Kati ya Hekima na Fedha Kipi ni Muhimu Kuliko Kingine?

kwa sehemu upo sawa Mkuu,
isipokuwa, kuwa na hekima ama kuitafuta HEKIMA si kuwa MASIKINI.
Wala haimaanishi kwamba wenye HEKIMA ndio masikini.
Hivyo, ni heri kuwa na Hekima,
maana ni rahisi Fedha kumfuata mwenye Hekima.
 
kwa sehemu upo sawa Mkuu,
isipokuwa, kuwa na hekima ama kuitafuta HEKIMA si kuwa MASIKINI.
Wala haimaanishi kwamba wenye HEKIMA ndio masikini.
Hivyo, ni heri kuwa na Hekima,
maana ni rahisi Fedha kumfuata mwenye Hekima.

Kweli kabisa japo nimesimamia swali la awali kwamba kipi ni bora kati ya hivyo viwili kwamba katika choice hiyo huwezi kuwa navyo vyote
 
Nadhani tunashindwa kumuelewa Suleiman na mawasiliano yake na Mungu, na tunashindwa kutofautisha mtu mwema na mtu Mwovu, Suleiman alifanikiwa kuwasiliana na Mungu kwa utu wema wake tena akiwa mfalme akaulizwa apewe nini yeye akiwa mfalme tayari anakazi ya kumuingizia kipato na mtu mwema pia kwenye kazi yake na maisha yake ndipo alipoomba hekima Ili aitumie kwenye maamuzi atakayokuwa anafanya yawe ya hekima na kuacha kuomba mabaya kama kuua maadui zake au mambo mabaya ila aliridhika na kazi aliyokuwa nayo na kuomba aongezewe hekima ndipo Mungu akambariki kwa kuwa mtu mwenye Mali nyingi kwa kuchagua kuwa mwema badala ya kuomba mambo mabaya, Sasa mtu huna kazi alafu uulizwe upewe nini alafu ujibu hekima Sasa hizo hekima ukipewa uzunguke nazo kutoa hekima bila kazi siutazeeka ukiwa masikini? Hao wakina Trump ni kweli wanamali lakini tunawapima kwa wema au ubaya wao maana sasa tunamfumo wa sheria ndiyo zinazotumika kurekebisha watu wabaya na pia tunakuwa na watu wema na watu wabaya katika maamuzi yoyote yanayofanyika katika ngazi zote hivyo watu wanatakiwa kuangalia maana yoyote yanayofanyika je yatakuwa yenye haki au wema au yatakuwa yenye chuki au mabaya tofauti ni kipindi cha Mfalme Suleiman yalitoka kwa Mfalme pekee mpaka kwa mambo ya kifamilia kitu kutenda katika wema bila kuongozwa na nguvu ya ziada kutoka ndani ilikuwa ngumu kutoa majibu ya haki ndipo Suleiman akaomba Hekima yaani kutendea watu wake Wema na siyo ubaya kwa mambo yatayokuja mezani kwake kutolea maanamuzi.
 
Hiyo ni tofauti ya wema na ubaya, au watu wema na watu wabaya wakikaa pamoja nini watafanya na siyo Hekima aliyoomba Mfalme Suleiman, watu wawe na hela ila wawe wema na Hekima aliyoomba Suleiman ilikuwa ni kutenda wema au kutoa maamuzi yenye haki Sasa Kuna watu wameshindwa kutofautisha hekima ambayo ni haki ya kumtendea mtu anayestahili na maarifa au elimu ya kujielewa aliyonayo mtu.
 
Nimeipenda sana hii comment yako, we live in the world where people have forgotten what's real matters in our life.
 
Hakuna mwenye hekima asiye na Pesa.
 
kwahiyo, hapo napata ufahamu kwamba hekima aliyoiomba Sulemani, ilikuwa ni kitendea kazi ktk ofisi yake ya Kifalme. ASANTE kwa ufahamu huo.
Lakini Mkuu, unadhani HEKIMA ni nini na ina THAMANI gani hata kuthubutu kuilinganisha na FEDHA?
 
Ni maneno ya kufarijiana ukweli ni kamba pesa ina hitaji discipline ya hali ya juu kama huwezi kua nayo pesa utazisikia kwa majirani
Ndio kuna kitu wanaita "Nidhamu ya fedha" Ukikosa nidhamu ya fedha ,fedha hazikai mkononi zitakimbia zote!!
 
Weka pesa kwapani,
Kaa na Hekima kichwani. Utaona raha ya Dunia.
Kama Mao Tsetung alivyoweka kwapani US$ 13 ml na Fidel Castro $ 900 ml na wote kukaa na hekima kichwani. Huku mwenzao Nicolae Ceausescu akipokea mshahara wa 18.000 Romanian lei sawa na US$ 1200 kwa exchange rate ya mwaka 1989, akidhaniwa yeye na Mwl Nyerere ndiyo Marais Wajamaa waliojilipa mishahara midogo kuliko wote kwenye urais wao.
 
Trump hana hekima ila kwa alipofikia kiuchumi hamna kitu ambacho atafanya kisiwe influential!

Not that kwamba yeye ni mtu mwenye hekima ila ni mtu ambaye ana ushawishi wa kifedha.
Hekima yake ndiyo ilimfanya Mike Tyson akamuajiri, baada ya yeye Trump kupata pesa nyingi pesa hizo zikabomoa hekima yake. Kumbe pesa zinaharibu hekima lakini hekima haziharibu pesa, bora basi hekima kuliko pesa kama ni hivyo.
 
Hekima yake ndiyo ilimfanya Mike Tyson akamuajiri, baada ya yeye Trump kupata pesa nyingi pesa hizo zikabomoa hekima yake. Kumbe pesa zinaharibu hekima lakini hekima haziharibu pesa, bora basi hekima kuliko pesa kama ni hivyo.
Sawa mkuu
 
Zawadi za Nyerere za kustaafu walikubaliana na Mama Maria wakazichukuwa wakazipeleka Mwanza kuanzisha kituo cha yatima na zingine wakasaidia maskini wa Butiama ikiwemo kukodisha mashamba Butiama na kuanzisha kilimo cha kufa na kupona na mazao ya shamba waligawa kwa wanakijiji bure kwa wasiojiweza na kwa bei ndogo sana kwa wanaojiweza. Mimi nimeishi sana Butiama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…