Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Wananchi wanyonge wanyonge maana yake ni wananchi wa kawaida wasiokuwa na mamlaka,uwezo mkubwa wa kiuchumi kiasi cha kuwa jeuri na na kiburi cha kuitiisha serikali mpaka inagwaya yenyewe kuchukua hatua kali endapo mtu mmoja au kikundi chenye mamlaka au nguvu za kiuchumi kitaamua kufanya uovu dhidi ya wananchi wa kawaida wasio na uchumi mkubwa wala mamlaka
 
wanyonge ni wananchi wa kawaida wasiokuwa na sauti wala wa kuwasemea matatizo yao
 
Hii ni sahihi, lkn inawezekana tu kama sanduku la kura linafanya kazi
 
Hili jina limeanza awamu hii ya tano, huko nyuma tuliitana ndugu..."ndugu wananchi". Lkn awamu ya tano tunaitwa "wanyonge".

Wanyonge ni watu ambao hawana cha kuwafanya wenye nguvu (watawala).
Katiba inasema mamlaka yote yatatoka kwa wananchi. Iweje huyu tuliyemweka atuite wanyonge?

Maneno huumba ati! Ukiitwa zoba na ukakubali unakuwa zoba kweli.

Sasa ktk awamu hii ya tano tumeona hili jina linatufanya wananchi tunaonesha unyonge halisi. Mifano:-

- wafanyakazi hawapandishiwi mishahara yao kwa kuwa hawana la kuwafanya watawala (ni wanyonge).

..wakulima wanalima wanafanya kila kitu kwa hela na nguvu zao lkn baadaye wanawekewa masharti, eti wasiuze nje ya nchi (ni wanyonge).

...Tumebomolewa majumba wakati vibali vya kujenga vilitolewa na wao (unyonge)..

..Tunaondolewa kazini eti tuna vyeti fake wakati ajira walitupatia wao (unyonge).

..katiba inaruhusu vyama vingi, watu wanachagua vyama vyao na kushiriki uchaguzi kupitia huko. Wanajiandikisha na kupiga kampeni, kisha wanapiga kura halafu kwasabb ya unyonge tu mazing-zong yanajitokeza.

Hili jina "wanyonge" lipigwe marufuku kutumika.
 
Hawa ccm wanatugeuzia majina tu. Walipoona tumekataa lile la masikini ,wamekuja na Hili la wanyonge. Huwa sitaki kusikia
 
Wanyonge ni waimba mapambio,wanyonge wanaita usiku mchana na mchana usiku,wanyonge wanasema nyeusi ni nyeupe,kwa vile wameamua kwa makusudi kujidai Wana upofu, kwa mtazamo wangu naona hilo jina bado linawafaa Hadi pale watakapo kuwa halisi,kwa kusema nyeupe ni nyeupe na sii nyeusi na kadhalika.
 
Awamu hii neno mnyonge limekuwa sifa!!yaani mtanzania kuitwa/kujiita mnyonge imekuwa ni sifa kubwa, badala ya kuwa laana!!na hiyo yote ni mbinu ya watawala kuona huyu kila kitu ambacho hata ni haki yake ionekane kuwa ni huruma!! Tu kukipata!!
 
Kuitwa mnyonge ni tusi kubwa Sana. Kwa mujibu wa kamusi.

Mnyonge ni mtu hoe hae asiye na mbele. A futureless person. Hawa ndio mtaji wa wanasiasa na ndio uamua hatma ya maisha ya watu wote katika nchi.
 
Akili zimewarudi, sasa mmeanza kuamka... usiku utapokwisha!
 
Jibu hii kwanza kama wewe si mwiba mchungu

 
Wanyonge kwenye nchi huru...napenda maraisi wa Marekani “American citizens “hii mijitu tumeichekea vya kutosha kuna siku bila ya kujali itikadi tutaifurusha
 
Wanyonge wamenyongwa mpaka wamenyongeka wao ndio wanaishi zaidi ya mashwetani japo walengwa walikuwa ni matajiri.
 
Uchaguzi umeisha nitakusemea kwa litundulissu likushitaki kwa kughushi ilani yake. Ila lenyewe lilisema "huyu magufuli mtakatifu wetu anayejiita mtetezi wa wanyonge". Huu usemi ni wa kawaida, hulka ya Watanzania, sioni kama una shida yoyote.

Ukimwita sugu mheshimiwa au pter msigwa mchungaji haina maana kwamba ni mheshimiwa au ni mchungaji; ndivyo tu tulivyo Watanzania. Kamanda, na wewe tafuta kibwagizo chako huru usipoteze muda wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…