Kamati kuu ya Chadema kwa kauli moja imeazimia kushiriki ktk sherehe za Uhuru zitakazofanyika Mwanza kitaifa.
View attachment 1284723
Waziri Kange Lugola, AGP Silo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Polisi wa mkoa wa Mwanza na vyombo vingine vyote vya Dola vinavyo husika, please! kuweni makini na kundi hili la CHADEMA, hawaji bure watakuwa kuna kitu wamekitengeneza ambacho kitawasaidia wao kuuonyesha ulimwengu jinsi gani serikali yatu ni serikali ya kidikteta inayo wavunjia haki wapinzani. Wanataka pics na clips za damu ya watanzania inayo mwagika ili wapate sababu ya kuuambia ulimwengu; "mnaona sasa! Tuliwaambia kuwa huyu mtu ni Dikteta," ili wapate sababu za kumsulubu Rais wetu in The Hague.
Rais Magufuli mambo unayo yafanya kwa watanzania hivi sasa, haijawahi kutokea katika Third World Country kama yetu. Tukifanikiwa sisi tutakuwa mfano kwa nchi nyingine za Afrika na hivyo kuwafanya wazungu waonekane kuwa ni kichaka.
Juhudi hizo unazo zifanya Mweshimiwa wazungu haziwapendezi hata mara moja. Umekuwa ni tishio kwao. Na ndiyo maana wanatafuta kila njia kuzuia ili sisi tusipate maendeleo unayo kusudia. Na kwa vile tuna watu miongoni mwetu ambao maslahi yao ni bora kuliko maendeleo ya watanzania wenzao wako tayari kuwaridhisha mabeberu wao kwa kuwatumikia kile wanacho kitaka ili wao nao wapate kile wanacho kizarajia, nacho ni madaraka. Kwa uroho wao wa madaraka wako tayari kuiuza nchi yetu na sisi pamoja.
Hawa ndiyo akina Mobutu Sese Seko wa Zaire na Blaise Compaoré wa Burkina Faso wanao kula njama na Mabeberu ili kuwaondoa Marais wa nchi zao wanao fanya kazi nzuri ili wao washike madaraka na hivyo kukamilisha malengo ya mabeberu wao.
Nafikiri watanzania wenzangu mmeyasikia ya Malim Seif wa NCC Wazalendo aliyo yatoa hivi juzi juzi ya kuhusiana na wizara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Alli. Hawa watu wanatafuta kila njia ili kutuchonganisha sisi ili tupigane vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hawako tayari kushindwa. Wako radhi tukose wote.
Watanzania tumlinde Rais wetu kwa hali na mali. Tukichfuana wenyewe kwenyewe kwa visenti watakavyo tupa, tusifikiri tutakuwa salama. Na hakuna nchi ambayo iko tayari kutupokea sisi kama wakimbizi. Wazungu wana hali mbaya sana!