Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Nimesemaje nyinyi wote mna-base upande mmoja Ila pande zote mbili zina makosa kwa kiasi chake, raia kataka kuonekana yeye ni mwamba mbele ya mwanajeshi kwa kutaka kumvimbia, hivi unanielewa lakini nakwambia Mimi mifano hai ninayo kuna madogo wanatukana wanajeshi kwa dharau kwamba wanajeshi hawana chochote soma hata comments za humu utaelewa, kwa hio hio mentality raia anatembea nayo anasubiria akutane na mwanajeshi yoyote amuanzishie vurugu popote pale na mwisho raia watamtetea raia na kumuona mwanajeshi hafai hio sio sahihi kabisa,
 
Sio kweli, hakuna Askari anaepiga raia unreasonably huo ni uongo, ukijikuta umepigwa na Askari tambua there's a reason behind hawezi akatoka Askari huko akaja kukupiga tu hio haipo, kwa hio hapo nakupinga
Kwahiyo hizo reasons,ndiyo zihalalishe askari anipige makofi?
Huoni atakua amenivunjia heshima?
Unategemea namimi ambaye siyo askari,nifanyaje nikipigwa makofi,nicheke au nijilinde kadri ya uwezo wangu?
Kwanini kama nimekosea,nisipelekwe mbele ya vyombo vya sheria?
Piga kofi,namimi nijilinde,kama ambavyo sikutegemea ntapigwa kofi,nawewe uwe tayari kwa usichokitegemea kutoka kwangu.
 
Duuh...! Sasa ona huyu mjeda?. Hapo nani kapata hasara sasa?. Amewaachia tu mzigo tu watoto, ndugu na jamaa wanaomtegemea. Kwani angekutumia hekima tu angepubgukiwa nini?. Sidhani kwamba huko jeshini wanafundishwa kuwa tu wababe tu hata mitaani
 
Iyo baa naijua inaitwa igole huyo pot anajulikana sana baa zote kwaanzia ukwamani mpaka kanisani kwa mwamposa ninacho shangaa wanaacha kulewa kule dar service wanakuja huku chini ukwamani kutafuta malaya achawaone chamoto
Kwa hio kwa mtazamo wako ni haki kumuua kwa sababu kaja maeneo hayo? Kwanini mnakua na mentality za kijinga ni wapi pamewekwa mpaka wa mwanajeshi kutembea kwamba mwanajeshi kutembea mwisho hapa?
 
kwangu mimi bosi wa jeshi na huyo kijana wa bajaji wote wajinga kwenye mambo kadhaa,
1. hawakulelewa vyema kama wanaume wa kiafrika
2. kuna wakati kwenye maisha ni lazima kutumia akili za kuzaliwa
3. kuna wakati lazima utumie akili ya darasani
4.kuna wakati utumie elimu ya kitaa,
-mimi ningepigwa makofi ningeondoka eneo la tukio kama mjinga lakini ningepanga ambush bila huyo bosi mlevi kutegemea, huwezi pambana vita ya moja kwa moja na mtu mwenye makuruta wengi nyuma yake lazima ucheze kama kinjekitile lazima uvizie kwa akili na usionekane kama kweli huyo bosi mjinga alipora haki zako.
-lakini pia ningekua bosi wa jeshi ningetumia vijana wangu kudeal na dogo asie na nidhamu kihuni sababu nipo kitaa maeneo ya wahuni swala la kutumia cheo maeneo ya wahuni ni uzuzu.
 
Huyu dogo kama wamemdaka,basi wahesabu kapoteza
 
Kaka wala usipoteze nguvu zako bure. Hao ni waonevu na ilo linasalia kama lilivyo
 
Nimesema pande zote zima makosa kwa kiasi chake, tatizo wengi wenu mnaegemea upande wa raia kusema kwamba raia kuua mwanajeshi yupo sahihi, hio sio sawa huo ni ujinga uliopitiliza na haikubariki hata kidogo
 
Kuna wanajeshi wawili walizoea kuendekeza ubabe kwenye baba moja Sinza. Kuna siku waliingia cha kike kwa black belt mmoja ambae kwa muonekano walidhani wanammudu.
Jamaa aliwanyoosha wote wawili halafu akaondoka zake mdogo mdogo hata hakimbii.
Wajeda kwa aibu wakainuana pale wakaita bajaji wakaondoka kwa aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…