuwafikirie vipi nyie?
 
Back
Top Bottom