Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023

Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023

Jifunze kuvumilia dhana na maoni ya wenzio.Tofauti na hapo tusi linadhihirisha kitu ndani yenu ambacho ni asili yenu na wewe unakipinga kwa maneno matamu.
Jikaze tu ingekua la maana huyo alievunjwa mguu hapo angejitetea kabla ili asidhalilike kiasi cha kugalagala wakati kashakua ni yesu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Matusi ya nini?Najitahidi kufikiria kutokana na alichosema mchangia mada.Kwamba watu wakisilimishwa lazima wakakomoe huko walikokua
Matusi yako wapi? Kwahiyo wewe ukiambiwa jambo basi unalibeba tu kama lilivyo bila kushirikisha kichwa chako?

Hakuna watu ambao wakisilimishwa lazima wakakomoe huko walipotoka,ingekua ni kweli basi haya matukio yangekua yanatokea kila siku.
 
hili nalo linawezekana asilimia mia moja. Wale watumishi hawana maadili kama wanavyotuaminisha tuamini ni watumishi wa Mungu. Kuna paroko mmoja ilibidi nimvae mzimamzima baada ya kuanza kunikemea kiholela nilipoazimwa ngazi na mlinzi wa kanisa, wakati ngazi ilikuwa inatumika kwa wapangaji wao wa fremu. Ile nairudisha nikakutana na huyo paroko akaanza kunipakia maneno makali bila kujali kwa wadhifa wake hapaswi kutamka maneno yale kwa mshirika wake au kwa yeyote yule. Mimi si mkatoliki lakini nilizaliwa kwenye ukatoliki, hivyo naujua ukatoliki vizuri. Ilibidi nimpe somo huyo paroko bila kujali heshima yake. Mpaka sasa huyo paroko ana nidhamu kubwa na mimi na amekuwa rafiki yangu.
Mkuu mapadre wengi hawana maadili. Kuna mmoja alikuwa parokia ya Mhonda alipoka mke wa mtu na akazaa nae watoto mapacha.
Kanisa likapotezea kwa kumhamisha, jamaa akahama na yule mke wa mtu na wale watoto mpaka hii leo watakuwa chuo au wameajiriwa mahala.
 
Mkuu mapadre wengi hawana maadili. Kuna mmoja alikuwa parokia ya Mhonda alipoka mke wa mtu na akazaa nae watoto mapacha.
Kanisa likapotezea kwa kumhamisha, jamaa akahama na yule mke wa mtu na wale watoto mpaka hii leo watakuwa chuo au wameajiriwa mahala.
hata masista nao si kama tunavyodhani. Kuna sista moja hakuwa na huruma kwa watoto wa wanawake wenzake, huenda ikawa ni kwa sababu hawajui uchungu wa kuzaa. Huyu sista alikuwa mmoja wa masista waliokuwa wanafundisha masomo yao katika shule moja kongwe ya serikali iliyowahi kutoa tanzania one ya 7 miaka ya nyuma.

Huyu sista alikuwa anatoa adhabu ya kulima nyasi kwa vidole, na kutokuingia darasani siku nzima unakosa masomo kama hutarudi jioni kumwagilia maua kwenye eneo la kitengo chake alichokuwa anakisimamia shuleni. Alikuwa hana urafiki na wanafunzi asiowajua wazazi wao ni kina nani
 
Geita, pengine kwa sasa ndio mkoa unaoongoza kwa matukio mabaya yanayohusishwa na ushirikina.

Jamii inayoendekeza ushirikina wa aina ile ya kutoa makafara na kuuana, huwa hawana kiasi.

Naangalia kama ni moja ya matukio hayo. Muda utaongea.
 
Back
Top Bottom