Kanisa limepiga marufuku wanasiasa kusalimia kanisani, wamekosea sana

Katoliki ndio limepiga marufuku.Waende KKKT wakafanyie huko, waende kwa Tapeli Mwamposa,kwa Katunzi ukonga, KUHANI MUSSA na kwa Geodevie Katoliki hatutaki huo upuuzi!! 🤔🤔
 
Orthodox ni kanisa la Urusi baada ya vila ndo hayo yametokea, Narudoa tena serikali haiwezi kuiguta RC, sababu ziko wazi RC ni kubwa kuliko Ccm na majamaa yameenda shule sio mafala, kuna majadusi huko RC wako na intelligence kuliko TISS
Roman Empire ni top. Ona Pope anachaguliwa na Cardinals ni cheo cha jeshi hichi.
 
Kiongozi wa ki serikali au taasisi nyingine akiwa kanisani ni muumini kama muumini mwingine.
Wanatakiwa kutoa hotuba, salamu na maelezo kanisani au misikitini ni viongozi wa dini na wasaidizi wao tu.
Hivyo ndivyo tutakavyodumisha undugu na umoja wa kitaifa.
 
Sisi Katoliki hatutaki kuwapa nafasi wanasiasa kuongea,wala kusalimia kanisani!! Yapi mengi mno makanisa!! Mnaweza kwenda huko sioni shida yoyote, ila ACHENI kung'ang'ania madhabahu ya kanisa Katoliki 🤔🤔
 
Jenga na sajiri kanisa lako uwaite waje waropoke,sisi Katoliki hatutaki
 
Wewe siyo mkristo unaumiaje na hili?
 
kama watu wa kanisa wako wengi humo serikalini basi kumbe kanisa linahusika na utekaji pia kama serikali ndiyo inateka watu
 
Sasa hivi tutafuta makanisa yooooote na kuyasajiri upya kwa sheria na mashariti yaliyoboreshwa, mojawapo ni kanisa kuweka milango wazi kwa wataalam na wanasiasa wa chama tawala kuningia na kutoa ujumbe wenye manufaa kwa raia na taifa kama vile sensa, covid, uchaguzi mkuu, rushwa, ulawiti, ushoga, nk kwenye nyumba za ibada. Hakuna sekta yoyote ambayo haina regulator.
 
Kuwazuia viongozi wa kidini kuongelea maswala ya siasa ni ujinga pia
 
Wamepatia Sana, walikuwa wanachanganya dini na siasa
 
Kanisani ni mahali pa ibada, watu wamekuja kusali, hivyo blah blah za wanasiasa hazina nafasi. Kanisa katoliki lilichelewa sana kuja na hilo tamko.
Na ndio maana wakileta siasa kwenye nyumba za I ada kama Fr. Kitima na Gwajima "wanashughulikiwa"!
 
Ni hivi haina uwezo na haitakuja kuwezaaaa.
 
Ni muhimu mahali POPOTE pa ibada pasitumiwe kisiasa au wanasiasa wasipewe jukwaa humo. Nenda pahala pa ibada, Fanya ibada, toka, ingia mtaani uanze siasa.
 
Kama wiki mbili zilizopita tupo msibani Mhe Diwani alipewa nafasi ya kuongea neno baada ya kumaliza alichoongea akawaambia waombolezaji wapige makofi mengi kwa mama aibu iliyompata anaijua mwenyewe.
 
Wapo kwenye ushindani ndio maana watu wanasema wana muonea rais kisa dini nyingine
Labda maana yake ni kwamba serikali ina uwezo wa kufuta si tu kanisa bali hata kufuta kila kinachohusiana na kanisa zikiwemo hizo huduma za kijamii ulizozitaja,watu wana jeuri aisee!
 
Ni muhimu mahali POPOTE pa ibada pasitumiwe kisiasa au wanasiasa wasipewe jukwaa humo. Nenda pahala pa ibada, Fanya ibada, toka, ingia mtaani uanze siasa.
Mtaani watu hawaji,hivyo tunawafuata wanakopatikana🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…