Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 349
- 805
Inasemekana ( kwa aliyenipa Taarifa Kamili kuwa ) Dereva Bajaji jana Usiku katika Baa Moja maarufu iliyo kwa ndani ( Mafichoni kidogo ) mkabala na Petro Station ya PUMA Kawe alipishana Kauli na Mwanajeshi ( tena Mkubwa wa Cheo cha Kanali ) kuhusu Kuzibiana njia ya kupita.
Ambapo Afande Kanali alikuwa Kapaki Gari lake lililokuwa limezuia njia kwa mbele na Dogo ( Dereva Bajaji ) kuhoji kwanini Afande aliziba njia hali iliyomkwaza Afande ( wa Cheo cha Kanali Muro kama sijalikosea Jina lake ) ambapo Afande Kanali akatoka ndani ya Gari lake na Kumzaba Makofi Dereva Bajaji huyo.
Kisha nae ( Dereva Bajaji ) kwa Hasira akaamua kwenda kuchukua Bisibisi Bajajini Kwake na kuja Kumchoma nayo Afande Kanali upande wa Moyo hali iliyomfanya akimbizwe Lugalo Hospital kwa Matibabu na Umauti kumkuta huko huko Wodini.
Pole kwa wafiwa. Marehemu alikosa hekima lakini. Ukishakua kwenye vyombo vya usalama haimaanishi uwe mtu wa shari pasipo na misingi yoyote. Ukivaa kombati haimaanishi una mwili wa chuma tayari. Bado mwili wako ni wa damu na nyama.