Kesi ya Uhaini dhidi ya Lissu: Brenda amaliza kutoa ushahidi Mahakamani Septemba 9, 2026

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 3.

Lissu: Kwa vile, Shahidi, nimekuita uje kunitolea ushahidi katika kesi hii, naomba uwaeleze Waheshimiwa Majaji mimi ni mtu wa aina gani kwa unavyonifahamu wewe.

Heche: Waheshimiwa Majaji, namfahamu Mwenyekiti wangu kama:

  • Mtu mwadilifu.
  • Mtu mkweli.
  • Mzalendo anayeipenda nchi hii.
  • Msomi mzuri wa sheria.
  • Mwanademokrasia.
  • Mtu anayependa kushindanisha mawazo kwa hoja.
  • Mtu ambaye amekuwa Mbunge na miongoni mwa wabunge bora kabisa kabla ya mimi sijaingia Bungeni, na nimefanya naye kazi Bungeni.
  • Mtu jasiri; kwa lugha yetu ni mpiganaji wa kweli.

Kwa sisi watu tunaotokea Tarime, tumemfahamu, hasa mimi nimemfahamu, wakati anakuja kumtetea Marehemu Chacha Wangwe wakati anafungwa kisiasa.

Na kuja kutetea wananchi wa Nyamongo, wamiliki wa maeneo ya asili ambayo yalipatikana dhahabu na wakawa wanahamishwa, kama akina Marehemu Agustino Sasi.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Heche Hana baya hawezi kusumbuliwa na mawakili wa mchongo

Tatizo hajui Sheria
So tegemea vituko kutoka kwake sio chengine
Pale sio jukwaa la Siasa kukusanya tone tone ✍️
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 4.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa nini umemtaja Mzee Agustino Sasi? What so special?

Heche: Mzee Agustino Sasi alifungwa miaka 30, na wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja kupitia CCM.

Alifungwa miaka 30 kwa kesi hizi za uonevu, za kunyang'anywa mali, ikiwemo ardhi yake.

Waheshimiwa Majaji, baada ya kutoka gerezani, Mzee Sasi alijiunga na chama chetu na akachaguliwa kuwa Diwani.

Wakati mimi naingia kwenye Baraza la Madiwani, nilimkuta yeye Diwani wa kipindi cha pili.

Lissu: Umemtaja Marehemu Chacha Wangwe na Marehemu Mzee Agustino Sasi.

Waeleze Waheshimiwa Majaji watu wengine ambao niliwatetea katika matatizo yao.

Kama unajua idadi, sema.

Heche: Waheshimiwa Majaji, siwezi kukumbuka idadi, ila ni zaidi ya 20 ambao aliwatetea, nakumbuka:

  • Marehemu Chacha Wangwe.
  • Marehemu Agustino Sasi.
  • Na wazee wengine.

Lissu: Sasa, Shahidi, nimekuita uje utolee ushahidi katika kesi ambayo nimeshitakiwa nayo.

Nataka uwaeleze Majaji, palikuwa na kitu gani tarehe 03 Aprili mwaka jana?

Heche: Waheshimiwa Majaji, tarehe 03 Aprili mwaka jana palikuwa na kikao cha watia nia/aspirants, wanaotaka kugombea kupitia chama chetu.

Lissu: Lengo la huo mkutano wa watia nia lilikuwa ni nini?

Heche: Ilikuwa ni kuwaeleza kuhusu msimamo wa chama kuwa bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Nia ilikuwa ni kuwaelimisha kwanini chama kimechukua msimamo huo uliowekwa katika vikao vilivyotangulia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hivyo vikao ambavyo vilikuwa vimetangulia ni vikao gani na tarehe zake, kama unakumbuka?

Heche: Waheshimiwa Majaji, mimi kama nilivyosema, nimekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.

Nilikuwemo katika vikao baada ya uchaguzi wa Vitongoji/Vijiji na Serikali za Mitaa 2024 kuharibiwa kwa nchi nzima, kwa wagombea wa CHADEMA kuenguliwa massively kwa nchi nzima.

Karibu asilimia 80, kwa watu kuuawa kama Manyoni, mgombea wetu kuuawa, na Dar es Salaam hapa.

Lissu: Kitu gani kilitokea?

Heche: Chama kilikutana chini ya Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe, tarehe 03 Desemba 2024.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Shahidi CHUMA cha pua anamaliza ngwe ya mwisho kuyagalagaza maCCM mahakamani leo saa 8 mchana.
 

..Heche ni " character witness " wa Tundu Lissu.

..Ndio maana Heche anaeleza jinsi anavyomfahamu Lissu ni mtu wa aina gani.

..sasa Katuga akianza kumuuliza Heche masuala yasiyohusiana na alichokieleza, kwa mfano amuulize kuhusu tonetone, atakuwa hausaidii upande wa mashtaka.

..Brenda Rupia kazi yake ilikuwa kuieleza mahakama kwamba Lissu hakuita vyombo vya habari virushe hotuba yake. Katuga alitakiwa ambane, na amlazimishe, Brenda kusema kinyume na hivyo.

..Heche anapomuelezea Lissu kwa mwanga mzuri anajenga utetezi kwamba Lissu ni raia mwema, mtetezi wa watu, mpinga mifumo kandamizi, na sio mhaini.
 
Hiyo shemeji heche sijaelewa nani kaoa kwa mwenzie apo

Heche Dadake ndio Mke wa Mwenyekiti wa Chadema mh Lissu

Ndiomana kwasasa ndani ya Chadema Mh Heche yupo juu na anaogopwa na wenzake pale Chadema

Si umeona upendeleo yeye kuwekwa baada ya wenzie ili Shemeji Heche ajifunze kwa wenzake βœ…οΈ

Ukiwa na Dada mjini ni fursa πŸ˜‚
 
We kweli ni bwege unaleta ushabiki km zuzu ktk mambo usiyoyaelewa, sheria siyo ushabiki, huyo demu wenu ni mtupu hakuna anachojua, amepigwa pini hawezi kujua maswali ya wakili mkuu msomi Katuga. Kila kitu hajui sasa ameenda kutoa ushahidi au kuuza sura. Huyo kibaraka wenu mhaini ana hali mbaya, akifijiri ni yeye tu ndiyo anajua sheria ila wako mapapa zaidi yake. Akitoka hatarudia kuchezea sheria za nchi kisa kasoma sheria.
jum
Sawa mkuu uwe unatoa updates, sio uzi uanzishe wewe updates anatoa mwingine.
singi
 
ccm hamna akili kabisa
 
Hivi jamani hakuna namna tukalitoa hili jizi na lipenda rushwa hapa jamii forum?

Hii Jamii forum jukwaa huru
Watu wako huru ndio Demokrasia yetu ndani ya Chadema au CCM kwako ipo wapi???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…