Katika ulimwengu wa kishirikina, nguo yako ni wewe

Katika ulimwengu wa kishirikina, nguo yako ni wewe

Mimi niliwahi kufanyiwa huo uchawi...kipindi hicho nilikuwa kidato cha tano kule karagwe secondary...yaani shule nzima mimi tu ndio nilikuwa naonekana kituko...ilifikia mpaka mkuu wa shule alinibatiza jina la 'truant boy'....na bado nilikuwa najitahidi kuswali sala tano...ila nilifanikiwa kumaliza kwa mbinde...hata shule niliyohamia watu wote waliokuwa wanasoma combination kama yangu wote walifaulu ila mimi tu ndie nilifeli...UCHAWI UPO
Mkuu maisha yako yamefanana sana na yako.
Mimi niliacha kuswali nikiwa form 2 hapo ndio nikawapa upenyo wachawi.
Nilivyoingia form 3 nikawa nayumba sana kimasomo wakati form 1 na 2 nilikuwa naongoza.
Kufika form 5 nilifaulu ila sio kwa viwango vile ambavyo watu walikuwa wanangojea surprise.
Nikaja kupitwa na watu ambao nilikuwa nawafundisha kila siku topics mbalimbali,badae tukaingia advance ndio wenge likaongezeka nikawa sijielewi.
Lakini hadi kufikia hapo bado nikawa sijashtuka chochote ni kama nilifungwa hivi,baadae nikaungaunga nikaingia chuo.
Baada ya kuingia chuo nikawa nakoswakoswa kudisco kila mwaka,kwa mfano unakuta GPA iko chini ya pass mark ukifuatilia unagundua kuna marks za somo moja zimesahaulika hazijahesabiwa.
Nikaja kushtuka niko chuo mwaka wa pili tena kuna jirani ndio alitushtua alimfuata mzee akamuuliza mbona huyu mwanao anakula vizuri milo yote lakini kila siku anazidi kukonda tu bila sababu,yaani nilikuwa kama mgonjwa aliyeugua TB kwa muda mrefu,mabega yamepanda hapo ndio nikashtuka na kuanza kuhangaika kwa wataalamu kuombewa.
Nikaingia mwaka wa 3 chuo nikiwa na afya nzuri na muonekano wenye nuru nikamaliza salama.
Baadae nikaingia mtaani kupambana ikawa vita inaendelea nikishtuka najipanga hivyo hivyo nikatoboa kiasi chake
 
Hata mm nilirudishwa kwa Stail hiyo! Kutoka Canada, ( nilikuja kujua baadae sana )Pia yupo baba wa msanii mmoja wa mchekeshaji maarufu nae wamemtia uchizi kwa ungese huo huo, mzee alikuwa don pale karachi, malay* anakuroga, ndugu wanakuroga, mke anakuroga, utatokea wapi
Ile ishu yako iliisha vipi je alirejea nyumbani
 
Amna mkuu, ukistukia mchongo, unajipanga upya muhimu ni kuusoma mchezo, ukitaka kujua unaishije waangalie sana waliokuzunguka utajua tu. Unaweza kujua upo sawa kumbe ni kinyume chake, meditation inasaidia sana
Tufundishe meditation mzee.Wengine wanasema meditation ni nguvu za giza
 
Habari zenu wakuu natumahi mu wazima wa afya.

Leo nimekuja na hili baada ya kuona matukio yakufanana yahusishayo Nguo.

TUKIO LA KWANZA (1):
Kuna jamaa yangu tulifahamiana nae yeye ni ndugu yake na binamu yangu. Yeye ni Upanga Boy (Mzaliwa wa kata ya Upanga wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam). Back to the story, yeye alikumbwa na tukio (la kishirikina)ambalo lilimfanya awe cha pombe sana, afu michongo sifuri. Ali-turn 40 akiwa home kwao Upanga.

Baada ya jamaa huyo kuwa tatizo katika familia na ukoo kwa muda mrefu. Mwaka 2018 ilikuja bainika kuwa jamaa kalogwa na Shangazi yake wa Singida, Na moja ya " Link " iliyotumika ni nguo (shati) ya jamaa. Jamaa alilitambua shati lake lililopotea siku nyingi akiwa Upanga ila siku hiyo ililiona likiwa Manyoni Singida likiwa limechomwa chomwa sindano, pia likiwa limenyunyuziwa dawa na kufungungwa Power Banks (Ilizi) mbalimbali zenye rangi tofauti tofauti ndani ya chumba ambacho kina giza nene na hakuna mtu uruhusiwa kuingia.

Vyote hivyo vilitosha kuhahakikisha mambo ya jamaa hayaendi, iyo mpaka umauti ulipomkuta 2019 kwenye kilabu kimoja cha pombe maeneo ya vigunguti.

TUKIO LA PILI (2):
Tukio la pili nililisoma humu JamiiForums.

Kuna jamaa yeye ni mzawa na mkazi wa jiji la Dar, Yeye alikuwa ana mpango South Africa.

Alifanya mipango yake kwa siri sana mpaka kufika Mbeya bila familia yake kujua. Kwa bahati mbaya alimtonya ndugu yake hapo Mbeya, Ndugu huyo akawa-informer kwa familia yake ilipo Dar. Mama yake mzazi hakutaka mwanae aende South Africa ivyo ikambidi aende kwa mtaalam amsaidie.

Mtaalam akaagiza Mama Mzazi wa jamaa alete nguzo ya mshikaji afanye mambo. Mtaalam baada ya kukabidhiwa nguo hiyo alifanya mambo kwa ustadi wakutosha.

Uwezi amini bhana yule jamaa ndani ya muda mfupi tu alibadili mawazo "completely" na kurudi kwao Temeke.

Kwako Mshana Jr na wajuvi wengine wenye nyota zenu na mwezi

Tupeni chemistry ya Nguo kwenye ulozi.

Uandishi tuvumiliane tu, hamna namna.
Nguo inatumiwa kwa sample kama sample zingine like nywele,nyayo, choo, dam, nk. Sema nguo inatumika coz ni sample rahisi kupatikana. Sema inatokana na utaalam wa mtu . Wale wakongwe wanachukua kimvuli boss.
 
yes hii ina ukweli. zamani nlikua napenda sana kuwatumia watu random nguo zangu used na viatu as watu wa kijijin ndugu mbali mbali wanaomba...siku nlipigwa stop na dingi hahah na hakunipa sababu. sasa naelewa.
Hivi kumbe vipo na watu tiyari wanajua.
 
Back
Top Bottom