Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

Umeona kwenye ndoto ya saa ngapi
Namimi nikaote kwa muda uho😂
 
Nimekuelewa sana mkuu leo nachokiona ni kujaribu ku test kumbukumbu za shahidi na kufanya ajipinge.
Binafsi leo naona kama shahidi anawekwa kwenye angle mbaya jambo ambalo si zuri. Nilitamani a stick kwenye kile jana amesema. Jambo nililoogopa zaidi ni swala la sumu, hili nisilisema maana nimeona ameenda oof track kwa uelewa wangu, am very sad
 
WASOMAJI WA KESI INAYOENDELEA * ANGALIZO
 

..suala la jaribio la sumu dhidi ya Tundu Lissu lilikuwa halina msaada wowote kwa Katuga na alipoteza muda kulishadidia.

..Jaji anaposema Wakili muongoze shahidi mara nyingi huwa analenga tukio kama lile.

..Wakili awe wa utetezi au mashtaka anatakiwa asimame ktk mstari na maswali yake yajielekeze ktk shauri lililopo mahakamani.
 
Muda wa John Heche unakaribia sasa mzee wa kazi yaani yeye kazaliwa anajiamini hakuna wa kumtisha apo mawakili wajipange sana

Kwaiyo Shemeji Heche
sasa atazitapika tone tone zetu

MUNGU ni. Mwema uyu ngoja kwanza mh Lissu amalize kucheka na Shemij wake❗️

kesho
Mh Lissu hatukabidhi uyo
Shemeji yake
Tujue pesa kaweka wapi na nguvu ya kuwafukuza Wanachama kaitoa wapi🤠🤠
 
MAHAKAMA IMERUDI TOKA MAPUMZIKO.

MAHAKAMA INAREJEA / MAJAJI WANAINGIA.

Mahakama ipo kimya kwa muda.

Majaji wanateta kidogo.

Mawakili wa Serikali wapo tayari.

Lissu yupo tayari.

Shahidi wa tano yupo tayari.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, kolamu inabaki kama ilivyo. Tupo tayari kumsikiliza shahidi namba 5 wa upande wa utetezi.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa unasemaje?

Lissu: Nipo tayari, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Palikuwa na jambo moja sasa. Mara ya mwisho tulireserve kuhusu wale mashahidi wengine.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nakumbuka mlichokielekeza kwamba nianze na hawa mashahidi kwanza, halafu nikikamilisha ndiyo tuendelee na uamuzi.

Kwa hiyo, tuendelee na mashahidi hawa kwanza.

MAJAJI WANATETA.

Jaji Ndunguru: Upande wa mashitaka?

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, tunaungana na alichosema Mshtakiwa. Tuendelee na shahidi, baada ya hapo Mahakama itasoma uamuzi.

MAJAJI WANATETA.

Bado Majaji wanateta. Kuna wingu zito hapa, wacha tusubiri tuone.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1

Jaji Ndunguru: Basi tumekubaliana tutaendelea na shahidi aliyepo.

Na leo, baada ya kusikiliza shahidi aliyepo, tutasoma huo uamuzi, kusudi pande zote mbili zijue status za hao mashahidi.

Lissu na Mawakili wa Serikali: Sawa.

Jaji Ndunguru: Shahidi, jina lako?

Heche: Naitwa John Wegesa Heche.

Jaji Ndunguru: Umri wako?

Heche: Miaka 45.

Jaji Ndunguru: Unaishi wapi?

Heche: Tarime/Mwanza.

Jaji Ndunguru: Unafanya shughuli gani?

Heche: Makamu Mwenyekiti CHADEMA.

Jaji Ndunguru: Dini yako?

Heche: Mkristo/Msabato.

Heche: Mimi, John Wegesa Heche, naapa mbele ya Mahakama hii tukufu kwamba ushahidi nitakaoutoa utakuwa wa kweli, ukweli mtupu. Mungu nisaidie.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Jaji Ndunguru: Utamuongoza?

Lissu: Nitamuongoza.

Lissu: Shahidi, umesema wewe ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Umekuwa kwenye nafasi hiyo tangu lini?

Heche: Nimekuwa Makamu Mwenyekiti Bara (Tanganyika) tangu mwaka jana, mwezi Januari 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anapatikanaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anapatikana kwa kuchaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa chama chako anatumikia nafasi hiyo kwa muda gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anatumikia nafasi hiyo kwa miaka 5.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo nafasi nani alikuwa mtangulizi wako?

Heche: Waheshimiwa Majaji, kabla yangu nafasi hii alikuwa Tundu Antipas Lissu, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Taifa.

Lissu: Kabla ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, ulikuwa kwenye nafasi gani?

Heche: Kabla ya mimi kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, nilikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Kamati Kuu ni chombo cha namna gani?

Heche: Kamati Kuu ndiyo chombo cha utendaji cha Baraza Kuu.

Lissu: Wajumbe wa Kamati Kuu wanapatikanaje?

Heche: Mwenyekiti wa Chama Taifa, Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu ambao ni Bara na Zanzibar, wanaochaguliwa kwa nafasi zao.

Wenyeviti wa Mabaraza:

Mwenyekiti wa BAWACHA,
Mwenyekiti wa BAVICHA,
Mwenyekiti wa BAZECHA.

Wenyeviti wa Kanda.

Kuna Kanda 10, ambazo 8 kutoka Bara na 2 kutoka Zanzibar.

Wajumbe wanaochaguliwa na Baraza Kuu la Chama.

Na wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa.

Lissu: Kwa ufahamu wako, wajumbe wa Kamati Kuu ni wangapi?

Heche: Kuna watano wa Baraza Kuu, watano wa Mwenyekiti.

Kuna 10 wa Kanda.

Kuna wanaoingia kwa nafasi zao 6.

Na wajumbe 3 ambao kwa nafasi zao.

Na kuna Sekretarieti ambao siyo wapiga kura.

Kwa hiyo, wapo jumla 29.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji majukumu ya Kamati Kuu.

Heche:

1. Kusimamia Sekretarieti ya Chama Taifa, ambacho ndiyo chombo cha utendaji wa kila siku.

2. Kufanya vikao na maamuzi ya vikao ya mambo yanayojitokeza mara kwa mara.

3. Kusimamia shughuli za utendaji wa chama.

4. Kupitia mihutasari ya nyuma na kuidhinisha.

5. Kupanga vikao vya Baraza Kuu la Chama.

6. Kupitisha ajenda zinazoenda katika Baraza Kuu la Chama.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, umekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kwa wakati gani?

Heche: Nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama kwa miaka 15, tangu mwaka 2011.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Leo hakuna jipya
Mh Lissu na Shemeji yake wapo kwenye kama matani yenye ukweli

Ngoma nzito kwanzia Kesho au kesho kutwa pale Heche wakikutana na kina Katuga nk✍️
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 2.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nafasi zingine za chama ulizowahi kushikilia.

Heche: Nimekuwa Mwenyekiti wa Tawi wa CHADEMA Students Organization (CHASO).

Lissu: Tawi gani?

Heche: Tawi la SAUTI Mwanza, tangu 2006 hadi 2009.

Lissu: SAUTI ni kitu gani?

Heche: St. Augustine University of Tanzania.

Lissu: Nafasi nyingine?

Heche: Nimekuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa (BAVICHA), mwaka 2011 mpaka 2014, nafasi ambayo ilinipa ujumbe wa Kamati Kuu.

Nimekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, mwaka 2016 mpaka 2019, nafasi ambayo ilifanya niwe Mjumbe wa Kamati Kuu.

Lissu: Kanda ya Serengeti ni kitu gani?

Heche: Ni Kanda yenye mikoa mitatu: Mkoa wa Mara, Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa Simiyu.

Nimekuwa Diwani wa Tarime.

Lissu: Nilikuwa nakuja huko, usinitangulie.

Heche: Sawa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nafasi yako ya uongozi nje ya chama.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nimewahi kuwa Diwani wa kuchaguliwa katika uchaguzi mdogo wa marudio mwaka 2008.

Baada ya Mbunge na Diwani kufariki, niligombea na kuchaguliwa kuwa Diwani wa Tarime Mjini.

For the record, nilichaguliwa nikiwa bado mwanafunzi wa chuo kikuu.

Lissu: Chuo gani? (Usidhani kwamba watu wanafahamu mambo yenu.)

Heche: Nilikuwa bado mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agustine, Mwanza.

Vilevile, nimekuwa Mbunge kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020.

Lissu: Kuna nafasi zingine za uongozi ambazo ungependa Majaji wazifahamu?

Heche: Nikiwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa, nilikuwa Mjumbe wa Bodi wa International Democratic Union, tangu nikiwa Mwenyekiti wa Vijana mpaka nilipomaliza.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Kitanzi kimekaribia

Uyu anaweza kufungwa Maisha Sababu kosa lake lipo kwenye kukusudia kutenda Uhaini limebaki apo✅️

Kama Jamhuri isingeshindwa kwenye kesi Mahakama y Rufaa kwenye ule mpango wa kuongeza Ushahidi mpya wa Mo29

mh Lissu yumkin angenyongwa kwa %80
 

..kivipi?

..kitu gani kinathibitisha kukusudia kutenda uhaini?

..hata Dudu Baya juzi alivyotoka kwa Katambi aliposti anakwenda kukinukisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…