Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania imewatangazia kuanzia kesho Alhamisi bodaboda na bajaji zote hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji hilo.
=================
TAARIFA HII IMEKANUSHWA
Your browser is not able to display this video.
DAR: BODABODA WAPEWA VITUO 9 MJINI
Baada ya kudaiwa bodaboda na Bajaji za biashara zimezuiwa kuingia Mjini Jijini Dar es Salaam, mamlaka zimekanusha zuio hilo na kuelezea kuna vituo 9 vimetengwa maalum kwa vyombo hivyo, mchakato ukishirikisha viongozi wa Bodaboda, TARURA, Jiji, Polisi na LATRA.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng`wilabuzu Ndatwa Ludigija amesema kuwa utaratibu wa vituo hivyo utawapa urahisi wa kushusha na kupakia abiria na siyo vituo holela kama ilivyokuwa awali.
Aidha, Msemaji wa Shirikisho la Vyama vya Madereva Pikipiki Mkoa wa Dar, Tito Lazaro amesema: “Utaratibu huo utapunguza uhalifu kwa kuwa kuna wasimamizi, mavazi maalum ya madereva, madereva watawasilisha nyaraka za utambulisho.
“Vituo hivyo ni Nasra Tower (Kariakoo), Sabasaba (Msimbazi), JK Park (Mnazi Mmoja), Fire, Mindu & Maliki (Upanda), Suwata (Kariakoo), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mnazi Mmoja na Kongo (Kariakoo).”
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania imewatangazia kuanzia kesho Alhamisi bodaboda na bajaji zote hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji hilo.
Nchi hiii inataka kujifanya ni NEW YORK CITY WAKATI BADO NI POLI KAZI KUUMIZA WALALA HOI HAYA MAAMUZI YA KENGE HAWA SIKU MOJA TUWACHENJIE BATA HAWA....
Wamejiajiri sawa ila miji council nayo ina mipango yake
Umesahau kuwa hii marufuku ilikuwepo tangu zamani na wahusika walitii . Ruhusa ya kuingia jijini ilikuja baada ya daladala kuzuia kusimamisha watu mwaka juzi
Kwahiyo kabla ya mwaka juzi watu walikuwa hawajajiajiri?
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam nchini Tanzania imewatangazia kuanzia kesho Alhamisi bodaboda na bajaji zote hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji hilo.