Uchaguzi 2020 Kauli mbiu ya Uhuru na Kazi yampaisha Tundu Lissu

Mshaurini aachane nayo atawainua wenye nayo. Amekosa Slogan hata aokoteze za TANU na CCM? Atasababisha waanze kuvaa sare zao za kuwasha mwenge.

 

Attachments

  • Screenshot_2020-08-19-19-36-25-1.png
    180.8 KB · Views: 1
Hii kaulimbiu aliitumia Mwalimu Nyerere mara baada ya Tanganyika kupata uhuru.

Watu walifurahi sana kupata uhuru wakafikiri kupata uhuru maana yake serikali itawafanyia kila kitu.

Kuna mzungu mmoja wa TANU - sikumbuki vizuri nani, inawezekana Derek Bryceson, akaanzisha kaulimbiu ya "Uhuru na Jasho".

Mwalimu Nyerere akaipenda, akaibadilisha kidogo na kuifanya iwe "Uhuru na Kazi".

https://www.google.com/url?sa=t&sou...FjACegQIARAB&usg=AOvVaw2W7ef6-8Dc1zb76RELjZNn
 
Uhuru upi?

Hivi mwananchi wa nanjilinji kule ukiongelea juu ya uhuru si anakushangaa?

Hilo la uhuru atawapata viongozi wenzie wa pale ufipa
Swali lilipaswa kuwa Uhuru upi? Comment zilizofata zimekuwa conclusive
 
....relax man..., silaha unazijua?
 
Kama mna wanachama wengi kwanini mnaogopa tume huru ya uchaguzi?
Hatujawahi kuwa na tume ambayo sio huru, haya maneno ya kukaririshwa na wanaoshindwa,wakati mwengine muwe mnawauliza wenyeviti wenu wa hizo Sacco's Kama tume sio huru mbona Kila chaguzi mnapata ongezeko la kura za uraisi na wabunge pia wanaongezeka idadi kwanini kusiwe inapungua tu, halafu Kama tume sio huru unashiriki uchaguzi wa Nini?
 
Dhana ya Uhuru zaidi kujiamulia mambo yao wenyewe ni dhana yenye maana pana sana. Watu jamii ya waislam wanaamini nadharia ya Serikali kutokuwa na dini ni nadharia iliyowekwa ili kuzuia ustaarabu wa dini yao kustawi.

Tundu anapaswa kusema bila kutafuna maneno endapo ataendeleza ukandamizwaji huo au kuweka wazi ili apate kura za wenye dini inayokandamizwa.

Huwezi kuwakandamiza watu kwa muda mrefu pasipo wao kuzinduka. Binafsi najaribu kuwaza ni jinsi gani CHADEMA itatatua tatizo hili. Watu wanajifunza asili yao na pale wanapojihisi wanabaguliwa huwa tayari kutetea haki zao na ikibidi ghasia hutokea.

Kwani watu hubadilika na kamwe hawatoridhika kujiona wao no jamii ya daraja la pili iwapo kuna chama kinaweza kuwapa Uhuru wa kujiamulia mambo hao ikiwemo utamaduni wao.
 
wanachama hai wa CCM mpaka jana Ni 18.2 milion hapo bado kura za wapenzi tu ambao sio wanachama, kwani ukiambiwa CCM Ni chama kikubwa na kina mizizi mpaka vijijini ulikuwa unafikiri Nini

Wapinzani wenu wana 22 Million na bado mashabiki wao.
 
Watanzania wote wanajua tume ya uchaguzi ya Tanzania sio huru, labda kama wewe unaishi Burundi. Hilo sio swala la kubishana kabisa sababu liko wazi na halihitaji degree kulifahamu otherwise elimu yako ni ile ya kukalili na sio ya uelewa.

Hatuwezi kususia uchaguzi mkuu sababu ndio utaamua mustakabali wa maisha yetu ya miaka 5 ijayo.

Mwaka huu mwizi asijaribu kuiba kura, atakatwa mkono.
 
Usiseme watanzania sema Wana Sacco's wa chadema
 
Mshaurini aachane nayo atawainua wenye nayo. Amekosa Slogan hata aokoteze za TANU na CCM? Atasababisha waanze kuvaa sare zao za kuwasha mwenge.

View attachment 1542362
Uhuru na Kazi' ndicho watu Wanachotaka kusikia kwa sasa.ingelikuwa wananchi hawataki kusikia juu ya Uhuru wao usingewaona kwenye mikutano yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…