Huyo siyo Mnigeria wala hawajawahi kuwa Mnigeria, ni Muingereza, amezaliwa Uingereza, kaishi, kasoma na kulelewa uingereza, ameolewa na Mzugu muingereza.
Huyo ni Muingereza - mweusi, siyo Mwafrika.
Watu weusi wanapofanikiwa nchi za watu mnakimbilia kuwafunika Uafrika na kuanza kujinasibu kupitia wao ilihali uafrika wao siyo uliowasaidia bali mifumo ya nchi hizo.
Wakitoka Waafrika walioishi nchi za Ulaya na Marekani kuja huko Afrika kukamata fursa na hata uongozi wa juu, huwa mnawakana si wenzenu na mnawaita vibaraka wa mabeberu.
Mayweather alishawarekebisheni kwamba, yeye siku zote atabaki kuwa black-american, siyo african-american.
Weusi siyo uafrika wala baba au babu siyo wanao dominate asili na mifumo ya maisha ya mtu, mtu ni matokeo ya culture anayoiishi, siyo culture ya mababa au babu zake ambayo yeye hajawahi kuiishi.