Katika Dunia yenye takribani watu Bilioni 8 leo, zaidi ya watu Bilioni 110 wamewahi kuishi na kufa

Katika Dunia yenye takribani watu Bilioni 8 leo, zaidi ya watu Bilioni 110 wamewahi kuishi na kufa

Hii itukumbushe kuwa hii Dunia tunapita, na itusaidie kupunguza kama sio kuacha kabisa kiburi na kujipa umuhimu.

Waliowahi kuishi na kuondoka ni wengi zaidi ya waliopo leo, na kila mmoja kwa wakati wake alikuwa na umuhimu wake.

Hivyo nafasi ya wewe kuishi leo isikufanye ufikiri kuwa ni ya kipekee sana, utaondoka siku moja na watakuja wengine. Maisha yataendelea vizuri tu bila uwepo wako.

Hii nimekumbushwa na huyu kijana wangu mkubwa, nami nikaona niwakumbushe.

Ncha Kali.
Data zako umeanzia kuchukua za mwaka gani? Je, hao watu ulio wahesabu ni wale watokanao na similizi za kiimani mababu au sayansi? Kama ni kwa mujibu wa imani, je ni imani ipi? Kama ni simulizi za mababu (tamaduni) je ni tamaduni ipi?
 
Death is real , walikuepo manabii na mitume na wote walikufa, watu wenye nguvu kama faraoh, goliath hao waliondoka, kila binadam huumbwa na uhai sasa ule uhai unapoisha ndio kifo chenyewe , kifo ni siri kubwa na fumbo la kiiman ambalo tulipewa, utaelezewa vile ulivoishi duniani na historia yako itasemwa vizazi na vizazi, ishi vile upendavyo lakini ufahamu utaondoka siku moja na utakua ni historia tu,
 
Nimeuguza mtu mpaka kanifia mikononi.
Alikuwa anatapatapa huku anasema anaogopa sana, anasema eti kuna watu wako kwa mbali anawaona wanamsubiri.
Tatizo lake mukishashiba huwa munakuja humu na kukufuru mara oooh thibitisha kama kuna Mungu na blahblah kibao,ila Mungu yupo na anatisha sana na kaburi pia linatisha mno...usiwasikilize wachungaji na manabii waongo wanaopotosha watu kuwa eti Yesu ni Mungu mara sijui mungu ana nafsi tatu
 
Mungu hatishi na wala hataki wewe umuogope, kwanini umuogope??
Kwanini akutishe wakati anakupenda, kama unampenda huwezi kumuogopa bali kuheshimu amri zake.

Heshimu usiogope, ndio maana ni ruksa kusoma chochote kumhusu ili kumjua zaidi, hajakulimit sasa kwanini utishike nae??
 
Daaah nomer sana, Io ina maana siku ya hukumu naweza nikakaa kama miaka kama themanini nikisubiri hukumu yangu, maana yesu atakuwa akidili na watu wengi sana, sijui atahesabu na zambi za katikati ukiwa wasubiri hukumu
 
Mungu wetu ni mwenye kusamehe, yaani utakuta tu ashapotezea dhambi zote na kuanza upya.
 
Kabla ya hao Billion 110 kuzaliwa dunia ilikua haina binadam?
 
Back
Top Bottom