Kero ya kukuta mtu kakaa kwenye siti yako ya dirishani kwenye Bus.

Kwani tatizo liko wapi, si umwambie akupishe tu. Akikataa muite Konda au wahusika waoneshe tiketi yako waambie na kinachoendelea.
 
Jinga ni wee ambae unashindwa kumuambia akupishe ukae kwenye seat yako.
Poleeeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nimekumbana na changamoto ya hivyo kwenye Azam marine boat wakati nasafiri kwenda Zanzibar lakini pia wakati nasafiri na ATCL kwenda Mwanza.

Seems Watanzania tunapenda sana kukaa seat za dirishani, yaani mnaweza hata kugombana katikati ya safari Kwa mtu kukaa seat yako ya dirishani πŸ™Œ

Binafsi nikikuta umekaa seat yangu ya dirishani hata siangahiki kukutoa, najua bila kukuta nimekata hiyo seat obvious ungekata wewe
 
Mwingine anafanya makusudi anajua utamuonea aibu...
 
Mama enyewe kule UK alipambabia siti ya dirishani.,, mimi ni nani nikuachie siti yangu
Ile siti ya dirishani ilikua ya Ruto, sema Ruto akaamua kumuachia Dada yake maana anajua kua wanawake by nature ndiyo wanapenda sana siti za dirishani haijalishi hata kama kawa Rais!!
 
Pisi zenyewe ndo kina wewe zenye akili kuchukua namba kwanza πŸ˜„
Huwa sihangaiki nikikaa na pisi...natoa earphone.

Ila kuna trip ya Mwanza 2013 siwezi sahau mtoto wa Kairuki pale dah Konda ashukuriwee heheee Konda nilimpa Kazi akaitimiza haswa
 

Niliikuta pisi kali sana imekaa kwenye siti yangu, nikaiuliza kistaarabu na yenyewe ikanijibu kistaarabu kabisa siyo siti yake.

Kwa ule ustaarabu wangu akafikiri hili nalo ndo wale wale, akanielekeza siti yake huko nyuma nikamwambia haiwezekani!! Sipendi siti za nyuma huko thus why nimechagua hapa.

Akapandisha sauti kwa kutoa maneno ya kejeli kunilainisha nikubaliane nae, nikamsikiliza alipomaliza nikamwambia kistaarabu kabisa kuwa "dada, ulikata siti kwa pesa yako, uhitaji wako, matumizi yako na chaguo lako, nami pia hivyo hivyo. Tuheshimu tuliyoyafanya." Akanyanyuka kimya kimya!!

Siangaliagi sura lakini pia afadhali tungekuwa siti za pamoja! Imagine aje akae siti namba tano eti nikakae siti yake namba 33 huko!!

She was not serious kwa kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…