Kariakoo haina umuhimu kwa uchumi wa nchi kama tunavyo aminishana Bongo lala

Nimemsikia mwenyekiti wa wafanyabiashara wa kariakoo anasema kwa mwezi Kodi inayopatikana Kariakoo ni bilion 14 , mbona kidogo sana?!
 
Kariakoo ni mkoa wa kikodi , watu kutoka nchi jirani wamejaa kariakoo kununua vitu.. wa comoro wamejaa kariakoo wakifunga mizigo..
Hili haliondoi ukweli kwamba ni eneo linalochangia pakubwa Tanzania kutofikia uchumi wa viwanda.
 
Karikoo ni TRADING ECONOMY ni uchumi unaojitegemea na hakuna nchi isiyofanya TRADING meli haziji TZ tu daily Meli zipo baharini kupeleka bidhaa kila sehemu ya Dunia.
Mzigo kiasi gani unatoka Kariakoo kwenda China?
 
Ndio vinatakiwa vipromotiwe, mapinduzi ya viwanda hayaji kwa kuoenda vya nje, Hii nchi inaend akuwa Dampo la kudumu la bidhaaa za nje
Imeshakuwa dampo la bidhaa za nje siku nying sana, hadi sukari na mafuta ya kula vinaagizwa kutoka nje!
 
Sawa, lakini tujiulize kama visipokuwepo hizo bidhaa za China n.k. wafanyabiashara watauza nini? Nchi hii hata sabuni ya mche ya kufulia zinaagizwa nje. Kuna mahali tumekwama.
 
Akikupinga hapa wala usimjibu, mpuuze.
 
Viwanda havijenngwi na Chama vinajengwa kwa Sera nzuri ambazo Bongo hazipo, tumekalia siasa za Uchawa tu na kudanganyana
Serikali gani iko madarakani?

Serikali ipi ilianzisha , ilirithi na kuendeleza na hadi kuua mamia ya viwanda ?

Tanganyika packers inaendeleaje?

National Milling cooperation inaendeleaje?

TANALEC inaendeleaje?

UFI inaendeleaje ?
 
Itabeba products za kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, Burundi na Rwanda. Afrika inalo tatizo la wanasiasa kudanganywa na wazungu na wao kugeuka tegemezi bila hata ya kupanua fikra zao juu ya nini wanachoweza kuuza huko nje.

Wazungu wanatumia sana hii mbinu ya kuwapumbaza viongozi wetu lakini tuna kila sababu ya kutazama SGR zaidi ya moja kwa uchumi mpana wa afrika na kwa kuanzia kwa faida ya hizi nchi za afrika mashariki na kati.
 
Mwa ujuavyo nchi yako uchumi wake unatokana na kuinport au kuexport? Katika mzan wa %

Ukipata jibu
Hutoibeza kariakoo ndo kitovu cha uchumi wa nchi kibiashara
 

Unachokieleza ni sahihi kabisa. Lakini kwa upande mwingine ni kuwa kwa kuwa tumekosa uzalishaji kutokana na sera mbovu za uchumi za Serikali, japo kiuhalisia uchuuzi una nafasi ndogo katika kujenga uchumi wa nchi, lakini angalao huo uagizaji nje hizo bidhaa duni za China, na ndiyo unaowahakikishia wananchi upatikanaji wa bidhaa. Wananchi hawana namna kwa sababu upeo wa viongozi wa nchi katika masuala ya uchumi ni hafifu sana.

Msululu wa kodi kwa viwanda, sera hovyo za uchumi uchumi, na sheria zinazobadilika kila mara kwenye uwekezaji, zinazuia kabisa ukuzaji wa viwanda.
 
Acha kudanganya , uchumi wa nchi hii unategemea kila mwananchi mwenye uhai , so kusema soko kama ilo halina umuhimu japo wanaondesha pale wapo na uhai na wana connection mbalimbali ya wafanyabiashara ndani ya nchi na kutoka nchi zinazotuzunguka ni uhuni wa kujifariji tu

Mfanyabiashara mmoja anaweza kuwa na connection ya wafanya biashasha wenzake 200 na kuzidi ndani na nje ya ichi usione watu wanafika pale kufunga mzigo ,unalija hilo , kama hujui tafiti ,msiipoteze serikali kwa mabandiko yenu uchwara , diplomacia inahitajika katika kutatua mgogoro huu sio ubabe au siasa

Nyie mnafikiri wapikao pale funga mizigo wanakuja tu , acheni ujua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…