Tangu ateuliwe Paul Christian Makonda kuwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM. CHADEMA kuanzia viongozi mpaka chawa wake mitandaoni mmegeuka kuwa washauri wa CCM.
Tunamuona Lissu huko Marekani kilio ni Makonda, humu JF tunawaona Pro CHADEMA woote ni kilio!
Imekuwaje leo CHADEMA imegeuke kuisaidia CCM isianguke? Iweje CHADEMA leo mnakuwa sehemu ya washauri wa CCM kuhusu namna ya kukiendesha chama chao, ilihali huku kwenu nako yamejaa makandokando lukuki?
Tukiwaambia CHADEMA ni chama la kudandia Matukio mnakuja juu! Sisi wenye weledi tunamuonea huruma Makonda sababu amelazimishwa kuja kuwatetea watesi wake!
Amelazimishwa kuja kukisaidia chama ambacho tayari kimejaa majeraha mwilini hususani mabegani huku Kanda ya Ziwa.
View attachment 2793370