Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

Pesa tu yatosha mkuu hata kama huna hekima utatumia pesa kupata wenye hekima watakuongoza na utawalipa ndio maana kuna wasomi wanaajiriwa kama managing directors kwa matajiri wasiosoma,dunia ya leo na hekima zako utaishia kudharaulika hata na watoto wadogo,..kuwa na pesa toa hata ushauri wa kipumbavu utaitikiwa ndio mkuu!
Ukichukuwa wenye pesa bila hekima ukawafungia kwenye kisiwa kimoja, alafu ukachukuwa wenye hekima bila pesa ukawafungia kwenye kisiwa chao unadhani ni kisiwa kipi kitafaa?
 
Ukichukuwa wenye pesa bila hekima ukawafungia kwenye kisiwa kimoja, alafu ukachukuwa wenye hekima bila pesa ukawafungia kwenye kisiwa chao unadhani ni kisiwa kipi kitafaa?
Yafuatayo yatajiri:

Wenye fedha:
1. Watauana kwa kuibiana fedha na wake/waume zao.
2. Watakosa ubunifu kwa kuwa hawana hekima.
3. Watahujumiana.
4. Hawatatembeleana.

Wenye hekima:
1. Watabuni vitu kutokana na hekima zao.
2. Wataamua magomvi kwa hekima hivyo watakuwa na amani.
3. Watapendana na kutembeleana hivyo watashirikiana.
4. Watakuwa na maendeleo kwasababu hawataibiana hekima.
 
umesema kweli mbaba suleiman hakuwa majalala kabisaa, lakin kumbuka pia suleiman huyohuyo hakuwa boya boya alikuwa na akili (hekima)

kuwa na hela zako jaza debe lakini bila akili (hekima) zitaishia kuziyeyusha kama siagi kwenye kikaango cha moto na utafanya mambo ya ajabu ajabu kama mwehu
Ukisoma vizuri kitabu cha mithali utagundua nambii suleiman alikuwa akitoa maneno yenye hekima zaidi na kuna hekima inatokana na binadamu kuitumia maarifa na ujuzi wa kidunia kufanikiwa kile anachokifanya kuwa tajiri na kuna hekima mtu anaipata kutokana nakuongeza bidii kumcha Mungu kuachana kabisa na maovu

Mithali 20:13 NEN​

Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
 
Hekima isiyoweza kuzalisha fedha au mali ni ujinga mtupu
Nawapenda wachaga kwao akili ni kitu kinachoonekana utaulizwa kama wewe una akili una shilingi ngapi tuonyeshe mali hizo akili zako ilizozalisha
 
Hekima isiyoweza kuzalisha fedha au mali ni ujinga mtupu
Nawapenda wachaga kwao akili ni kitu kinachoonekana utaulizwa kama wewe una akili una shilingi ngapi tuonyeshe mali hizo akili zako ilizozalisha
 
Mkuu,

Mandela alisema anataka aishi maisha ya zaidi ya thamani ya pesa, yaani hata kama hana pesa lazima atapata anachotaka kwa kutumia hekima, mfano ni nchi gani duniani ambayo Mandela angeenda kuomba chakula, nguo au matibabu ikamnyima? Hayo ndiyo maisha ambayo ni zaidi ya thamani ya pesa kwasababu aliwekeza hekima mioyoni mwa watu.

Nyerere kwa kutumia hekima yake aliwekeza kwa maskini na wanyonge duniani akawa hana maadui (kwasabbu maadui wanatengenezwa toka kwenye kundi la maskini wanaotafuta kujikomboa). Nyerere nyumba ya Msasani alizawadiwa na NHC, ile ya Butiama alijengewa kwa nguvu/ulazima na JKT, hakuwahi kujenga nyumba ya thamani ama kwa ela zake au ela za Ikulu. Kwa nafasi yake kama Mshauri wa Malkia wa UK Mwl alipewa nyumba Uingereza na Malkia akaikataa. Ni tajiri yupi basi mwenye ela asiyejuwa umuhimu wa kumiliki nyumba/makazi? Nyerere hakuwa na ela.

Nkrumah alitumia hekima kuasisi harakati za kudai uhuru na ukombozi wa Afrika, ikaja kumlipa uraia wa Afrika nzima badala ya Ghana pekee.

Katika kundi la marais tajiri Afrika Mandela, Nyerere na Nkrumah hawamo.
Nyumba ya Rais anajenga mwenyewe au anajengewa na serikali?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
I will name 5 most poor elites in the world's richest country:

1. James A. Garfield 20th US President.
2. Chester Arthur 21st US President.
3. Woodrow Wilson 28th US President.
4. Calvin Coolidge (a.k.a The Silent Cal) US President.
5. Harry S. Truman 33rd US President. Huyu amevunja rekodi ya umaskini katika safu ya marais wa US. Lakini pia Abraham Lincoln (aliyetoa tafsiri ya kimarekani ya neno Demokrasia alikuwa mchoma mkaa na aliwahi kushitakiwa kwa kesi ya kuharibu mazingira kabla ya kuwa rais)
If you are President of the richest country on earth being poor is a choice not inanyway an outcome.
 
Hautoweza kuwafahamu na hata ukitajiwa hautaweza kusadiki kwakuwa tu hawana fedha ambayo ingewasaidia watambulike.

Unategemea utajiwe watu wenye hekima zao vijijini huko ambao ni masikini utawajua?
Hao unaowaona vijijini wana busara tu hamna hekima mule usichanganye hii mambo,hamna mwenye hekima aliye maskini otherwise aone kuwa pesa hazikamilishi furaha yake and choose not to go for it.
 
Nani kakwambia Trump hana hekima?
Trump hana hekima ila kwa alipofikia kiuchumi hamna kitu ambacho atafanya kisiwe influential!

Not that kwamba yeye ni mtu mwenye hekima ila ni mtu ambaye ana ushawishi wa kifedha.
 
Mkuu,
Mbona Nyerere, Nkrumah na Mandela wamestaafu hawana ela ila hekima, na bado wanavuma kuliko wenye ela? Hii inakuwaje?
Nyerere alikua na pesa za kufa mtu. Kumbuka kipindi anastaafu, alizawadiwa ng'ombe na vitu vingi sana sema mzee yule hakujionyesha.
Nkrumah hakustaafu, alipinduliwa na waliompindua walimfuata huko huko Misti kwa wakwe zake kummalizia.
Mandela alikua na pesa
 
Hata Suleman aliomba hekima akapewa ni vingine.. Maandiko yanasema hajawahi kutokea wala hatokaa atokee mwenye utajiri kama wake.


Unamuiga huyo wakati Hakuwa na shida na pesa Kwa sababu kazaliwa kwenye familia Tajiri ya kifalme.

Mtu huomba asichokuwa nacho.
Sasa Suleiman alikuwa na Utajiri tayari na ufalme kutoka Kwa Baba yake ulitaka aombe tena mambo ambayo tayari anayo?

Alichokikosa ni hekima ndio maana akaomba hekima ya kumuwezesha kuzitumia pesa na ufalme wake vizuri.

Wewe ukiambiwa uchague cha kuomba usimuige Suleiman Mkuu
 
Ukiwa na hekima huku huna hela unaonekana zoba tu

Huyo mfalme Suleiman alikuwa na mali zote, hazina yake ilijaa na ndo maana kasema anataka hekima.

Usilinganishe nyakati
 
Trump hana hekima ila kwa alipofikia kiuchumi hamna kitu ambacho atafanya kisiwe influential!

Not that kwamba yeye ni mtu mwenye hekima ila ni mtu ambaye ana ushawishi wa kifedha.
My question still what makes you say that Trump hana Hekima?
 
Ukiwa na hekima huku huna hela unaonekana zoba tu

Huyo mfalme Suleiman alikuwa na mali zote, hazina yake ilijaa na ndo maana kasema anataka hekima.

Usilinganishe nyakati
Huwezi kuwa na Hekima ukawa kapuku.Ukiona mtu hana hela hiyo ni indication moja wapo kuwa hekima haimo kwake.
 
Back
Top Bottom