Napinga hii hoja, kujitoa mapema kwenye hii kesi kwa style ya kususa ndio kutawapa jamhuri sababu ya kupandikiza propaganda zao ambazo mpaka sasa zimefeli, kesi ibaki mahakamani mpaka dakika ya mwisho, na ikibidi kama hukumu itakuwa mbaya wakate rufaa mahakama ya rufani.
- Wacha ulimwengu unaofuatilia hiyo kesi uendelee kujionea kila hatua ya uozo wa mahakama zetu na majaji, wawakilishi wao wapo wanahudhuria hiyo kesi, kitendo chochote cha kujitoa utakuwa ni utoto usiokuwa na maana yoyote.
Kila jambo linalofanywa huacha precedence iwe mbaya au nzuri, kususia kesi mahakamani itaonekana jamaa ni wahalifu kweli na wataitumia karata hiyo kuwajaza ujinga wale wasiojitambua na watawaamini, kwamba Chadema ni chama cha vurugu, hakuna kuitoa kesi mahakamani, wacha waendelee kujivua nguo mpaka dakika ya mwisho, wenye akili zao wanaujua ukweli.