Hivi unafahamu kuwa Sri Lanka wala si demokrasia ndio hiliyo wafanya wandamane bali hali ngumu ya maisha ndio iliyopelekea watu kutokujali chochote kile . na wala sio ishu ya demokrasia unayoeleza wewe maana porisi wa Sri Lanka wameuwa waandamanaji wengi Sana , wajeruhi waandamanaji wengi Sana , na wametumia njia zisizo za kidemokrasia kuzuia maandamano kwa kiwango kikubwa swali la kujiuliza je wewe , Mimi na sisi WATANZANIA tunaudhubutu wowote wa kufanya maandamano yatayoleta matokeo chanya katika ukombozi wa taifa hili bila kujali ni wangapi watakufa ama kujeruhiwa katika maandamano je huo utayari tunao? Maana hii ndio ilikuwa Siri ya mafanikio ya Sri Lanka na wala sio demokrasia unayozungumzia wewe hapa. Bila dhamira wala uthubutu kamwe hatuwezi kuleta ukombozi kila siku tutaishia kumlaumu Mwalimu Nyerere ambaye amekwisha kufa hawezi kufufuka kuja kusahihisha mahali alipokosea hii itakuwa ni kazi bure tu.