Kariakoo haina umuhimu kwa uchumi wa nchi kama tunavyo aminishana Bongo lala

Hata China ukienda utakuta bidhaa za Japani, India Ulaya, Marekani na Korea kusini, Maada ngumu hii huwezi elewa.
Kariakoo pale ni asilimia 100, Kariakoo ni Dampo make pake ni asilimia 100
Wewe uwezo wako ni mdogo sana wa kuelewa mambo

Kwani ni Mchina anayeleta bidhaa Kariakoo au ni wafanyabiashara wa Tanzania ndio wanaonunua bidhaa kutoka China?

Ilitakiwa ujiulize, kwani nini wafanyabiashara wa Tanzania hawaleti bidhaa za mataifa mengine bali wanaleta hasa za China?

Maada ❌
Mada
 

SGR itakuwa ya kupigia picha watawala ili waweze kusifiana.

Watawala wetu upeo wao ni duni sana. Uliza kwa wenye viwanda, usikie upofu wa watawala wetu. Kwenye viwanda kulikuwa na kodi 41, wanajisifu kuwa wamepunguza, sasa kodi kodi na tozo, jumla zimebakia 38. Botswana kodi na tozo, kwa pamoja, marufuku kuzidi 6.

Kwa watawala wetu hawa wasiojitambua, ni muhimu sana kuwa na katiba imara inayowaongoza. Yaani katiba itamke kuwa kwenye viwanda kodi na tozo ni marufuku kuzidi 4, kwenye bidhaa za nje, zisioungue 6.
 
Haiondoi neno Dampo, Kariakoo ni Dampo la products za kigeni, shida wana siasa wanawadanganya sana, mitaji haibadili ukweli, maada ngumu huwezi elewa
Unawalaumu watu wa kariakoo au wanasiasa kutokua na viwanda lawama unawapa watu wa kariakoo
Kama kariakoo hakuna umuhimu unataka watu wahishije kumbuka Tanzania hakuna viwanda, ajira ni finyu unataka watu waishije

Tatizo la vijana wanaokula ugali wa shikamoo ndo hili
 
Hembu tulia uandike kwa utulivu, ulichokiandika hata wewe mwenyewe unaweza usikielewe.
 
Huu ni ujinga kuanza kuleta propaganda ilihali tatizo lipo, dawa ya tatizo nikulitatua na sio kuleta blahblah.

Matatizo ya Wafanyabiashara sio Kariakoo tu ni matatizo ya Wafanyabiashara nchi nzima, hao wakariakoo ni wawakilishi tu.

Ni ujinga sana kusema Kariakoo haina umuhimu wowote wakati ndio moja ya business hub kubwa kabisa Tanzania na East Africa.
 
Mkuu wangu kuna mambo ya hovyo sana tz hasa katika uwekezaji na kufanya biashara.

Siku moja nipo mkoa flani hivi nakutana na bwana mmoja alitaka kuanzisha shule ,majengo yanaendelea ,amepita kote amefaulu ila inakujq kwa bwana afya tu wa wilaya husika ,ameenda amekagua sasa kutoa report ya ukaguzi wake ili uyu bwana kuendelea na hatua nyingine ,ikawa njoo kesho njoo kesho kutwa

Sasa kwa ujinga wa namna hii nani atataka wekeza , yani mtu kaisha pata vibali vyote ,ila ofisi moja tu ndo inaona ipo na umuhim kuliko ofisi zingiene
 
Wabongo kitu pekee tunacho weza kufanya kwa weledi wa hali ya juu basi huwa ni KULALAMIKA, KULIA LIA na KUKOSOA

Tz hakuna kiwanda cha nguo, viatu, simu, kompyuta, simu, tv, radio nk nk....... Lakini wanao leta hizo bidhaa ambazo ni muhimu na za lazima kwenye maisha unawaita HAWANA UMUHIMU WOWOTE

Badala tuchangamkie fursa ya kujenga viwanda sisi tunalia lia eti katiakoo hai hamasishi ukuaji wa viwanda Tz
Sasa sijui ulitaka Chalamila apige marufuku uagizaji bidhaa nje?

Mkuu swala la uchumi halipo hivyo, nchi inanunua kwa wingi nje bidhaa ambazo haizalishi
Kama tunataka hivyo tujenge kwanza viwanda vyetu
BTW unajua ni kiasi gani serikali inakusanya kwa mwaka pale kariakoo?
Unadhani ni kwa nini kariakoo ni “mkoa maalumu”wa kikodi?

Angalia tu sakata la sukari lilivyo
Serikali inalinda viwanda vya ndani kwa kudhibiti uagizaji sukari nje lakini bado viwanda vinasuasua tu

Ukweli ni kwamba Kariakoo ni MUHIMU sana kwenye kuchangia pato kwasababu hatuna viwanda mbadala vya kuzalisha bidhaa zinazoagizwa

Ni kazi ngumu sana kutuelewa Wabongo huwa tunataka nini haswa
 
Nadhani hiyo ndo sababu pesa yetu kukosa thamani kariakoo being a dumping place
 
Mwa ujuavyo nchi yako uchumi wake unatokana na kuinport au kuexport? Katika mzan wa %

Ukipata jibu
Hutoibeza kariakoo ndo kitovu cha uchumi wa nchi kibiashara
Kitovu cha kuwa kituo cha Ku import bidhaa za nje, Tungekuwa na viwanda vingekuwa na mchango mkubwa sana kuliko hio Kariakoo
 
Ile project ya ubungo ikishaanza kazi karikooo .ndo itakuwa imeisha... maana kila.kitu kitakuwa wazi leo hii kkoo kila mtu ana bei yake mkononi kitu hicho hicho
 
Sikiliza wewe ,ndio hatuna viwanda ,ila tuna wafanyabiashara wakubwa , kupita wafanyabiashara serikali inaweza kuamua tu kwamba

Kupitia wafanyabiashara tulionao ikaingiza mguu kwamba kama ni vifaa vya entronics, wafanyabiasha hawa ndo watakua wanaleta baada ya ushindanishi kutoka mataifa mbalimbali , kadhalika vyombo vya ndani n.k ,ila hata hivyo viwanda nani ameviua?
 
Mmh umesoma kweli alicho kujibu mkuu apo juu?
Je ulichokiandika pia umekisoma?

Jamaa amekujibu kiuchumi zaidi sio porojo Kama zako, inaonesha zahiri wew unakinga mkono mwisho wa mwezi..
 
Mmh umesoma kweli alicho kujibu mkuu apo juu?
Je ulichokiandika pia umekisoma?

Jamaa amekujibu kiuchumi zaidi sio porojo Kama zako, inaonesha zahiri wew unakinga mkono mwisho wa mwezi..
Hujaelewa pita kushoto ,kuchapia jambo la kawaida jf is my home ,hatuna mtiani wa kuandika hapa , nimekosea jiongeze
 
Mmh umesoma kweli alicho kujibu mkuu apo juu?
Je ulichokiandika pia umekisoma?

Jamaa amekujibu kiuchumi zaidi sio porojo Kama zako, inaonesha zahiri wew unakinga mkono mwisho wa mwezi..
Tuna wachumi uchwara tena wanikome, Mbunge Msukuma uchumi kasomea wapi ,na yupo na hela kiasi gani, Kishimba kasomea uchumi wapi ,nenda pale Dodoma mkabala na chuo cha mipango angalia kijiji kama sio makazi ya wapangaji alichofanya pale na je ni pale tu hulizia historia yake .

Mnakua na wasomi na wachumi wezi alafu unakuja na ujinga apa , niliowataja hapa juu sio kwa chuki ila japo hawajafika kidato cha nne akili zao zinafanya kazi sana na ndo watz tunawataka

Mchukue mmojawapo au aina hii ,mpe mwedo kasi ,au SGR au shirika la ndege au posta au yale mashirika ambayo yamejifia na wape mkataba wa miaka mitno huone nini watafanya watu wa aina hii kama sie wasomi hatutajiona wajinga , shida hii tz makaratasi imekua mizigo kwetu , unalikuta jitu profesa ila upeo wake zero , tuko kuitana dr, udr, unakusaidia nini kama hauleti impact ya maana katika jamii yako , ujinga tu,

Mimi sio ccm na siwezi kuwa ccm ila hao mamwamba nawakubali wanawakilisha kundi kubwa kwama maisha sio mavyeti au makaratasi japo ninayo ya kutosha
 
Founder wa jf anayo nafasi kubwa huko siku Mungu akimuita , umelifanyia jambo kubwa Taifa pitia platform hii ya jf , barikiwa na imekua .

Angalizo
Mkurugenzi jf nimekushukuru ila mie sio Chawa wako au Serikali ya ccm ila nimekushukuru na nitakuombea maana umetenda jema kuu kwa nchi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…