KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE: Tundu Lissu apewa kila anachohitaji gerezani

Unaelewa hata ulichokiandika kweli?
 
Sasa hapa mh rais anaingiaje, kwamba haki yamfungwa inatolewa na rais ,hii ni haki ambayo ipo kwa mjibu wa sheria sio takwa la mtu yoyote, hata rais akifungwa lazima pata haki hizi
 
Elewa kuwa wewe ni Mpumbavu na sio Mjinga. Raisi sio hakimu, alichokipigania Lisu ni haki zake zilizopo kisheria, Rais hagawi haki chawa wewe.
Mbona hakupewa hizo haki kabla ya Rais kusikia manyanyaso yake?
 
Sasa hapa mh rais anaingiaje, kwamba haki yamfungwa inatolewa na rais ,hii ni haki ambayo ipo kwa mjibu wa sheria sio takwa la mtu yoyote, hata rais akifungwa lazima pata haki hizi
Ndio amiri jeshi mkuu
 
Na huu hasa ndio ugonjwa wa Tanzania, kuamini kila kilicho haki yao ni msaada kutoka kwa mtu mmoja.

Hakuna sifa yeyote kwa mama kwa hili la Lissu kupata kile alichopaswa kukipata kwa haki yake toka awali, if anything lawama zinapaswa ziende kwa mamlaka husika juu ya kwanini Lissu alipokonywa haki yake hapo awali
 
Hii ndiyo ile kanuni ya kutengeneza tatizo kisha litatue upate sifa, hapa umetuhakikishia kuwa Samia ndiye alikuwa anamnyima hizo haki sasa amemrudishia, mwambie basi na hii kesi ya kujitungia aliyombambikia Lissu aifute ili azidi kuapa ujiko, sawa sawa?
 
Hahaha so mama apewe sifa sio? Zimezidi sana sasa awe tu mtume mwingine yaishe!
Chezea Marekani na Bunge la Ulaya wewe!!! Sasa ukijiuliza kwa nini walimnyima haki zake? Hawakuwa wanajua Na nani aliwatuma?
 
Itakuwa wamestuka kuona anataka kujitetea mwenyewe awakutegemea.

Lissu sio push over kwenye kesi za kisiasa, wameona ohoo kasheshe; si umeona alivyowaburuza wanasheria wa serikali kwa muda mfupi tu.

Halafu haki za mfungwa sio hisani ya raisi. Ingekuwa huyo raisi kakerwa ukandamizaji wa haki za wafungwa.

Kuonyesha kukerwa angemtimua mkuu wa gereza husika, mkuu wa jeshi la magereza na waziri wa mambo ya ndani. Kwa treatments zao mbaya kwa wafungwa.
 
Huyu mama anaeshidwa hata kutoa watu kafara kujisafisha hapo mkuu wa Magereza angeondoka waziri wa Mambo ya ndani angeondoka Mama Tungejua kwamba hakuwa na mkono wake
 
Haahaa huyo Samia alikuwa wapi muda wote huo?
 
Nchi nyingine waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa gereza wangefukuzwa fasta...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…