Kesi ya Mbowe: Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi atajwa kumtumia pesa Mtuhumiwa

Kesi ya Mbowe: Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi atajwa kumtumia pesa Mtuhumiwa

... issue ni lego la miamala hiyo ni lipi? Hope mahakama itaamua kwa busara!
Wewe unafikiri lengo la miamala ya kutoka kwa Mbowe ilikua na lengo gani? Yeye alitaka watu wa kumlinda (VIP protection), hivyo kuwasaidia pesa hawa watu waweze kutatua baadhi ya matatizo kabla hawajaanza kazi rasmi, haikua jambo la ajabu.
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi,huyu shahidi si ndiye aliyeingia mitini mara ya kwanza alipoitwa?Nahisi ameshurutishwa!
 
... kwa hili Airtel haliwahusu sana; wanaweza kujitetea. Orodha ya miamala wao waliitoa kama walivyokua instructed na barua ya polisi ambao walikuwa wanataka miamala among specific numbers so, (Airtel) wasingeweza kutoa miamala ambayo hawakuulizwa!
Kumbe hujapitia hiyo cross examination, kuna miamala 19 ambayo ilifanyika kwa Bwire ikiwemo ya watu ambao barua ya maombi haikuhitaji, ni miamala ya mh. Mwinyi tu ndiyo imeondolewa. Mawakili wa utetezi wameanzia mbali kuhakikisha wanafunga mianya yote kabla ya kufika kwenye hoja ya mh Mwinyi. Labda kama ni mvivu wa kufuatilia au ni mzito kuelewa logic za maswali ya mahakamani.

CcBwana PGO
 
Kwani alituma wakati gani akiwa bado yuko uraiani au akiwa tayari ameshitakiwa?
Kwani Mbowe alituma wakati gani? Unafikiri Mbowe alituma wakati Bwire akiwa ameshitakiwa? Ukiwa neutral utakuta unapata ufahamu sana kwenye haya mambo. Jiweke mbali na huko uliko jing'ang'aniza, uwe huru, huwezi kuwa mzito kuelewa.
 
Inawezekana alikua anamsaidia commando wake baada ya kuwa hana kazi, ukichukulia yeye alikua ni waziri wa ulinzi. Kosa ni hao upande wa mashitaka walioziondoa hizo transactions, kitu kinachoonyesha nia yao ni kuwafunga kwa hila tu. Hakukua na sababu ya kuondoa baadhi ya miamala, kama ushahidi wao ni genuine.
Excellent observations!
 
Back
Top Bottom