Huwa nazingatia yafuatayo;
1. Bajeti, sio nna laki mbili nitake simu ya laki tano....
2. Reviews, simu hata sifa zake zivutie vipi lazima nisome machapisho ya waliozitumia
3. Brand yake, mtengenezaji ni mhimu sana, kuna watengezaji hawaaminiki leo anatoa kitu kizuri kesho anachemsha, hao waepuke
4. Maisha ya hicho kifaa, kuna vifaa vizuri ila havina maisha marefu na kuna vifaa og unatumia mda kidogo hivyo inategemeana na lengo
5. Hadhi, kuna vifaa vyenye hadhi hata ukitaka kuuza husumbuki mfano samsung
6. Spare, kuna vifaa havina spare hapa nchini mpaka uagize nje na mafundi hawaviwezei vizuri
7. Uzoefu, kama nina uzoefu na kumpuni yenye huduma nzuri ntanunua hiyo sio kwenda na kila kampuni mpya inayozuka
Reuben Challe