ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
-
- #41
Sijui hata unazungumzia kitu gani?Katiba nayo inaendana na culture ya watu, maarifa na mwamko wao. Huwezi kulazimisha katiba ya kumbana kiongozi katika jamii ambayo hakuna utamaduni huo. Utamaduni wa Tanzania kwa sehemu kubwa ni wakubwa hawakosei, kuanzia kwenye familia, ukoo, mtaani mpaka ngazi ya taifa.
Hili IQ umekua ukirudia mara nyingiKatiba nzuri ni muhimu ila tatizo la Waafrika liko zaidi kwenye IQ kuwa ndogo kwa majority ya watu na utamaduni.
Swali lako ni paradox.Watanzania tunahitaji mabadiliko, na wengi tunaamini kuwa Katiba mpya ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo
Tunatarajia itasaidia kurekebisha mifumo yenye changamoto kupunguza migogoro na kuweka mipaka na uwajibikaji katika matumizi ya madaraka
Lakini binafsi napokua nafatilia mijadala kuna maswali hua yananijia kicwani
Moja ya swali ni hiliπ
JE, TUNAPIGANIA KATIBA MPYA KWA AJILI YA KUBADILISHA MFUMO, AU TUNATAKA KUBADILISHA CHAMA KILICHO MADARAKANI?
Kwa mfano, CHADEMA wakiingia madarakani je, bado tutadai Katiba mpya kwa nguvu ileile, au msimamo wetu utabadilika kwa sababu tu chama tunachokitaka ndicho kinachoongoza?
Tujadili: Je, tunataka mfumo bora utakaomfunga kila kiongozi, au viongozi tunaowaamini ndani ya mfumo uliopo?
Karibu kwa maoni π«‘
ShesRise_1 βοΈ
FactKatiba mpya itasimamia na kufanya mifumo thabiti na taasisi imara ambavyo vitasababisha automatic viongozi wawe bora bila kupenda au kutaka.
Swali lako ni paradox.
1. Ni dhahiri kuwa wa mfumo uliopo (status quo), CHADEMA au chama kingine chochote nje ya CCM hakiwezi kuingia madarakani.
2. Katiba ikiandikwa upya kiusahihi kurekebisha mfumo, CHADEMA au chama kingine chochote nje ya CCM kitaweza kuingia madarakani.
3. Chama kitakachokuwa madarakani baada ya marekebisho ya mfumo aka katiba mpya maana yake kitawajibika kuenenda kama katiba mpya aka mfumo mpya unavyodai.
Btw, wadau wa demokrasia hatuna chama tunachokitaka au kukipenda. Tunachotaka ni kuona utawala bora na wa haki unaongoza nchi, period.
Baada ya mabadiliko ya katiba, hata CCM ikitakaswa inavyotakiwa, ikakubaliwa na wapiga kura kuwa madarakani na kuenenda kikamilifu kama katiba mpya inavyodai, hatutakuwa na tatizo kabisa.
Shukran mkuu ni dhahiri watu wanataka Katiba mabadilikoKwa mtazamo wangu,dawa ya nchi hii ni kuwa na katiba ambayo itakidhi mahitaji na kutatua changamoto za nchi hii
Katiba tulinayo kwa kiasi kikubwa sana haina shida isipikuwa baadhi tu mambo ambayo labda inabidi yapewe kipaumbele zaidi, mfano matokeo ya uraisi kuhojiwa endapo kuna sintofahamu
Swala la wasimamizi wa chaguzi wasiwe sehemu ya mamlaka ya ya uteuzi
Majaji wawe wanateuliwa nje ya utawala wa namba moja
Na kero zote ambazo kwa katiba ya sasa haitatui changamoto hizo basi zitafutiwe ufumbuzi
Kuongozwa bila katika ni changamoto sana,kwasababu itategemea na huruma na utashi wa kiongozi,kuna siku tutapata kiongozi ambaye hafungwi na katiba na matokeo yake yatakuwa mabaya
Kwahiyo dawa ni kuwa na katiba ambayo itakuwa ni dira ya kila kiongozi ambaye atashika madaraka ya nchi,na hapo ndio tutakuwa tumepata muarobaini wa changamoto zetu mbali mbali ambazo zinatukabili
Kwahiyo tunafanyaje ?katiba kimaandishi ndo iko juu ya watu ila kiutendaji inatumiwa na watu..
watu wenyewe ndo sisi ambao kila mtu ni mwizi tokea ngazi ya familia, maisha ya shule na hata utafutaji...
kila kitu kinachoihusu Afrika kipo kiwiziwizi ... hata wenzetu Asia japo wapo chini ya influence ya mabeberu kama sisi lakini tamaduni na maisha yao ndo yanatutofautisha nao..
malezi yenyewe ni mabovu, kwamba mfano leo hii skendo ndogo tu pengine ya ngono inaweza kumaliza carrier ya msanii huko nchi za Asia lakini kwa sisi Afrika ndo unapata na kuongeza followers na ndo utafanikiwa zaidi..
ingelikuwa kuwa hili ni tatizo la baadhi ya nchi tu au viongozi basi angalua tungepata hata nchi moja ambayo pengine ngozi nyeusi yenyewe wameijenga na kuwa dunia ya kwanza...
Endelea kupambania familia yako..Kwahiyo tunafanyaje ?
Maana hapo hujasema nini kifanyike
Hovyo kabisaEndelea kupambania familia yako..
hakuna wa kumpambania na hakuna wa kukupambania,,,, kilichopo ni unafki na kila mtu anapambania maslahi yake..Hovyo kabisa
Then TL anasema ana watu anawapambania
Bora angevuta mpunga ale maisha
Wewe ni miongoni mwa hizo ng'ombe pia?hakuna wa kumpambania na hakuna wa kukupambania,,,, kilichopo ni unafki na kila mtu anapambania maslahi yake..
yeye avute mpunga tu,, aache ng`ombe ziendelee kuswagwa tu, ni stahiki yao..
sibishani na maono yako,,, ila ukiacha mihemuko utajua ukweli kwamba inabidi uipambanie familia yako na si kusubiri upambaniwe maana mfumo wa maisha katika bara lako la watu wenye ngozi nyeusi ulishaharibiwa kabla hujazaliwa... pole..Wewe ni miongoni mwa hizo ng'ombe pia?
Kuna sehemu nimesema nasubiri kupambaniwa?sibishani na maono yako,,, ila ukiacha mihemuko utajua ukweli kwamba inabidi uipambanie familia yako na si kusubiri upambaniwe maana mfumo wa maisha katika bara lako la watu wenye ngozi nyeusi ulishaharibiwa kabla hujazaliwa... pole..
endelea kusubiri kupambaniwa na TAL au usubiri maendeleo HEWA ya waliopo..
Hapana japo huwa nakwenda kule mara kwa mara.Wewe unatokea ule mkoa unaopakana na Kwa M7?
Kuna sehemu nimesema nasubiri kupambaniwa?
Hebu nioneshe hiyo sehemu?
Kwahiyo wewe unataka watu tusijadili kabisa ?
Then unahisi kua sifanyi mambo mengine ya familia
Nimeona kama sifa zipo juu kaka ndege π πHapana japo huwa nakwenda kule mara kwa mara.
Nawe pia pambania familia yakovizuri kama unaipambania familia yako...
Yeah, lazima ujisifu hapa duniani, la sivyo unaweza kuzikwa bila kuonja utamu wa sifa.Nimeona kama sifa zipo juu kaka ndege π π